HEWA UKAA NDIYO HABARI YA MJINI KWA SASA

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson,akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Mazingira hususan Hewa Ukaa waliofika bungeni kufanya walsha na wabunge, wadau hawa waliwaambia wabunge kuwa kuna mazao ya misitu mingi  lakini hakuna viwanda vya kuyachakata mengi yanavunwa na kupelekwa nje ya nchi, muda umefika sasa wa kuwa na viwanda. hivi sasa wageni waningia nchini na kuja kuanzisha upandaji miti kisha kwenda kukopa mamilioni ya fedha kwenye Taasisi za fedha za kimataifa kisha fedha hizo kuzipeleka makwao ili wakaazishe utunzaji wa mazingira  ambapo huko kwao wameyahalibu sana. hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Tabora Carbon Credit Harvest Programme Dkt. Ernest Phillip Irungu. Maneno hayo yaliungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalum Riziki Lulida, aliyesema kwamba muda umefika sasa laslimali za nchi kuwanufaisha wazawa na siyo wageni ambao wanakuja kutajilikia hapa na kuwaachi wazawa na umaskini wao."Mabenki yana ybukuwa na ubaguzi ombi la mkopo akiomba Mtanzania atahangaika hata miaka mitatu hapati lakini mgeni akiomba miezi miwili anapatiwa sasa muda umefika tuamke",alisema Mbunge Riziki. Kulia mstari wa mbele ni Mwenyekiti wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali linalojihusisha na Upandaji miti nchini la Habari Conservation Organzation (HCO) Bernard Ngwanawile.











Ofisa kutoka Shirika lisilokuwa la Kiserikali linalojihushisha na upandaji miti nchini la Habari Conservation Organzation (HCO) akitoa mada kwa wabunge


Mbunge Riziki, akizungumza

Naibu Waziri wa maliasili na Utalii, Mary Masanja, akizungumza




Picha ya pamoja baada ya walsha

 

Comments

Popular posts from this blog

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.