RAIS SAMIA AMEWAUNGANISHA WATANZANIA---DKT. BITEKO


*Asisitiza Wototo Kupatiwa Elimu na Malezi Bora ili kujenga Taifa lililo bora*

*Chemba, Dodoma*

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaunganisha watanzania katika Sekta zote nchini ili kuhakikisha wananufaika na rasilimali mbalimbali zilizopo pamoja na kujenga uchumi wa Taifa.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa kutoka Jumuiya ya Wazazi katika Maadhimisho Wiki ya Wazazi Kimkoa (Miaka 68 ya Jumuiya) yaliyofanyika Aprili 29, 2023 wilaya ya Chemba kwa Mtoro, Mkoani Dodoma

"Rais Samia na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi amefanya kazi kubwa ya kuwaunganisha watanzania, leo wote tunaimba maendeleo, wote tunaimba maji, wote tunaimba barabara,  wote tunaimba madarasa kwa ajili ya watoto wetu na wote tunaimba maendeleo kwa ajili ya nchi yetu," amesema Dkt. Biteko.

Akizungumzia kuhusu shule ya Sekondari Kuryo iliyosimama kwa muda mrefu amesisitiza kuwa atasimamia ili ufumbuzi upatikane na hatimaye shule hiyo ianze kufundisha. Pia, amewataka wananchi wa wilaya ya Chemba kuungana kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko ameitaka Jumuiya ya
Wazazi wa wilaya ya chemba na Taifa kuwekeza kwa wototo ili Taifa liweze kufanikiwa kwa kuwapatia elimu na kuwafundisha malezi yaliyo bora na kuwa kizazi chenye maadili.

Naye, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dodoma, Samwel Malecela amemshukuru Dkt. Doto Biteko kwa kukubali  kuwa Mgeni rasmi maadhimisho hayo. Amesisitiza wananchi kupendana na kufanya kazi kwa bidii na kuheshimu taratibu za nchi zilizowekwa.

Dkt. Biteko ametembelea eneo la Shule ya Sekondari Kuryo na kufungua Shina la wakereketwa. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ni "Taifa Bora, hutokana na Malezi Bora ya Watoto". Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi wa vyama vya siasa, Mbunge wa Jimbo la Chemba Mohamed Monni na wananchi wa wilaya hiyo.


Mbunge wa Jimbo la Chemba Mohamed Monni,akihutubia katika mkutano huo
Wananchi wakimsikiliza Dkt. Biteko
Akivalishwa skafu na Chipukizi wa Chama baada ya kuwasili kwa ajili ya mkutano huo

akiwa katika eneo la Shule ya Sekondari Kuryo na kufungua Shina la wakereketwa kama anavyoonekana
 

Comments

Popular posts from this blog

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.