MALEZI YA WATOTO NCHINI NI YETU SOTE --PJT-MMMAM

Baadhi ya wazazi na walezi walioshiriki kwenye mafunzo ya malezi ya watoto kuanzia unri sifuri Hadi miaka minane Katika manispaa ya Temeke
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@

Na PATRICIA KIMELEMETA

HALMASHAURI ya Manispaa ya Temeke wameendesha mafunzo ya malezi ya watoto kwa wananchi wa Manispaa hiyo ili kupunguza vitendo vya ukatili vinavyoweza kujitokeza Katika jamii. 

Hatua hiyo imekuja wakati Serikali inatekeleza mradi wa Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) kuanzia umri sifuri hadi miaka minane.

Mradi huo ambao ulizinduliwa mwishoni mwa Mwaka Jana, ambao umelenga kundi la watoto wadogo ambalo linahitaji kuangalia Kwa ukaribu na kufanyiwa uwekezaji Ili waweze kukua Katika hali ya utimilifu.

Ofisa Ustawi wa Jamii Mfawidhi wa Manispaa hiyo, Dorice Tefurukwa alisema kuwa, mafunzo hayo yameshirikisha wazazi na walezi ambao wanaishi na watoto wadogo ili waweze kubadilisha mawazo na kupeana mbinu mbalimbali za malezi ambazo wanamini zitasaidia kupunguza vitendo vya ukatili.

Alisema kuwa, watoto wenye umri sifuri hadi miaka minane ni kundi muhimu katika jamii ambalo linahitaji kuangalia kwa umakini, kuanzia umri wa miaka minane ambao anatakiwa kuanza elimu ya awali ambapo atakuwa anakutana na jamii tofauti pindi anapoenda shule, hivyo basi jamii inapaswa kumlinda ili asiweze kufanyiwa vitendo vyovyote ambavyo vinaweza kuathiri ukuaji wake.

" Tumeshirikisha wazazi na walezi lengo likiwa ni kubadilishana mawazo ya namna ambavyo watoto wanaweza kulelewa katika hali ya utimilifu kwa mzazi kushirikiana na jamii husika, jambo ambalo tunaamini tunaweza kupunguza vitendo vya ukatili.

"Mtoto anapofikisha miaka minne anatakiwa kwenda shule ya awali na anapofikisha umri wa miaka sita au Saba anatakiwa kuanza darasa la kwanza, hawezi kujitetea mwenyewe, anategemea jamii iweze kumlinda na kumsaidia kwa sababu anakutana na watu tofauti wema na wabaya, ikiwa jamii itaelimisha wataweza kutekeleza malezi jumuishi na kuwalinda watoto," alisema.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (Tecden) Mwajuma Rwebangira alisema kuwa, malezi ya mtoto yanahitaji ushirikiano wa jamii husika, wazazi, walimu na walezi.

Alisema kuwa, katika kipindi hiki ambacho kumejitokeza matukio mbalimbali ya unyanyasaji wa watoto, wanapaswa kutoa elimu ya malezi ya mtoto kwa jamii ili waweze kuishi katika mazingira salama.

"Wanaotekeleza vitendo vya unyanyasaji wa watoto wapo katika jamii zetu, hivyo basi tunapotoa elimu, tunaelimisha jamii ili iweze kumlinda mtoto na hatari zozote ambazo zinaweza kujitokeza kwenye maeneo hayo jambo ambalo tunaamini linaweza kupunguza vitendo vya ukatili,"alisema Rwebangira.

Naye Daktari Bingwa wa watoto kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Judith Cosmas alisema kuwa, ikiwa watoto watalelewa katika mazingira salama, ukuaji wao unakua mzuri na kumuelusha na magonjwa mbalimbali.

" Ikiwa mtoto atalelewa katika mazingira salama, atakua ameepukana na magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kuathiri ukuaji wake kimwili na kiakili," alisema Dk. Cosmas.

Aliongeza kuwa, mtoto huyo atakua mchangamfu kutokana na ubongo wake kukua katika hali ya utimilifu na kumfanya kuwa na afya njema.  

Hata hivyo, baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa, elimu ya malezi jumuishi ni muhimu katika jamii ambapo ndipo watoto wanapoishi, kusoma na kufanyika kwa vitendo vya ukatili.

" Hawa watoto ni wetu, tunaishu nao Katika jamii zetu na wanaotekeleza vitendo vya ukatili wanatoka ktika jamii zetu, hivyo basi kutolewa Kwa mafunzo haya kutabdilisha mtazamo kwa wananchi na kuongeza ulinzi Kwa watoto," alisema Adam Mtenda.

Kwa upande wake, Shadya Junior ambaye ni dada wa kazi alisema kuwa, wazazi wanapaswa kusihi vizuri na wasichana wa kazi Ili kuleta ushirikiano, jambo ambalo litaweza kupunguza vitendo vya ukatili.

" Kuna baadhi ya wazazi wanawatesa sana wasichana wa kazi, jambo ambalo linasababisha chuki na baadhi yao kuwafanyia watoto vitendo vya ukatili, hivyo basi kutolewa kwa mafunzo haya kutabadili mtazamo na kuishi nao vizuri halk ambayo itapunguza vitenso vya ukatili," alisema Shadya.

Programu ya PJT-MMMAM, Serikali inashirikiana na Asasi za kiraia katika kutekelezaji wake, ulianza 2021 hadi 2026 ambao unalenga kutatua changamoto za ukuaji wa watoto nchini.





 

Comments

Popular posts from this blog

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?