NMB na maadhimisho wiki ya unywaji maziwa kitaifa.

 

Meneja Mahusiano Idara ya Kilimo Biashara Berdon Mwakatobe (wapili kutoka kushoto)  akimkabidhi Katibu tawala wa  mkoa wa Katavi Rodrick Mpogolo Shati 300 zikiwa ni sehemu ya udhamini WA benki hiyo kwa ajili ya maadhimisho wiki ya unywaji maziwa kitaifa inayoadhimishwa mkoani katavi  kwa mwaka 2022. Kulia ni Mwakilishi WA Bodi ya Maziwa Tanzania Christabel Swai na Meneja wa NMB Mpanda Hygrace Mwanjuguja (kushoto)
MWAKILISHI WA MENEJA WA NMB KANDA YA WESTER ZONE BERDON MWAKATOBE AKIMKABIDHI RAS WA MKOA WA KATAVI LODRICK MPOGOLO TISHETI 300 
KULIA NI MENEJA WA BENK NMB MPANDA HYGRACE MWANJUGUJA,WAPILI KULIA NI MWAKILISHI WA MENEJA WA NMB KANDA YA WESTER ZONE BERDON MWAKATOBE,WATATU NI RAS KATAVI LODRICK MPOGOLO NA WANNE NI CHRISTERBEL SWAI  
BERDON MWAKATOBE Akizungumza kwa niaba ya  Meneja wa kanda WESTER ZONE   



NMB  YAPIGA TAFU WIKI YA UHAMASISHAJI  UNYWAJI MAZIWA KITAIFA MKOANI  KATAVI


Benki ya Nmb imekuwa mdau wakubwa kwa upande wa serikali,  kilimo ,uvuvi na upande wa mifugo na niwazamini wakubwa wa maadhimisho wiki ya unywaji maziwa kitaifa inayoadhimishwa mkoani katavi  kwa mwaka 2022.

Nmb imekuwa ni sehemu ya maendeleo ya kilimo kwa upande wa uwezeshaji nmb wamekopesha fedha nyingi kwenye kilimo lakinipia kwenye uvuvi na uzalishaji wa maziwa na uzalishaji wa maziwa na ufugaji wa Ng’ombe.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB  kanda ya Magharibi Berdon Mwakatobe wakati akikabidhi tisheti 300 zilizizotolewa na Benki hiyo kwa katibu tawala mkoa wa katavi aliepokea kwa niaba ya Waziri wa mifugo, zitakazo tumika kwenye maadhimisho ya wiki ya unywaji maziwa  kitaifa yanayofanyika mkoani katavi.

Mwakatobe ameeleza kuwa ukiachana na kudhamini maazimisho haya NMB wamekuwa wadau wakubwa wa maendeleo kuliko benki yeyote hapa nchini kwa kukopesha fedha nyingi katika sekta za kilimo ,mifugo,  uvuvi na Sekta ya uzalishaji wa  Maziwa kwa lengo la kuisadia serikali katika kumukomboa mwanachi kuichumi.

Amebainisha kuwa Benki hiyo  imetoa shilingi Bilioni 100 ambazo zimekopeshwa kwa asilimia10 na zimekwisha na wameongeza fedha nyingine ambazo kwa sasa zinakopeshwa kwa asilimia 9. Fedha zipo kwa ajili yenu wadau wote wa kilimo karibu kwenye Tawi lolote la NMB kupata fursa hii. Wadau waje wajitokeze kukopa kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Aidha alisema kuwa NMB wanaendelea kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo Umwagiliaji na sekta ya Tumbaku na sekta nyingine zote za kilimo kwenye Maadhimisho hayo ya wiki ya unywaji maziwa  NMB watakuwawanatoa huduma mbalimbali kwa wateja wao ikiwemo kufungua Akaunti kutoa elimuya mikopo ya NMB na kwa ajili ya wajasiliamali.

Katibu tawala wa  mkoa wa Katavi Rodrick Mpogolo aliishukuru NMB na Bodi ya maziwa kwa kuleta Wiki  ya uhamasishaji wa unywaji wa maziwa kitaifa katika mkoa wa katavi.

Alisema mkoa wa Katavi nimiongoni mwa mikoa yenye mifugo mingi sana wanasema kuwa mkoa wa Katavi nimiongoni mwa mikoa mitano hapa nchini yenye Idadi kubwa ya mifugo katika taifa letu.

Mpogolo amefafnua kuwa Mkoa wa Katavi unamaziwa mengi sana lakini inawezekana uhamasishaji wa unywaji wa maziwa bado upo kidogo inawezekana wengi wetu hatutumii maziwa kwani maziwa nilishena nayanaboresha afya zetu ukinywa maziwa umepata mlokamili  bodi ya Maziwa na NMB wameleta kitu muhimu sana kwa wanachi wa mkoa wa Katavi kwaajiliya maendeleo na usitawi wa kiuchumi na afya kwaajili ya wanachi wa mkoa wa Katavi.

Amesisitiza kuwa kazi ya uhamasishaji ya unywaji wa maziwa katika Mkoa wa Katavi bado nikubwa kwani kuna baadhi ya familia zinakunywa maziwa mara moja tu maziwa kwa mwezi hivyo uhamasishaji kwa wadau bado unahitajika.

Nae mwakilishi wa Msajili wa Bodi ya maziwa Tanzania Christerbel Swai aliishukuru NMB kwakuwa wadau muhimu katika shughuli muhimu kwenye nchi yetu ya Tanzania ya uhamasishaji wa unywaji wa maziwa.

Swai alisema shughuli ya uhamasishaji wa unywaji wa maziwa hapa nchini hufanyika kila mwaka Mwezi wa Sita kwenye shughuli hizi wadau wa maziwa huwa wadhamini wakuu wa shuguli hizi na mwaka huu Benki ya NMB imewadhamini jumla ya Tisheti 300.

 MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.