RIPOTI YA CAG YABAINI MADUDU KIBAOI KATIKA MAKAMPUNI YA TTC, ATCL NA TRC

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu  za Serikali (CAG) Charles Kichele, akizungumza na wanahabari  Leo jijini Dodoma wakati akiwasilisha ripoti yake baada ya kutoka bungeni akishuhudia ikifikishwa kwenye meza  ya  wabumnge leo



Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali kwa mwaka 2022/2023 imeonyesha mashirika ya umma 34 yaliripoti
hasara au nakisi kwa miaka miwili mfululizo ambapo Mashirika haya
yalijumuisha mashirika yanayojiendesha kibiashara 11 na mashirika
yasiyo ya kibiashara 23.

Akiwasilisha ripoti hiyo leo jijini Dodoma  mbele ya Waandishi wa habari,Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu  za Serikali (CAG), Charles Kichele amesema Mashirika yasiyo ya kibiashara yaliripoti nakisi kutokana na upungufu wa
fedha kutoka Serikalini na vyanzo mbadala vya mapato.

Ripoti hiyo iliwasilishwa Machi 28,2024 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, Ikulu Chamwino na  leo imewasilishwa Bungeni na Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande kisha baadaye CAG kuzungumza na Vyombo vya habari ofisini kwake  jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo imeonesha mashirika ya umma 24 yaliyopata faida au ziada
katika mwaka wa fedha 2021/22, yamepata hasara au nakisi katika
mwaka wa ukaguzi wa 2022/23 huku Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) imeendelea kupata hasara kwa
miaka sita mfululizo.



Wafanyakazi wa Mkaguzi huyo wakiwa katika mkutano huo



Wanahabari wakiwajibika katika mkutano huo



Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Halima Mdee, akizungumza katika mkutano huo


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Omar Mohamed Kigua, akizungumza  katika mkutano huo



 

Comments

Popular posts from this blog

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.