ADAM MALIMA AANZA KUWASHUGHULIKIA WALIOHUJUMU KIWANDA CHA MAZIWA CHA UTEGI



UFAFANUZI: Mkuu wa Mkoa wa Mara (RC), Adam Malima (wa pili kushoto) akimsikiliza mmoja wa watu wanaodaiwa kuunda Kampuni ya UDAFCO akitoa maelezo kwenye kikao cha RC Malima huku Mbunge wa Jimbo la Rorya, Lameck Airo (kushoto) na viongozi wengine wakisikiliza mgogoro wa shamba la mifugo na kiwanda cha maziwa cha Utegi. Picha Na Peter Fabian.
 


Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (wapili kulia) aliyekaa akipitia nyaraka za mfanyabiashara ambaye ni mwekezaji wa shamba la mifugo na kiwanda cha maziwa cha Utegi kwenye kikao kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rorya juzi ikiwa ni agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alilolitoa hivi karibuni wengine Mwekezaji na Mkurugenzi wa Kampuni ya UDAFCO, Otieno Igogo (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Saimon Chacha (wapili kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Rorya, Lameck Airo (wa kwanza kushoto). 
 Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima akihutubia wananchi wa vijiji sita kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mji wa Utegi kusikiliza kero ya mgogoro wao na mwekezaji wa kiwanda cha maziwa cha Utegi na shamba la mifungo kama ilivyoagizwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa hivi karibuni alipokuwa kwenye ziara ya kikazi Wilayani Rorya.


Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima ( wa nne katikati) akionyeshwa na Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Saimon Chacha (wa pili kulia) eneoilipokuwa mashine ya kusindika maziwa katika jengo la kiwanda cha kusindika maziwa cha Utegi ikiwa imeng'olewa na kuibiwa na mwekezaji na kuuzwa nchi jirani ya Kenya alipotembelea kiwanda hicho kufatia agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa hivi karibuni alipokuwa mkoani Mara kwenye ziara ya kikazi.

Comments

Popular posts from this blog

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.