BALOZI DKT. CHANA ASISITIZA USHIRIKIANO KUFIKIA MALENGO YA SERIKALI

 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) akimpokea Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Hamis Mwinjuma (Mb) alipowasili ofisini Mtumba jijini Dodoma Februari 28, 2023, mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Februari 27, 2023 Ikulu Chamwino.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma (Mb) akiongea na wajumbe wa Menejimenti mara baada ya kuwasili na kupokelewa katika Ofisi za Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akimkabidhi vitendea kazi ikiwemo Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 hadi 2025 Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma (Mb) mara baada ya kuwasili ofisini Mtumba jijini Dodoma Februari 28, 2023 baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) akiongea na wajumbe wa Menejimenti wakati wa mapokezi ya Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma (Mb) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Nicholas Merinyo Mkapa Februari 28, 2023 katika Ofisi za Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@

Na Eleuteri Mangi-WUSM, Dodoma

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewasisitiza Wajumbe wa Menejimenti na watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufikia malengo ya Serikali.

Waziri Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema hayo Februari 28, 2023 wakati wa mapokezi ya Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma (Mb) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Nicholas Merinyo Mkapa katika Ofisi za Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Februari 27, 2023 Ikulu Chamwino Dodoma.

- Advertisement -

Akizungumza na Menejimenti ya Wizara hiyo Mhe. Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana amewasisitiza viongozi wafanye kazi kwa ushirikiano ili kutekeleza malengo ya Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Tuna kazi ya kufanya,  tufunge mkanda, timu imekamilika, nimesimama hapa tukumbushane habari ya “Team Work”  Maana huku tayari tunaye Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu. Hawa wenzetu ni wataalam wa kufuatilia masuala tuliyopanga na kukubaliana kuyafanya” amesema Waziri Balozi Dkt. Chana.

Amewataka Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo wampe ushirikiano wa kutosha Naibu Waziri mpya Mhe. Hamis Mwinjuma kama wanavyoendelea kumpa yeye ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake.

- Advertisement -

“Tuna dhamana mbele ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tuna mambo ya kuonesha umma, uwezo tunao na nia ya kufikisha malengo ya Serikali ambayo tumepewa tunayo na sababu tunazo na tunawajibu wa kuhakikisha mambo yaende na yakamilike” Amesisitiza Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana.

Amesema kuwa wadau wa Wizara hiyo ni watu wote ambao wanaguswa kwa namna moja au nyingine kwenye sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, ni wengi na wapo mikoa yote 26 kuanzia watoto, watu wazima, wanawake kwa wanaume na sekta hizo zinatoa ajira kwa wadau hao na kuongeza Pato la Taifa na la mtu mmoja mmoja kutokana na kazi wanazofanya.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mhe. Hamis Mwinjuma amemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dhamana aliyompa katika Wizara hiyo na kuwahakikishia menejimenti na watumishi wa Wizara hiyo kuwapa ushirikiano na kufanya kazi kama timu moja ili kufikia malengo ya yaliyowekwa.

“Mimi sitaki kushindwa, mambo yote ambayo tulikuwa tunayafanya kwa kushirikiana na BASATA, COSOTA, Bodi ya Filamu tutayaendeleza. Ninaomba ushirikiano wa kila namna, twende mpaka nje ya njia zetu wakati mwingine ili kuhakikisha mambo yanatimia” amesema Naibu Waziri Mhe. Mwinjuma.

Ameongeza kuwa Wizara hiyo inapaswa kufanya kazi yake ya kutangaza na kuzisaidia wizara nyingine na jukumu la Wizara hiyo ni kulitangaza Taifa kwa usahihi zaidi kwa kushirikiana na Wizara zote hapa nchini. 

Naye Katibu Mkuu Bw. Saidi Yakubu amesema kuwa Naibu Waziri Mhe. Mwinjuma amekuwa mdau muhimu wa Wizara hiyo kwa muda mrefu na ameongeza nguvu katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara hiyo huku Naibu Katibu Mkuu Bw. Nicholas Mkapa akiwaomba ushirikiano wajumbe hao wa Menejimenti katika utekelezaji wa majukumu yake.

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.