TWENDE NA SERIKALI NA SIYO TWENDE NA SAMIA- MWENYEKITI WAQ CHAMA SAMIA AWAAMBIA UWT KATIKA MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan, ameutaka Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kujipanga upya kimkakati katika kujiimarisha kiuchumi, kijamii na kisiasa ili kutimiza malengo, dira na shabaha ya jumuiya hiyo, katika kutataua changamoto za wanawake nchini, sambamba na kuwafungamanisha katika kutumia fursa za kujikwamua na umasikini na kujiletea maendeleo endelevu.

Ndugu Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo (leo) Novemba 28, 2022 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa kumi (10) wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na ajenda ya uchaguzi wa viongozi wa jumuiya hiyo ngazi ya Taifa watakaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo (2022- 2027).

Amesema kumekuwa na jitihada kubwa zinazofanywa na serikali za kuwaletea maendeleao wananchi katika nyanja za uimarishaji wa huduma mbali mbali za kijamii ikiwemo Maji safi na salama, Afya, Kilimo, ujenzi wa miundombinu ya kisasa pamoja na kuimarisha huduma za nishati ya umeme maeneo ambayo yanampa unafuu mkubwa mwanamke ili kuweza kufanya shughuli za maendeleo,

hivyo amewataka viongozi watakaochaguliwa kuwa kiungo kizuri baina yao na serikali hasa katika ufuatiliaji wa miradi hiyo ambayo inaligusa kundi kubwa la wanawake katika jamii.

“Wanawake katika historia ya Taifa letu waliunganisha watu wa rika zote na hadhi tofauti katika harakati za kudai uhuru, dhima hii ya kuwaunganisha watu ni yetu sisi wanawake, hatuwezi  kuikimbia kama vile ambavyo  hatuwezi kukimbia na kuziona familia zetu zikisambaratika. Mwanamke ni muhimili mkuu katika kuunganisha familia na jamii na vivyo hivyo ni lazima tubebe jukumu la kuunganisha, ili Chama chetu kiendelee kuwa madhubuti siku hadi siku” Alisema.

Kuhusu udhalilishaji wa kijinsia, Ndugu Samia Suluhu Hassan amewakumbusha UWT  kuendelea kupaza sauti zao  katika kupinga aina zote za udhalilishaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kutoa rai kwa ngazi zote kuanzia shina hadi Taifa ili kuondokana na vitendo hivyo ni vyema kushirikiana pamoja katika kupiga vita kwa  lengo la kupunguza maumivu na kuongeza furaha katika jamii.

Aidha, ameitaka UWT kuendelea kujipanga vyema katika kuimarisha jumuiya hiyo kiuchumi kwa kuwa na miradi ya uwekezaji yenye kwenda na wakati na kuisimamia vyema ili kuleta tija kwa taasisi hiyo ambayo ndio tegemeo kubwa katika ukombozi wa wanawake nchini kisiasa.

“Miradi tuliyonayo bado haijawa miradi mikubwa ya kutupa nguvu kubwa ya kiuchumi katika jumuiya. Kama mnavyojua uwezo wa kiuchumi hununua uwezo wa siasa, hivyo  tusiposimama vizuri na kwa sababu hatuna nguvu ya kiuchumi huenda tukanunuliwa kisiasa, twendeni kukajiimarishe na tukajipange vizuri ili kufikia lengo” Amesema.

Hata hivyo, Ndugu Samia Suluhu Hassan amezipongeza jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (WAZAZI, UVCCM na UWT) kwa kukamilisha chaguzi katika ngazi zote ambapo amezikumbusha  kuwa jukumu kubwa liliko mbeleni ni kusimama na serikali katika kufanya shughuli za kujiletea maendeleo bila kujali itikadi za kisiasa na kwa kutanguliza Utanzania jambo ambalo litaendeleza ushirikiano, umoja na mshikamano wa Taifa.

Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa umoja huo wakijinadi mbele ya wajumbe
Aliyekuwa Mwenyekiti wa umoja huo akiozungumza kwa mara ya mwisho akiwa katika nafasi hiyo
Wapambe wa wagombea wakiwapokea wajumne wa mkutano huo huku wakiwa wamebeba mabango ya wagombea
Wajumbe kutoka mkoa wa Kagera

Mjumbe kutoka Kagera, Oliver Semguruka, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Muungano, nae akiwa katika mkutano huo
Mawaziri wa zamani na spika mstaafu, Anne Makinda na Sophia Simba ambaue pia alikuwa Mwenyekiti wa umoja huo wakishuhudia mkutano





Wasanii wa TOT wakionyesha ujuzi wao katika mkutano huo
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni ma Almas Nyangasa, nae alikuwepo katika mkutano huo


Wajumbe kutoka Simiyu

Wajumbe kutoka Mwanza














Mjumbe Lucy Mayenga,ambayue pia ni Mbunge wa Mkoa wa Shinyanga

Waliokuwa wagombea nafasi ya Mwenyekiti wakisikiliza matokeo
Mwenyekiti mpya Mary Pius Chatanda, akiwashukuru wananchi baada ya kuibuka mshindi
 

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.