SIMBA CEMENT YATOA MIFUKO 3000 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI MKOANI SINGIDA




Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akipokea mifuko 3000 ya Saruji kutoka Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya elimu katika Jimbo lake la Iramba Magharibi leo katika anayeshughudia ni Meneja wa Kiwanda hicho Benny Lema
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba kushoto akipokea mifuko 3000 ya Saruji kutoka Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya elimu katika Jimbo lake la Iramba Mashariki leo katika anayeshughudia ni kushoto ni Afisa Uhusiano wa Simba Cement Noor Mtanga kulia ni Msaidizi wa Mbunge huyo Abdallah Salim
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akimkabidhi Msaidizi wake,Abdallah Salimu mifuko hiyo mara baada ya kukabidhiwa anayeshughudia katikati nyuma ni Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart

Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akipokea sehemu ya mifuko ya Saruji 3000 kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Simba Cement Noor Mtanga kulia kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu katika Jimbo lake la Iramba Magharibi katika kulia anaye shughudia ni Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kushoto ni Meneja wa Kiwanda hicho Benny Lema
Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart akieleza mikakati ya kiwanda hicho kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba ambaye hayupo pichani ambaye alikwenda kiwanda hapo kupokea mifuko 3000 ya saruji kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya Elimu Jimboni kwake Iramba Magharibi
aziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba na vyombo vya habari mara baada ya kupokea mifuko 3000 ya saruji ambapo alikishukuru kiwanda cha Simba Cement kwa kusaidia sekta ya Elimu Jimboni kwake kuli ni Mkurugenzi wa Kiwanda hicho,Reinhardt Swat
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba kushoto akimshukuru Mkurugenzi wa Kiwanda cha Simba Cement Reinhardt Swat mara baada ya kupokea mifuko 3000 ya Saruji kwa ajili ya kuimarisha Sekta ya Elimu Jimboni Kwake

Sehemu ya Saruji mifuko 3000 aliyokabidhiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kushoto akiwa na Mkurugenzi wa Simba Cement Reinhardt Swat wakitembelea kiwanda hicho kabla ya kukabidhiwa mifuko 3000 ya Saruji Mkurugenzi wa Kiwanda cha Simba Cement Reinhardt Swat kulia akimuonyesha eneo ambalo wanalotumia kwa shughuli za kiwanda Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchema katika ambaye alitembelea kushoto ni Meneja wa kiwanda hicho,Beny Lema Meneja wa Kiwanda cha Simba Cement Beny Lema akimuogoza Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kushuka ngazi mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali kwenye kiwanda hicho

Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kulia akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iramba mara baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kwa ajili ya kupokea mifuko 3000 ya saruji kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu kwenye Jimbo lake la Iramba Magharibi
Sehemu ya wafanyakazi wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement Jijini Tanga wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba
Meneja wa Kiwanda hicho Benny Lema kushoto akiwa na wafanyakazi wengine wa kiwanda hicho wakimsikiliza kwa umakini Waziri wa Mambo ya Ndani ,Mwigulu Nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba katika akiwa na Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kulia kushoto ni Msaidizi wa Mbunge huyo Abdallah Salim wakiongia ukumbini kwa ajili ya kupata taarifa.
Sehemu ya Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Tanga ambao nao waliambatana na Waziri wa Mambo ya Ndani katika makabidhiano hayo kulia ni Mkuu wa Polisi wilaya ya Tanga (OCD) Jumanne Abdalla(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

UJENZI WA BARABARA YA NYAHUA-CHAYA KM 85.4 KWA KIWANGO CHA LAMI WAANZA RASMI

Mkandarasi kutoka kampuni ya CHICO kutoka China, Bw. li, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, kuhusu hatua za awali za maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiwaonesha Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Queen Mlozi na Mbunge wa Jimbo la Igalula ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya miundombinu Mhe. Mussa Ntimizi, eneo ambapo ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami itajengwa, mkoani Tabora.
Tingatinga likikata miti kwa ajili ya kusafisha eneo ambapo ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami utaanza, mkoani Tabora. 


Serikali imeanza ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi wa kampuni ya CHICO kutoka China, ili kuweza kuufungua mkoa wa Tabora na mikoa jirani ya katavi na kigoma.
Amesema hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati aliposimamishwa na wakazi wa kijiji cha Tura, wilaya ya Uyui, mkoani Tabora, alipokuwa akikagua kambi ya mkandarasi na kuangalia hatua za awali za matayarisho ya ujenzi wa barabara hiyo.
Prof. Mbarawa amesema ujenzi wa barabara hiyo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 117.9 na utachukua miezi 24 mpaka kukamilika kwake."Serikali imeanza rasmi ujenzi wa barabara hii na sasa ni jukumu lenu kuhakikisha mnampa ushirikiano mkandarasi huyu ili mradi uwahi kukamilika mapema", amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amefafanua kuwa barabara hiyo ni kiungo muhimu katika kukuza biashara na usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwemo inayokwenda nchi jirani. Ameongeza kuwa sasa Serikali imeshapata fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kutoka daraja la Kikwete mpaka Uvinza, mkoani Kigoma na hivyo itasaidia wananchi wanaotumia usafiri wa mabasi kutoka mkoa wa Dar es Salaam mpaka mikoa ya katavi na Kigoma kupita kwenye lami njia nzima.
Naye Mbunge wa Jimbo la Igalula mkoani Tabora ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya miundombinu Mhe. Mussa Ntimizi, amemueleza Waziri Prof. Mbarawa kuwa yeye na timu yake watajitahidi kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kutohujumu vifaa vya mkandarasi huyo.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Queen Mlozi, ameishukuru Serikali kwa mradi unaoendelea katika wilaya hiyo na kumuahidi Waziri kuwa yeye na kamati ya usalama itahakikisha mkandarasi hahujumiwi.
Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi DamianNdibalinze, amemueleza Waziri kuwa kazi imeanza kwani Mkandarasi ameshaanza kuleta vifaa eneo la kazi na ujenzi wa kambi unaendelea.
Waziri Prof. Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Tabora ikiwa ni lengo la kukagua maendeleo ya miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea mkoani humo .

WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA DAWA ZA KULEVYA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wakiwemo wakazi wa mkoa wa Mwanza kuachana na biashara ya dawa za kulevya.


Pia Waziri Mkuu amegiza vijana nchini waelimishwe madhara mbalimbali yanayosababishwa na matumizi ya dawa za kulevya ili wajiepushe nazo.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumanne, Februari 20, 2018) alipozindua kliniki ya methadone kwa ajili ya waathirika wa dawa za kulevya.

Alizindua kliniki hiyo iliyopo kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure akiwa katika siku ya sita ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.

“Serikali imejizatiti katika vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya, hivyo nawataka wananchi wasijishughulishe nayo. waache kutumia, kusambaza na kuuza.”

Pia aliwaomba wananchi washirikiane na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na dawa hizo.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers Siyanga aliishukuru Serikali kwa kutambua madhara ya dawa za kulevya na kuchukua hatua.

Bw. Siyanga alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa waathirika wa dawa za kulevya kwenda katika kliniki za methadone ili wapatiwe matibabu yatakayowafanya kuachana na matumizi ya dawa hizo.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella alisema kuwa, mkoa huo ni miongoni mwa waathirika wakubwa wa biashara ya dawa za kulevya. Aidha, aliongeza kuwa bado kuna watu wanaoendeea kujishughulisha na biashara hiyo na kwamba Mkoa unaendelea kupambana nao.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile alisema dawa za kulevya zinasababisha madhara makubwa katika sekta ya afya kwa kuwa yanachangia kusambaa kwa magonjwa mbalimbali yakiwemo ukimwi na kifua kikuu.

Pia alisema kwa sasa dawa za methadone zinazotolewa kwa waathirika wa dawa za kulevya wanazipata kutoka kwa wahisani mbalimbali. Hata hivyo, Serikali imepanga kuingiza suala hilo katika bajeti ijayo ili ianze kuagiza yenyewe.

Baadhi ya vijana waliokuwa wanatumia dawa za kulevya mkoani Mwanza akiwemo, Nyamizi Sospeter na Abdul Abdallah, waliishukuru Serikali kwa kuanzisha vituo vya methadone.

Nyamizi alitumia dawa za kulevya kwa muda wa miaka saba na muda wote huo alikuwa akiisumbua familia yake kutokana na matukio mbalimbali ya kihalifu aliyokuwa akiyafanya ili apate fedha za kununulia dawa hizo.

Naye Abdul Abdallah alisema alitumia dawa za kulevya aina ya heroine kwa takribani miaka 20 na muda wote huo alikuwa anakaba watu ili apate fedha za kununulia dawa hizo.

“Naishukuru Serikali kwa kuanzisha kliniki ya methadone na sasa nimeacha mimi pamoja na mke wangu. Najiona binadamu maana nilikuwa mwizi, mchafu kwani nilikuwa nakaa mwezi bila kuoga na hata kutengwa na jamii.”

Kwa pamoja waathirika hao wa dawa za kulevya waliiomba Serikali kuwasaidia kwa kuwapa elimu ya ujasiriamali ili waweze kupata ujuzi utakaowawezesha kufanya kazi na kupata kipato kitakachowasaidia kuendesha maisha yao.

Awali, Waziri Mkuu alizindua muongozo wa uendeshaji wa nyumba za waathirika wa dawa za kulevya (Soba Houses) ambao unalenga kuwawezesha wamiliki wa nyumba hizo kuziendesha vizuri na kuwasaidia ipasavyo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,



JUMATANO, FEBRUARI 21, 2018.

RAIS MAGUFULI AWASILI UGANDA, AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS YOWERI MUSEVEN

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na ujumbe wake katika Mazungumzo na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitaabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda ambapo pamoja na mambo mengine atahudhuria vikao vya Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki vitakavyoanza kesho jijini Kampala nchini Uganda.
Kikundi cha ngoma za Asili cha Masters of ground kutoka Wilaya ya Kyotera, Masaka nchini Uganda wakitumbuiza baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda. PICHA NA IKULU
 

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MISUNGWI NA MWANASHERIA WAKAMATWA

JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoani hapa imemkamata Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Anthony Bahebe.

Pia Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw. Alphonce Sebukoto naye amekamatwa na Jeshi hilo. 

Viongozi wote hao wanakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhilifu wa fedha za umma. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.

Kamanda Msangi alisema, Bw. Sebukoto alikamatwa Februari 19, 2017 na Bw. Bahebe amekamatwa leo na wote wanaendelea kuhojiwa na Polisi kwa kushirikiana na TAKUKURU.Naye Kamanda wa TAKUKURU wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Ernest Makale alisema Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Bahebe.
Alisema Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo hayo kwa Bw. Bahebe Novemba 2017 wakati alipokuwa anakaimu nafasi ya ukurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi ambapo jumla sh. milioni 138 ziliingizwa katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti huyo. Alisema kiasi kingine cha fedha kinachunguzwa kubaini kilipo.
Februari 19, 2019 akiwa katika ziara yake wilayani Misungwi Waziri Mkuu Kassim Majaliwaalimsimamisha kazi Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Sebukoto na kuagiza achungunzwe na vyombo husika.Alichukua hatua hiyo baada Mwanasheria huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kushindwa kuishauri vyema halmashauri hiyo na kuisababishia hasara ya sh. milioni 278.
Amesema Mwanasheria huyo Novemba 2017 wakati alipokuwa anakaimu nafasi ya ukurugenzi aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Anthony Bahebe.
Waziri Mkuu alisema Bw. Bahebe aliishtaki halmashauri hiyo akidai kulipwa fedha kwa ajili ya kazi ya ukandarasi wa mradi wa maji Igenge uliojengwa na kampuni ya ukandarasi ya Seekevim. Alisema mradi huo ulianza 2014 na ulitakiwa ukamilike 2015. Mwanasheria huyo aliidhinisha malipo hayo wakati ambao tayari hati maalumu ya uwakilishi ilikuwa imekwisha tangu Desemba 2015.
Alisema Mwanasheria alimlipa Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kufanya kazi na Halmashauri jambo ambalo ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma.Hivyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi wa umma kuzingatia maadili ya utumishi na matakwa ya kisheria katika utekelezaji wa majukumu yao.
 

DCC LUSHOTO YASITISHA MPANGO WA UJENZI WA JENGO LA HALMASHAURI YA BUMBULI

Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Lushoto (DCC) imeamua kusitisha mpango wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Bumbuli lilokuwa lijengwe kwenye eneo jipya la Kwehangala hadi hapo suluhu ya mgogoro baina ya viongozi wa halmashauri hiyo itakapopatikana. 
Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Lushoto January Lugangika (Pichani Juu) alisema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya kuwepo sintofahamu kati ya Madiwani wa halmashauri hiyo na viongozi wengine juu ya suala hilo. .
Hivi karibuni kumekuwepo na mvutano mkubwa kati ya viongozi hao juu ya wapi pajengwe majango ya makao makuu ya Halmashauri hiyo. Baadhi ya viongozi wanadai utaratibu wa fedha za manunuzi haukufuatwa katika kufikia maamuzi ya kujenga jengo la Halmashauri katika eneo la Kwehangala na kuacha majengo yaliyokwisha jengwa Bumbuli kwa gharama ya Sh. milioni 700.
Kutokana na mvutano huo, Mkuu huyo wa Wilaya amesema kikao kiliafiki kisitishe zoezi hilo mpaka maelewano yatakapopatikana." Wajumbe wameshauri suala la kuhamisha makao makuu lisitishwe hadi hapo utakapopatikana utangamano,kwani tayari imeonekana kuna mgogoro ambao umeleta utengano kwa viongozi" Alisema Lugangika .

Mbunge wa jimbo hilo, January Makamba alikiri kuwepo kwa mvutano huo ambao alisema hauna tija katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Bumbuli.Makamba alisema ni vyema kama viongozi wakazungumzia suala la maendeleo mfano;maji,barabara,umeme,nyumba za watumishi badala ya kila siku kuzungumzia wapi kujengwe jengo la halmashauri. 
Alishauri kuwa wananchi washirikishwe katika suala hilo, ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu ya kutosha juu ya hoja ya kuhamisha halmashauri kwa kuwa ndio wenye chombo chao badala ya viongozi kuamua wao pekee.
"Suala hilo nakubaliana na maoni wa kikao cha DCC tulisitishe kwani kwa sasa hatuna shida na majengo ya halmashauri kwa sababu majengo tunayo ambayo hatulipii kodi ya pango. Sasa hivi tuzungumzie maendeleo kwani wananchi mwaka 2020 hawatatudai majengo ya halmashauri bali watatudai maendeleo juu ya huduma muhimu za jamii alisema Makamba.
Hivi karibuni baadhi ya Madiwani wa Halmashauri hiyo walipiga kura ya kupitisha azimio la kujenga jengo hilo la halmashauri huku Madiwani nane wakigoma kupiga kura kwa madai kuwa hawawezi kupiga kura wakati kuna ukiukwaji wa kanuni na utaratibu ktk kitengo cha manunuzi.
Madiwani hao nane ambao waligoma kupiga kura kupitisha azimio hilo mnamo January 18 mwaka huu walimuomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi kuingilia kati mgogoro na kuzuia walichokiita ukiukwaji wa utaratibu wa manunuzi pamoja na maelekezo mbalimbali ya viongozi juu ya mpango huo.
Pia walimuomba aingilie kati na kuchukua hatua dhidi ya ubadhirifu wa fedha za umma na ukiukwaji wa utaratibu wa uendeshaji wa halmashauri na kudharau kwa makusudi maelekezo yaliyotolewa na viongozi mbalimbali wa serikali kuu.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Amir Shehiza alisema kuwa baraza ni chombo chenye maamuzi sahihi hivyo alikitaka Kikao hicho cha DCC kuacha kuingilia Kazi za baraza . 

WAMILIKI WA LESENI ZA MADINI WAASWA UONGEZAJI THAMANI YA MADINI

Na Mathias Canal, Mbeya

Wamiliki wa leseni za madini ya dhababu, vito na mengineyo kote nchini wametakiwa kuiga mfano wa Ndg Salim Jesa mmiliki wa kiwanda cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd kinachojishughulisha na kukata, Kusaga na kuuza mawe kwa kufanya mchakato mzima mpaka bidhaa kukamilika hapa hapa nchini.

Kauli hiyo kwa wamiliki wa leseni za madini nchini imetolewa leo 20 Februari 2018 na Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya.

Alisema kuwa kiu ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ni kuona rasilimali za nchi zinaongezwa thamani zikiwa ndani ya nchi jambo ambalo linaakisi umakini wa utendaji na ulipaji kodi ya serikali pasina kukwepa ama kutorosha rasilimali madini yakiwa ghafi. 

Aliseama kuwa faida ya kuongeza thamani ya madini nchini ndio muarobaini wa sekta ya madini kuongeza kiwango cha uchangiaji wa pato la Taifa hatimaye kufikia asilimia 10% kama ulivyo mpango wa wizara kuongeza kiwango cha uchangiaji wa pato la Taifa.

“Nchi nyingi ambazo zimejua siri hii kwa kiasi kikubwa zimefanikiwa lakini sisi Tanzania tulichelewa sana, na kama tungeendelea kuchelewa ingefika kipindi ambacho madini yasingekuwepo kamwe na kama Taifa tungeambulia mashimo makubwa na kusalia katika wimbi la umasikini” Alisema Mhe Biteko

Aidha, amemuhikishia mmiliki wa kiwanda hicho kuwa serikali itazungumza na taasisi zinazofanya kazi za ujenzi nchini kuunga mkono juhudi za umahiri wa kiwanda hicho kwa kununua bidhaa zinazozalishwa hususani wakati huu ambao serikali inaendelea na mchakato wake wa kuhamia Mjini Dodoma.

Sambamba na hayo pia uongozi wa kiwanda hicho umempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kuweka sera nzuri hususani kwa wawekezaji wa ndani katika sekta ya madini na juhudi zake za kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na serikali kwa ujumla wake.

Kampuni ya Marmo E. Granite Mines (T) Ltd iliyopo mkoani Mbeya ilianzishwa mradi wa kukata, kusaga na kuuza mawe Januari 2004 baada ya kukidhi masharti ya usajili wa makampuni.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua mawe yaliyo katwa, Kusagwa na kuongezewa thamani katika kiwanda cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwasili katika kiwanda kinachoshughulika na kukata, Kusaga na kuuza mawe cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Ndg Salim Jesa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Marmo E. Granite Mines (T) Ltd kuhusu usafirishaji wa mawe baada ya kuyaongezea thamani wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua utendaji kazi wa kiwanda cha kukata, Kusaga na kuuza mawe cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.