RAIS WANGU DKT.SAMIA SULUHU HASSAN NAOMBA UTENGE MUDA WAKO UFUATILIE SAKATA HILI C W T

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
 

 RAIS wangu Dkt. Samia Suluhu Hassan, mtoto wako akikunyea mkono unaukata,  hebu tenga muda wako mfupi fuatilia Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kisichoisha migogoro, kinapata mchango mkubwa wa ruzuku unaofikia Sh. Bilioni  4 Kila mwezi kutoka Serikalini.
 

Kunamadai wasaidizi wako hizo fedha wanazimezea mate ndiyo maana ugomvi haushi hapo.

Wanachofanyiwa walimu ni sawa yanayofanyika katika Halmashauri nchini wakurugenzi wanakwapua fedha kwasabau wanaelewana na wakurugenzi.

Wakurugenzi wanahamishwa kwenda kituo kingine cha kazi baada ya kukwapua mamilioni ya shilingi wabunge wanalalamikia wakurugenzi hao lakini  hatua hazichukuliwi kwa sababu wanakula na wakubwa waliopo wizarani.

Rais wangu mimi siyo mtetezi wa Maganga na wenzake lakini walichofanyiwa ni unyanyasaji mkubwa walikamatwa katika mkutano wa kamati kuu wa kupanga matumizi ya chama.

Haya wakati yanatokea kulikuwa na kutoelewana kati ya katibu mkuu na Mwenyekiti wa kikao hicho Rais wa Chama hicho Leah Ulaya.

Taflani ilianza baada ya Maganga kusema hana imani na Mwenyekiti anaomba kikao hicho akiendeshe Makamu mwenyekiti ndipo ugomvi ukaanzia hapo na kusababisha Rais kuita polisi na kukamatwa.

Kibaya zaidi kumbe katika kutano huo kulikuwa na majina ya viongozi waliotakiwa kukamatwa, Mwekahazina wa chama hicho mkoa wa Geita akaaza kusoma majina ya viongozi 9 akiwemo Maganga wakachukuliwa na kwenda mahabusu kwa siku nne bila dhamana.

Rais wangu ukistajabu ya Musa basi ya filauni balaa, baada ya kupelekwa mahabusu kikao kiliendelea na agenda za kikao zilibadilishwa ikaingizwa ya viongozi waliofukuzwa na kamati hiyo eti walejeshwe huku wakiwa na kesi mahakamani na kweli wakalejeshwa akiwemo Naibu Katibu Mkuu  Joseph Misalaba, na sasa hivi ndiye kaimu katibu mkuu wa chama.

Eti wangekuwa katika mkutano huo mapinduzi hayo yasingefanikiwa katiba ya chama hicho imesiginwa kisa kwani  kuna madai kwamba, kulikuwa na fedha zimetolewa kutoka kwa viongozi serikalini na katibu mkuu amekuwa akikwamisha uchotaji fedha hizo.
 
Rais wangu ,walimu wamekuwa wakikatwa fedha zao katika mishahara  kulingana na vyeo vyao kuanzia elfu 7 hadi 25 hiyo kulingana na mishara yao, katika katiba yao wanautaratibu mwalimu akistaafu akiwa amechangia kwa miaka 15 analipwa mkono wa kwaheri sh. laki tatu na nusu.

Rais wangu walimu wanalilia michango yao tangu mwaka 2018 hadi 2022, Katibu Mkuu aliyeondoshwa alianza kulipa madai hayo kwa awamu  amelipa madai ya mwaka 2020 na 2022 inabaki miaka 6 ya madai ulipwaji huo ndio uliomponza kutokana na wachotaji kukosa fedha za chama hicho.

Rais wangu kwanini  CWT pekee kwani vyama vya wafanyakazi vipo vingi lakini kutokana na uchunguzi wangu huo wa fedha hizo ndiyo maana pindua pindua wanavunja hata amri za mahakama kundi la wasomi wamefanywa kama zezeta kutoka na nguvu kutoka nje.

Wajumbe waliomchagua Maganga kuwa katibu mkuu wao hawanashida naye lakini baadhi ya wenyeviti na makatibu kutoka mikoani wanaotumiwa na wanasiasa wemeshinikiza anyimwe kibali kwani kunatatizo gani kwani yeye siyo Mtanzania.
 

Chaajabu Rais wangu aliyekaimishwa  ukatibu mkuu Joseph Misalaba, kunamadai kwamba baada ya kufukuzwa na Baraza kuu la chama hicho na wenzake 17 alilejeshwa kwa mwajili wake Wilaya ya  Kasulu 18.4 2023 na kibali chake kilimalizika 14.12.2023 hadi sasa hana kibali

Istoshe tangu arudishwe kwa mwajili wake hajaripoti katika kituo chake cha kazi kwa siku 47 sheria inasema, ukiwa mtoro kwa siku tano umejifukuzisha kazi mwenyewe lakini kwa sababu nguvu zinatoka nje kwa kumtumia Rais wa chama hicho Leah Ulaya wamefanikisha jambo hilo.

Rais wangu hata wewe umekuwa ukisema kunawatendaji wako wanafanya kazi huku wakijiandaa kugombea urais wateule wako  wanajipanga kwa fedha na kusimika watu wao katika tasisi hizi usipokubaliana nao wanakutimua au kukufanyia mizengwe kama wanayomfanyia Maganga.


Comments

Popular posts from this blog

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.