MAJI YA BOMBA MUSOMA VIJIJINI - MAKABIDHIANO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA USAMBAZAJI WA MAJI YA BOMBA YAFANYIKA KIJIJINI KWIKUBA

 


Kata za Busambara (vijiji: Kwikuba, Maneke na Mwiringo) na Kiriba (vijiji: Bwai Kumsoma, Bwai Kwitururu na Kiriba) zimeshuhudia Mkataba wa kusambaziwa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria ukitiwa saini katika Kijijini cha Kwikuba.

Makabiadhiano hayo kati ya RUWASA na MKANDARASI (Otonde Construction & General Supplies Ltd) yalifanyika siku ya Jumatano asubuhi, 20.3.2024.

Walioshuhudia utiaji wa saini za Mkataba huo ni: wananchi kutoka Kata hizo mbili, viongozi kadhaa wa Chama (CCM) na Serikali, DAS Wilaya ya Musoma, na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

RUWASA inasifiwa sana kwa kufanya kazi nzuri Musoma Vijijini - hongereni sana RUWASA!

Gharama za Mradi huu:
Jumla ni: Tsh bilioni 4.42
Kazi za awali zitatumia: Tsh bilioni 1.44

Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 26.3.2024



Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA