WASHINDI WA NMB “MASTABATAKOTEKOTE” WAKABIDHIWA TIKETI KWENDA DUBAI

 

Philbert Casmir Mkuu wa Idara ya Kadi Benki ya NMB akikabidhi tiketi za ndege kwa Chintan Kamania na mke wake Kaminy Chudasama pamoja na mtoto wao Eirny Kamania  baada ya kushinda bahati nasibu ya “Mastabatakotekote” aliyojishindia safari ya kwenda Dubai kwa ajili ya mapumziko,  Shindano hilo lilikuwa likiendeshwa na Benki ya NMB kwa wateja wake wanaofanya malipo ya huduma mbalimbali kwa kutumia Master Card ya NMB

Philbert Casmir Mkuu wa Idara ya Kadi Benki ya NMB akizunguma wakati benki hiyo ilipowakabidhi washindi wa bahati nasibu ya “Mastabatakotekote” waliojishindia safari yakwenda Dubai kwa ajili ya mapumziko, Shindano hilo lilikuwa likiendeshwa na Benki ya NMB kwa wateja wake wanaofanya malipo ya huduma mbalimbali kwa kutumia Master Card ya NMB.

Philbert Casmir Mkuu wa Idara ya Kadi Benki ya NMB akikabidhi tiketi za ndege kwa John Lubisha mmoja wa washindi wa  bahati nasibu ya “Mastabatakotekote” aliyojishindia safari yakwenda Dubai kwa ajili ya mapumziko,  Shindano hilo lilikuwa likiendeshwa na Benki ya NMB kwa wateja wake wanaofanya malipo ya huduma mbalimbali kwa kutumia Master Card ya NMB.

Picha ya paoja ya washindi.

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@


Akizungumza na waandishi wa habari mshindi wa droo ya “MastaBatakote kote”iliyokuwa ikie deshwa  na Benki  ya NMb Ndugu John Lubisha ameishukuru Benki ya Nmb kwa kuweka shindano hilo lililomuwezesha kuwa mshindi wa kwenda Dubai Kwa mapumziko

“Nilifurahi sana baada ya kupokea simu kwamba mimi nimekuwa mshindi, nashukuru Mungu kwa kupata hii nafasi,” Amesema John Lubisha

John ameongeza kwamba alikuwa anatumia kadi ya Nmb ya Mastercard (Kuchanja) kulipia bidhaa mbali mbali na hatimaye ameweza kupata ushindi katika droo hiyo.

“Ili kushiriki hizi droo mshiriki anatakiwa kuwa mvumilivu kwa kuendelea kutumia huduma ya kadi( kuchanja) kwa muda mrefu na siku moja anaweza kuwa yeye ndio mshindi,” Amesema John Lubisha

Aidha John amewashauri Watanzania kutumia kadi ya Mastercard kwani ni rahisi lakini pia ni usalama zaidi kwani kutembea na pesa nyingi(Cash) si salama kwakuwa kuna matukio mengi ya kihalifu hata hivyo kutumia Mastercard kuna rahisisha maisha.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya kadi wa Benki hiyo Bw. Filbert Casmir  amesema washindi hao wa kampeni ya “Mastabatakotekote” iliyoanzishwa mwezi wa kumi 2022 watakabidhiwa tiketi zao leo tarehe 28 Februari 2023.

Washindi hao watalipiwa gharama zote watakazotumia Dubai ikiwa ni pamoja na kutembelea vivutio hayo yote ni kurudisha shukurani kwa wateja wa benki hiyo.

Aidha amewashauri Watanzania kuendelea kutumia Mastercard kwani benki hiyo itaendelea kuwa na kampeni mbali mbali zitakazoambatana na zawadi.

Benki ya NMB ilianzisha kampeni ya “Mastabatakotekote”  ikiwa na malengo mbali mbali ya kuhamasisha wateja wao kutumia Mastercard,kuwajali wateja wao ambapo washindi waliopatikana wataenda Dubai kwa siku nne

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.