WAOKOTA VYUMA CHAKAVU HATARINI KUPATWA NA MIONZI

Mkurugenzi wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania, Profesa. Lazaro Busagala (kulia), akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Austria, Naimi Aziz, alipotembelea ofisi za Tume hiyo leo jijini Dodoma na kuzungumza na wafanyakazi wa Tume


Baalozi Naimi akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili hapo

Mkurugenzi Busagala, akimuonyesha Maabara za Tume hiyo



Mkurugenzi akimweleza jambo kwa msisitizo Balozi


Wafanyakazi na wanahabari wakiwa katika mkutano huo
Mkuu wa Idara ya Habari wa Tume hiyo akiwakalibisha  wanahabari na balozi katika mkutano huo

Mkuu wa Tume hiyo Kanda ya Kati, Machibya Matulanga,akitoa maelezo kuhusu kazi za Tume hiyo

Picha zikionyesha miili ya binadamu iliyopata madhara kutokana na kukusanya vyuma chakavu

Balozi na Mkjurgenzi wakisikiliza kwa makini maelezo ya tume hiyo

Mkurugenzi wa Nguvu za Atomu nchini Profesa Lazaro Busagala, amesema wakusanya vyuma chakavu wapo katika hatari kubwa ya kupata maradhi ya mionzi kama hawatakuwa makini wakati wakifanya kazi hiyo, Mkurugenzi huyo aliyasema hayo leo wakati akimkalibisha Balozi wa Tanzania nchini Austria, Naimi Aziz (kushoto) alipotembelea Makao Maku ya tume hiyo zilizopo eneo la Kikombo jijini Dodoma. Mkurugenzi huyo amebainisha kwamba wakusanya vyuma chakavu hawanabudi kuwa makini pindi wanapokusanya vyuma hivyo ama sivyo watakuwa katika matatizo makubwa ya kupatwa na  maradhi mbalimbali, Pia alisema  hivyo hivyo kwa wale wanaochimba visima vya maji  kwa matumizi ya binadamu bila  kuwashirikisha wafanyakazi wa tume hiyo  ambapo maji yanayopatikana katika visima hivyo ni lazima yapimwme na watalamu wa tume hiyo ili wathibitishe kama yanafaa kwa matumizi ya binadamu, Baadhi ya maji yamekuwa yakibainika kuwa na mionzi ambayo inaweza kuleta madhara kwa binadamu kama wataruhusiwa kuyatumia.



Mkurugenzi Busagala, akimpatia zawadi Balozi Naimi baada ya kumalizika mazungumzo






Balozi Naimi,akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tume hiyo baada ya kumalizika kwa kikao chao

Balozi Naimi, akizungumza na Mkurugenzi Busagala  wakati akijiandaa kuondoka katika ofisi za Tume hiyo



 

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.