WAZIRI MKUU AFUNGA MAONYESHO YA WIKI YA NISHATI 2024 YALIYOKUWA YAKIFANYIKA VIWANJA VYA BUNGE DODOMA

Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Doto Biteko, wakimsikiliza mmoja wa wakurugenzi wa REA baada ya kuwasili katika banda lao
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu Nishati Safi
ya Kupikia kutoka kwa Mkurugenzi  wa  Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
Mhandisi Hassan Saidy wakati alipotembelea na kufunga  Manyesho ya Wiki ya Nishati Jijini Dodoma,
tarehe 19 Aprili 2024.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile (kushoto), akibadilishana mawazo katika maonyesho hayo

Mkuu wa mawasiliano  katika Maonyesho hayo Neema Mbuja, akimkalibisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuzungumza katika ufungaji huo


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramb, akizungumza 
Waalikwa katika hafla hiyo wakiwemo wabunge wakisikiliza kwa makini ufungaji huo

Watumishi wa wizara hiyo wakipiga picha ya pamoja na Waziri Mkuu na vionvozi wengine
Majaliwa na Doto wakiagana baada ya kumalizika ufungaji huo
Majaliwa akiagana na Spika Dkt. Tulia


Katibu Mkuu Mramba, akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo na Taasisi zake

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
 

Waziri Mkuu,  Kassim  Majaliwa, amefunga Maonyesho ya Wiki ya Nishati katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma na  kutoa maagizo kwa
Wizara ya Nishati na Taasisi zake kuendelea kuboresha maoyesho hayo na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Majaliwa ameitaka Wizara ya Nishati kuweka mkakati wa kuhakikisha maonyesho hayo yanakuwa endelevu ili wabunge wapate fursa za
kuwasilisha hoja zao moja kwa moja kwa wataalam na kupewa majawabu ya hoja na changamoto zinazowakabili wao na wananchi wanaowakilishwa.

Aidha, ameagiza Maonyesho ya Nishati yafanyike kuanzia ngazi ya wilaya, mikoa na halmashauri ili yale yanayofanyika Makao Makuu yabaki kuwa ya
Kitaifa.

Waziri Mkuu Majaliwa amefafanua kuwa kwa kufanya hivyo huduma zitakuwa zimesogezwa zaidi
kwa kwa wananchi na pia Mameneja wa TANESCO wa Kanda, Mikoa na Wilaya watoe ufafanuzi wa hoja na changamoto zinazowakabili wananchi husika.

Vilevile ameitaka Wizara kuweka mkakati wa kuwawezesha wananchi wote kupata ufafanuzi na fursa zinazotokana na miradi inayotekelezwa katika
Sekta ya Nishati.

Pia ameagiza maonyesho hayo yafanyike maeneo yanayofikika kwa urahisi kwa wananchi wengi kama vile katikati ya miji ili wananchi wengi
washiriki na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali.

Pia Waziri Mkuu ameitaka Wizara isimamie na kuondoa mlundikano
wa maombi ya kuunganisha umeme kwa wananchi na TANESCO ihakikishe inaimarisha mfumo wa kupokea maombi na kutekeleza maombi hayo kwa
haraka.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa agizo kuwa Taasisi zote
zinazolisha watu wengi kuanzia 50 hadi 100 waanze kubadilisha
teknolojia ya kupikia na kutumia Nishati Safi ya Kupikia na ifikapo
mwisho wa mwaka 2024 Serikali inataka kuona asilimia 99 ya Taasisi za aina hiyo zinatumia Nishati Safi ya Kupikia.

Aidhae amempongeza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kwa
utendaji kazi wake ambao umechochea hali ya upatikanaji umeme nchini kuongezeka na kutosheleza mahitaji na pia kuwezesha upatikanaji wa
umeme wa ziada.
 
Naye Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Wizara hiyo Doto Biteko, alimsahukuru Waziri mkuu kwa kukubali kufika kuwafungia maonyesho yao kwa mwaka huu 2024  na kumwahidi kwamba maagizo aliyowapati watayafanyia kazi kwa uharaka zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.