NJOONI KWENYE KILELE CHA MIAKA 60 YA JKT UWANJA WA JAMHURI DODOMA---BASHUNGWA

Waziri wa Uliniz na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa, amewaomba wananchi wa mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi katika sherehe za kilele cha miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa inayotalajiwa kufikia kesho kutwa katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Bashungwa ameyasema leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akiwa ameambatana na Mkuu wa Jeshi hilo  Meja Jenerali Rajabu Mabele, na maofisa waandamizi kutoka Wizara ya Ulinizi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Katika sherehe hizo mgeni rasmi anatalajiwa kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri amebainisha kwamba  kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya bidhaa zinazozalishwa na Jeshi hilo  watapata historia yake lilikotoka hadi sasa

Aidha Waziri Bashungwa, amemshukuru  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada  anazozifanya za kuhakikisha  JKT linaendelea kuwa kitovu cha malezi bora kwa vijana wa Kitanzania

Pia Waziri amelishukuru JKT kwa maandalizi ya maadhimisho  hayo, wadhamini na wote wanaoshirikiana nao katika maandalizi ya kesho kutwa , kwa namna ya pekee ameupongeza mkoa wa Dodoma chini ya Mkuu wa mkoa wake Rosemary Senyamule kwa uratibu mzuri unaoendelea katika kufanikisha m aadhimisho hayo.

 Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT kilitanguliwa  na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na JKT Marathoni 2023, iliyofanyika Juni 25 hapa Dodoma ambapo imekuwa marathoni ya kwanza kuandaliwa na JKT tangu kuanzishwa kwake.

Katika marathoni hizo mgeni rasmi alikuwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete, aidha Makamu wa Rais Philip Mpango Julai 1 2023 alizindua Mnara wa kumbukumbu Makao Makuu ya Jeshi hilo Chamwino na kufungua maonyesho ya bidhaa  siku hiyo ambayo yanaendelea hadi sasa, viwanja vya Medeli East mkabala na SUMAJKT House.

Pia huduma za kijamii kama kutembelea Hospitali ya Uhuru wilaya ya Chamwino pamoja na  vituo vya kulelea watoto wenye uhitaji cha Kikombo zilifanyika.



Wanahabari wakimsikiliza kwa makini  Waziri





Waziri Bashungwa akisisitiza jambo


 

Comments

Popular posts from this blog

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?