WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI LA UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es salaam . Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akipokea moja ya vifaa vya uchunguzi wa saratani ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran (kushoto) wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam. Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akipokea moja ya nyenzo za kufundishia juu ya uchunguzi wa saratani ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran (kushoto) wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam katikati ni Afisa Afya kutoka USAID Bi. Ananth Thambinygan . Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es salaam . Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya afya, Jpiego na USAID wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es salaam wa tatu kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran na aliyevaa nguo ya pundamilia ni Afisa Afya kutoka USAID Bi. Ananth Thambinygan .picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii. NA WAMJW-DAR ES SALAAM. WAZIRI Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amewaelekeza waganga wakuu wa mikoa yote nchini kuanzisha zoezi la wazi la uchunguzi wa saratani ya kizazi angalau mara moja katika mwezi ili kusaidia kutokomeza tatizo kwa wanawake hilo nchini. Hayo amesema wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 ambavyo vimetolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya JHPIEGO kwa kushirikiana na USAID ili kusaidia kupambana na tatizo hilo nchini. “Angalau ifikapo Desemba 2018 nataka vituo vya Afya vya Serikali 524 viwe vinatoa huduma ya matibabu ya awali ya Saratani ya mlango wa kizazi na kufikia wanawake milioni 3 watakaopata huduma hii ili kuokoa wanawake wa vijijini kwani mpaka sasa hivi tunavyo vituo vya afya 265 vinavyotoa huduma hii ” alisema Waziri Ummy. Aidha Waziri Ummy amesema kuwa uchunguzi na kutoa chanjo ya Saratani ya mlango wa kikazi kwa wasichana kuanzia miaka 9 mpaka 14 ili kuweza kupunguza vifo vitokanavyo na tatizo hilo kwani katika kila wanawake 100 vifo vinavyotokana na ugonjwa huo ni 32. Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa katika kuongeza jitihada za kupambana na ugonjwa huo Serikali imeongeza vituo vya afya 100 kutoka 343 hadi kufikia 443 mwaka huu ili kutokomeza tatizo hilo nchini. Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran amesema kuwa walianzisha mpango wa kupambana na tatizo hilo na kufanikiwa kuwafikia wanawake elfu 75 kwa mikoa 4 tangu mwaka 2009. “Mbali na mikoa hiyo 4 bado tunalengo la kuongeza mikoa mingine 7 ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa ajili ya kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi ili kuweza kuokoa wanawake wengi zaidi nchini” alisema Bw. Zoungran. Posted by MICHUZI BLOG at Monday, November 20, 2017 No comments: Links to this post Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest VODASTAR YAICHAKAZA NOKIA MAGOLI 8-1 MECHI YAKIRAFIKI Mshambuliaji wa timu ya VodaStar, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (wapili kulia)akishangilia goli baada ya kuifungia timu yake wakati wa mchezo wakirafiki dhidi ya timu ya Nokia uliofanyika katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam,VodaStar iliiadhibu Nokia kwa magoli 8-1. Wachezaji wa timu ya VodaStar,wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (wapili kulia mwenye miwani) wakishangilia kombe lao baada ya kuihadabisha timu ya Nokia kwa magoli 8-1 wakati wa mchezo wakirafiki uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kikosi cha timu ya VodaStar kilichoisambaratisha timu ya Nokia kwa magoli 8-1 wakati wa mechi yakirafiki wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mechi hiyo kuisha iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mashabiki watimu ya VodaStar, wakifurahia kombe lao baada ya timu yao kiichakaza timu ya Nokia kwa magoli 8-1 wakati wamchezo wakirafiki uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (kushoto) akimshuhudia Mkurugenzi wa Nokia Tanzania,Martin Talbot ( kulia) akimvisha medali nahodha wa timu ya VodaStar, Ngayama Matongo baada ya kuilaza timu hiyo kwa magoli 8-1 wakati wa mechi yakirafiki uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mshambuliaji wa timu ya VodaStar, Ian Ferrao ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, (kushoto) akipongezwa na Mkurugenzi mtendaji wa Nokia Tanzania, Martin Talbot kwa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya kampuni hizo ambapo VodaStar iliichapa Nokia kwa magoli 8-1 mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Nahodha wa timu ya Nokia Tanzania,Charles Domingos(kulia) akiachia shuti kali na kuifungia goli timu yake na lapekee wakati wa mechi yakirafiki iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam kati ya timu yake na VodaStar ambapo VodaStar waliichakaza timu hiyo kwa magoli 8-1. Posted by MICHUZI BLOG at Monday, November 20, 2017 No comments: Links to this post Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest Mkurugenzi Mkazi wa USAID bwana Andy Karas atembelea walengwa wa TASAF mkoani Iringa. Na Estom Sanga – Iringa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada ya Kimataifa la Marekani –USAID-bwana Andy Karas amepongeza jitihada za serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika kuwafikia wananchi wanaokabiliwa na umasikini kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ambao umeanza kuonyesha mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali nchini, jambo linalovutia wadau wa maendeleo kuendelea kusaidia jitihada hizo. Bwana Karas ameyasema hayo alipokutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli katika halmashauri ya Wilaya ya Iringa ,mkoani Iringa ambako licha ya kuelezwa namna TASAF inavyoendelea kutekeleza Mpango huo, lakini pia alishuhudia namna walengwa wa mpango huo walivyoboresha maisha yao kwa kutumia fedha za ruzuku za mfuko huo. Amesema hamasa inayoonyeshwa na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kujiletea maendeleo kwa kuanzisha miradi midogo midogo kwa kutumia fedha zinazotolewa na Serikali kupitia TASAF, imelivutia Shirika hilo na kuahidi kuwa litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuboresha utaratibu wa kuwainua wananchi kiuchumi . Bwana Karas amesema utaratibu wa kuwafikia na kuwasaidia moja kwa moja wananchi wanaoishi katika mazingira magumu ya kiuchumi umekuwa ukitumika katika nchi nyingi duniani na umeonyesha mafanikio makubwa kwa kusisimua shughuli za kiuchumi na kijamii kwa kaya masikini . Aidha Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID amevutiwa na masharti ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kupitia TASAF hususani katika nyanja za elimu, afya, lishe na uwekezaji kwenye shughuli za kiuchumi kwa walengwa wa Mpango huo kuwa umeamusha ari ya kutokomeza umasikini miongoni mwao. Akiwa katika kijiji hicho cha Igingilanyi kata ya Nduli bwana Karas alitembelea baadhi ya kaya za Walengwa wa TASAF na kujionea namna walivyonufaika na ruzuku ya Mpango huo kwa kuanzisha miradi midogo midogo ya ufugaji wa kuku na nguruwe na kutumia sehemu ya mapato yao kuboresha makazi kwa kujenga nyumba za matofali na kuezeka kwa mabati. “ni jambo jema sana mnalolifanya kwa kuwekeza katika elimu ya watoto wenu na kuboresha makazi yenu kwa kutumia ruzuku mnayoipata” alisisitiza bwana Karas. Bwana Karas pia alionyesha kuvutiwa na utaratibu wa kuanzisha vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana unaofanywa na Walengwa wa Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini ambao alisema ukiimarishwa utatoa fursa kubwa zaidi kwa wananchi hao kukuza shughuli zao za kiuchumi kwa kukopeshana kwa riba ndogo ikilinganisha na ile inayotozwa na taasisi za kibenki. Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Miradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF,Bwana Amadeus Kamagenge alimweleza Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID kuwa licha ya Serikali kupitia Mfuko huo kuendelea kutoa ruzuku kwa Kaya Masikini sana katika mikoa yote nchni ,hivi sasa umeanza kujikita zaidi katika kuhamasisha walengwa kuanzisha vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana kwa kuwatumia wataalamu walioko kwenye maeneo yao wakiwemo Maafisa wa Maendeleo ya Jamii, kilimo, Mifugo na biashara ili waweze kuboresha shughuli za kiuchumi kwa walengwa. “Mkakati huo umeanza kuonyesha mafanikio kwa kuwaongezea walengwa kwa Mpango huo kipato na kuwapa uwezo wa kubuni na kusimamia kwa ufanisi miradi yao midogo midogo wanayoianzisha. Hata hivyo bwana Kamagenge amesema mafanikio yaliyoanza kupatikana kwa kaya za walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini yameibua kilio kutoka kwa kaya nyingine ambazo hazikuingizwa kuingizwa kwenye Mpango huo kutaka nazo pia zijumuishwe kwenye utaratibu huo. Hadi sasa TASAF inatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika vijiji 9,835 ambayo ni sawa na asilimia 70 ya vijiji na shehia zote Tanzania bara na Zanzibar. Mkurugenzi M kazi wa Shirika la Misaada la Marekani –USAID-bwana Andy Karas (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa walenwa wa TASAF katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli wilaya ya Iringa baada ya kutembelea nyumba aliyoijenga mlengwa huyo (nyuma yao ) baada ya kupata ruzuku kutoka TASAF. Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani USAID bwana Andy Karas akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF katika kijiji cha Igingilanyi wilaya ya Iringa Vijijini ambako akutana na walengwa wa Mpango huo kuona namna wanavyonufaika na Mpango huo. Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID bwana Andy Karas akisoma taarifa kwenye mkutano wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli wilaya ya Iringa Vijijini ambako alitembelea kuona namna walengwa wa Mpango huo wanavyonufaika na ruzuku inayotolewa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF. Baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi wilaya ya Iringa Vijijini wakiwaburudisha wageni kutoka Shirika la Misaada la Marekani –USAID waliotembelea kijiji hicho kuona shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF . Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani Bwana Andy Karas akisalimiana na mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli wilaya ya Iringa Vijijini wakati alipotembelea kijiji hicho.Katikati yao ni Mkurugenzi wa miradi wa TASAF bwana Amadeus Kamagenge. Posted by MICHUZI BLOG at Monday, November 20, 2017 No comments: Links to this post Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest BENKI YA KILIMO YATEMBELEA MIRADI YA JKT KITEULE CHA BULAMBA, BUNDA Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetembelea mradi wa ufugaji wa vifaranga vya samaki unaotekelezwa na kikosi cha 822 Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Rwamkoma wilaya ya Butiama kupitia Kiteule chake cha Bulamba, wilayani Bunda. Akizungumza lengo la ziara hiyo, mkuu wa msafara huo ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila amesema lengo kubwa la kutembelea Mradi huo ni kujionea juhudi za serikali za kuchagiza mapinduzi ya kilimo hasa katika tasnia ya ufugaji na uvuvi wa samaki nchini. Bibi Kurwijila aliongeza kuwa tasnia ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa ufugaji wa samaki nchini. Aliongeza kuwa Benki ya Kilimo imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Samaki na uvuvi nchini ili ziweze kuchangia ukuaji wa uchumi nchini. Mradi huo wa ufugaji wa samaki unaotekelezwa na JKT Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba ulizinduliwa rasmi mwezi Novembea, 2014 kwa kupandikiza vifaranga vya samaki katika vizimba ndani ya Ziwa Victoria. Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wakiwemo Economic Social Research Foundation (ESRF) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Ufugaji wa samaki kwa kutumia teknolojia ya vizimba ndani ya Ziwa Victoria, umekuwa maarufu zaidi katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Uganda na Kenya ambapo umepunguza kwa kiasi kikubwa uvuvi haramu katika fukwe za ziwa hilo. Afisa Kilimo na Ufugaji wa kikosi cha 822 Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Rwamkoma, Kapteni M. Kinana (kulia) akiongea na Ujumbe kutoka Benki ya Kilimo (hawapo pichani) walipotembelea mradi huo uliopo wilayani Bunda. Kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki wa JKT Kiteule cha Bulamba, Luteni Kelvin Gondo. Maafisa wa Jeshi la Kujenga Taifa wanaotekeleza Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwa Vizimba Kiteule cha Bulamba wakifuatilia mkutano wa pamoja kati ya JKT na Ujumbe kutoka Benki ya Kilimo. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (kulia) akizungumza wakati walipotembelea Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwa Vizimba Kiteule cha Bulamba uliopo wilaya ya Bunda, Mkoani Mara. Kushoto ni Afisa Uvuvi wa wilaya ya Bunda, Bw. Steven Ochieng’. Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Bw. Dome Malosha (kulia) akizungumza wakati walipotembelea Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwa Vizimba Kiteule cha Bulamba uliopo wilaya ya Bunda, Mkoani Mara. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Bw. Joseph Mutashubilwa (katikati). Afisa Uvuvi wa wilaya ya Bunda, Bw. Steven Ochieng’ (kushoto) akichangia wakati wa mazungumzo hayo. Anayemsikiliza ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (kulia). Msimamizi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki wa JKT Kiteule cha Bulamba, Luteni Kelvin Gondo akitoa maelezo juu ya maendeleo ya ufugaji wa samaki katika hatua mbalimbali. Posted by MICHUZI BLOG at Monday, November 20, 2017 No comments: Links to this post Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest MAHAFALI YA KWANZA YA CHUO CHA MANJANO BEAUTY ACADEMY YAFANYIKA JIJINI DAR Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama Sophia Mjema Akizungumza Machache wakati wa Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy .Ambapo amewataka Wanawake Kuchangamkia Fursa ya Urembo kwa kuwa ukuaji wake kwa sasa ni kubwa na inakabiliwa na Upungufu wa Wataalamu hivyo akiwashauri wanawake wengi Kujiunga na Kuiga Mambo Mazuri Yanayofanywa na Chuo cha Manjano Beauty Academy.Akieleza zaidi Alisema Sekta ya Urembo ina Fursa kubwa kwa Ajira kwa sasa,Katika Mahafali hayo Wahitimu 120 Wametunukiwa vyeti katika katika nyanja ya urembo. Mwanzilishi wa Chuo cha Manjano Beauty Academy Mama Shekha Nasser Akitoa Hotuba yake wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliofanyika Kwenye Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam.Mama Shekha Nasser Amewashukuru wazazi na walezi kwa kuwapeleka Watoto wao kwenye chuo hicho kwa LengoKupata Ujuzi wa Maswala ya Urembo,Aidha Ametaja Changamoto kubwa Alizokabiliana nazo wakati anaanzishi Chuo hicho Ikiwemo ukosefu wa Wataalamu wazawa wa Maswala ya Urembo. Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama Sophia Mjema Akiwa na Wageni Waalikwa wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy Baadhi ya Wahitimu waliotunukiwa kwenye Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy yaliofanyika Kwenye Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam Mshauri wa Maswala ya Kisaikolojia Anti Sadaka Akitoa Neno la Shukrani kwenye Mahafali hayo Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama Sophia Mjema Akitoa Cheti kwa Mmoja wa Wahitimu Kwenye Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy.. Mgeni Rasmi,Uongozi wa Chuo cha Manjano Bauty Academy ,Wageni waalikwa na Wahitimu Wakiwa katika Picha ya Pamoja Chuo cha Manjano Beauty Academy kimetunuku Astashahada (Certificates) na Stashahada (Diploma) kwa wahitimu 120 wa kwanza wa chuo hicho katika nyanja ya urembo na utengenezaji wa nywele.Urembo na mitindo ni moja kati ya sekta zinazoajiri mamilioni ya wanawake kwa sasa, lakini bado sekta hiyo imeendelea kuwa isiyo rasmi. Wanawake wengi wanaofanya kazi kwenye saluni hawana utaalamu, lakini ndiyo wanaofuatwa na wanaume na wanawake kwa ajili ya kutengenezwa mionekano inayovutia, wanaishi kwa kufanya kazi kubahatisha. Akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya Manjano Beauty Academy iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwanzilishi wa Manjano Beauty Academy, Shekha Nasser alisema kuwa maono hayo ndiyo yaliyosababisha yeye kuanzisha Manjano Beauty Academy.Manjano Beauty Academy ni shule kwa ajili ya afya na urembo ambayo ina lengo la kuwawezesha wasichana wa Kitanzania. “Tunashauri, tunatoa mafunzo na kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya soko kwa kuwapatia ujuzi unaohitajika. Serikali haiwezi kuwaajiri wahitimu wote, hata sekta binafsi haiwezi kwa hivi sasa, kwa hiyo mafunzo haya yanawasaidia wasichana wadogo kuweza kujitengenezea soko kwenye sekta ya urembo,” alisema Shekha.Kwa mujibu wa Shekha, wasichana hao wamekuwa wakipewa mafunzo na wakufunzi bora wanaopatikana katika sekta ya urembo ambayo yatawatasaidia wao kutimiza malengo yao binafsi pamoja na malengo ya kitaasisi. “Naamini kuwa wahitimu hawa watabadilisha sekta ya urembo hapa nchini, kama Korea na Filipino wanavyotambulika ulimwenguni kwa kuwa na bidhaa bora za ngozi na wataalam wa matibabu wenye weledi, huko mbeleni Tanzania itajulikana ni nchi inayotoa bidhaa bora za urembo kwa ngozi za Kiafrika, kuanzia bidhaa za urembo wa uso zinazozalishwa kutokana na Mwani wa baharini toka Zanzibar mpaka bidhaa za poda ambazo zina virutubisho vya Manjano ya asili na vyakutosha,” alisema Shekha ambaye pia ni mwanzilishi wa Shear Illusions. Mwaka 2015, kupitia bidhaa za LuvTouch Manjano, Shekha alizindua kampeni inayoitwa Manjano Dream Makers iliyokuwa na lengo la kuwawezesha wasichana wenye mafunzo ya kijasiriamali kujikwamua kiuchumi ili kutimiza ndoto zao. “Katika miaka miwili tangu kuanzishwa kwa taasisi ya Manjano, mtandao wa wanawake wa Manjano Dream-Makers umeweza kuenea katika majiji na miji Saba nchini na kuwasaidia kutengeneza ajira na kutengeneza kipato kwa kuuza bidhaa zao kupitia mfumo wa nyumba kwa nyumba kwa wanawake wasio na ajira,” alisema Shekha. Aliongeza kuwa, “Leo tunajivunia kuwa na wasichana 360 katika mtandao wa ‘Manjano Dream-Makers’ wenye matumaini ya kuboresha maisha yao na familia zao kwa kuuza bidhaa za LuvTouch Manjano. Posted by MICHUZI BLOG at Monday, November 20, 2017 No comments: Links to this post Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest CHAMA CHA MBIO ZA MAGARI TANZANIA (AAT) CHAWAKUMBUKA WAATHIRIKA WA AJALI NA KUJADILIANA NA WADAU NAMNA YA KUZIPUNGUZA 1 Mgeni Rasmi Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Afande Deus Sokoni akifungua mjadala katika Siku ya Kukumbuka waathirika wa Ajali Duniani (The World Day Of Remembrance For Road Traffic Victims 19 November 2017) iliyoandaliwa na kufanyika kwenye ofisi za Chama Cha Mbio za Magari Tanzania AAT Upanga jijini Dar es salaam ikishirikisha wadau kutoka taasisi mbalimbali nchini Tanzania. Wadau mbalimbali wamekutana na kujadiliana namna ya kupunguza ajali hasa katika kuzipitia sheria za usalama barabarani na kuzifanyia marekebisho pamoja na kuwakumbusha watumiaji wa Barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani, Taasisi zilizoshiriki katika mjadala huo ni WHO, KIkosi Cha Usalama Barabarani, SUMATRA, Chama Cha Mbizo za Magari Tanzania AAT, Chama cha Kutetea Abiria Tanzania CHAKUA, TIRA na wawakilishi Idara ya Habari Maelezo. 2 Mratibu wa Semina hiyo Bw. Alferio Nchimbi akizungumza katika semina hiyo na kukaribisha wadau mbalimbai ili kuchangia michango yao katika mada mbalimbali zilizowasilishwa. 3 Mgeni Rasmi Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Afande Deus Sokoni akisisitiza jambo wakati akijibu maswali katika semina hiyo kulia ni Mratibu wa Semina hiyo Bw. Alferio Nchimbi. 4 Bw. Monday Likwepa Katibu Mkuu wa Chama cha Kutetea Abiria akichangia mada katika semina hiyo. 5 Bi Mary Kessi Mratibu Programu ya Usalama Barabarani WHO akitoa mada katika semina hiyo iliyofanyika kwenye ofisi za Chama cha Mbio za Magari Tanzania (AAT) Upanga jijini Dar es salaam. 6 Afisa Leseni Mwandamizi kutoka SUMATRA Bw. Gabriel Anthony akitoa mada katika semina hiyo. 7 Daktari Bingwa wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharura na Ajali Muhimbili Dk Juma Mfinanga akitoa ufafanuzi kwa upande wa hospitali ya Muhimbili wakati wa semina hiyo. 8 Baadhi ya washiriki wakiwa katika semiha hiyo 9 10 Posted by MICHUZI BLOG at Monday, November 20, 2017 No comments: Links to this post Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest KABURI LAFUKULIWA MOSHI KUONDOA UTATA WA MWILI WA MTU ALIYEZIKWA BAADA YA KUOKOTWA MTONI Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. UTATA umeighubika familia ya Jackson Makundi ambayo kijana wake aliyetambulika kwa jina la Humphrey Makundi,Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo kupotea katika mazingira tatanishi. Utata wa kupotea kwa mwanafunzi huyo unatiliwa shaka zaidi na familia hiyo baada ya kufukuliwa kwa kaburi ulimozikwa mwili uliookotwa mto Ghona mita 300 ,jirani na shule hiyo ukidaiwa kushabihiana na wa mwanafunzi huyo. Humphrey Makundi, mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Scolastica anatajwa kupotea tangu Novemba 7 mwaka huu akiwa shuleni hapo huku wanafunzi wenzake wakiendelea na mitihani ya kidato cha Pili ya upimaji ya kitaifa . Familia ya kijana huyo yenye makazi yake mkoani Dodoma ikalazimika kutumia mitandao ya kijamii kutoa taarifa za kupotea kwake ikidai mazingira ya kutoweka kwake ni ya kutatanisha na baadae kuwasilisha taarifa katika kituo cha Polisi cha Himo . Kutokana na kuwepo kwa taarifa za kuokotwa kwa mwili huo ,familia iliwasilisha maombi katika mahakama ya Hakimu Mkazi, Moshi na mahakama ikaamuru kufukuliwa kwa Kaburi hilo zoezi lililoanza majira ya saa 8:30 mchana na kudumu kwa zaidi ya saa moja. Jeshi la Polisi liliongoza zoezi hilo katika makaburi ya Karanga huku likishuhudiwa na ndugu wa mtoto aliyepotea ambapo baada ya mwili kutolewa kaburini hali ya simanzi ilionekana katika nyuso za baadhi ya ndugu wa Mwanafunzi huyo akiwemo baba mzazi wa kijana huyo. Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issa akathibitisha uwepo wa tukio hilo huku akieleza kuwa tayari jeshi la Polisi linawashikilia wati 11 akiwemo mmiliki wa shule hiyo Edward Shayo huku likifanya uchunguzi wa kina kuhusu matukio hayo mawili. Mwili uliofukuliwa katika makaburi ya Karanga upande wa marehemu wasiokuwa na ndugu ulipelekewa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya KCMC kwa uchunguzi zaidi chini ya uangalizi wa jeshi la Polisi wakishirikiana na madaktari kutoka KCMC. Jeshi la Polisi likiwa limezungushia utepe eneo ambalo kuna kaburi ulimozikwa mwili ambao familia ya Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo aliyepotea ,Humphrey Makundi ulitilia shaka. Kaburi ulimozikwa mwili wa mtu aliyezikwa na Manispaa ya Moshi baada ya kuokotwa Mto Ghona jirani na ilipo shule ya Sekondari . Askari Polisi wakishirikiana na ndugu wa Mwanafunzi aliyepotea Humphrey Makundi wakifukua Kaburi ulimozikwa mwili wa mtu aliyeokotwa Mto Ghona katika wilaya ya Moshi. Kaburi likifukuliwa. Baba mzazi wa Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Scolastica aliyepotea,Jackson Makundi (Katkati) akijadili jambo na wanandugu wakati zoezi la kufukua kaburi likiendelea. Baba mzazi wa Mwanafunzi Humphrey ,Jackson Makundi (Mwenye suti nyeupe) akitizama mwili (haupo pichani) baada ya kaburi kufukuliwa. Baba mzazi wa Mwanafunzi Humphrey ,Jackson Makundi (Mwenye suti nyeupe) akionekana akiwa amekaa chini baada ya kutizama mwili uliofukuliwa katika kaburi . Askari Polisi na Wanandugu wa kijana aliyepotea wakijaribu kusaidia kumnyanyua mzazi wa Mwanafunzi huyo kutoka katika eneo lilipo kaburi lililofukuliwa . Baba mzazi wa Mwanafunzi Humphrey ,Jackson Makundi (Mwenye suti nyeupe) akisindikizwa kutoka katika eneo la Makaburi ya Karanga katika manispaa ya Moshi. Mwili uliofukuliwa katika makaburi hayo ukiwekwa katika gari la Polisi kwa ajili ya kwenda kuhifadhiwa katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC. Gari la Polisi likiwa na mwili uliofukuliwa katika Makaburi ya Karanga.

WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI LA UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE

 Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98  leo jijini Dar es salaam .
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akipokea moja ya vifaa vya uchunguzi wa saratani ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran (kushoto) wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam.
 Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akipokea moja ya nyenzo za  kufundishia juu ya uchunguzi wa saratani ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran (kushoto) wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam katikati ni Afisa Afya kutoka USAID Bi. Ananth Thambinygan .
 Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98  leo jijini Dar es salaam .
Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu  (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa  Wizara ya afya, Jpiego na USAID wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98  leo jijini Dar es salaam wa tatu kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran na aliyevaa nguo ya pundamilia ni Afisa Afya kutoka USAID Bi. Ananth Thambinygan .picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

WAZIRI Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amewaelekeza waganga wakuu wa mikoa yote nchini kuanzisha zoezi la wazi la uchunguzi wa saratani ya kizazi angalau mara moja katika mwezi ili kusaidia kutokomeza tatizo kwa wanawake hilo nchini.

Hayo amesema wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98  ambavyo vimetolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya JHPIEGO kwa kushirikiana na USAID ili kusaidia kupambana na tatizo hilo nchini.

“Angalau ifikapo Desemba 2018 nataka  vituo vya Afya vya Serikali  524  viwe vinatoa huduma ya matibabu ya awali ya Saratani ya mlango wa kizazi na kufikia  wanawake milioni 3 watakaopata huduma hii ili kuokoa wanawake wa vijijini  kwani mpaka sasa hivi tunavyo vituo vya afya  265 vinavyotoa huduma hii ” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa uchunguzi na kutoa chanjo ya Saratani ya mlango wa kikazi  kwa wasichana kuanzia miaka 9 mpaka 14 ili kuweza kupunguza vifo vitokanavyo na tatizo hilo kwani katika kila wanawake 100 vifo vinavyotokana na ugonjwa huo ni 32.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa katika kuongeza jitihada za  kupambana na ugonjwa huo Serikali imeongeza vituo vya afya 100 kutoka 343  hadi kufikia 443 mwaka huu ili kutokomeza tatizo hilo nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran amesema kuwa walianzisha mpango wa kupambana na tatizo hilo na kufanikiwa kuwafikia wanawake elfu 75 kwa mikoa 4 tangu mwaka 2009.

“Mbali na mikoa hiyo 4 bado tunalengo la kuongeza mikoa mingine 7 ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa ajili ya kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi ili kuweza kuokoa wanawake wengi zaidi nchini” alisema Bw. Zoungran.

VODASTAR YAICHAKAZA NOKIA MAGOLI 8-1 MECHI YAKIRAFIKI

 Mshambuliaji wa timu ya VodaStar, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (wapili kulia)akishangilia goli baada ya kuifungia timu yake  wakati wa mchezo wakirafiki dhidi ya  timu ya Nokia uliofanyika katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam,VodaStar iliiadhibu Nokia kwa magoli 8-1.
 Wachezaji wa timu ya VodaStar,wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (wapili kulia mwenye miwani) wakishangilia kombe lao baada ya kuihadabisha timu ya Nokia kwa magoli 8-1 wakati wa mchezo wakirafiki uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Kikosi cha timu ya VodaStar kilichoisambaratisha timu ya Nokia kwa magoli 8-1 wakati wa mechi yakirafiki wakiwa katika picha ya pamoja  baada ya mechi hiyo kuisha iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mashabiki watimu ya VodaStar, wakifurahia kombe lao  baada ya timu yao kiichakaza timu ya Nokia kwa magoli 8-1 wakati wamchezo wakirafiki uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (kushoto) akimshuhudia Mkurugenzi wa Nokia Tanzania,Martin Talbot ( kulia) akimvisha medali nahodha wa timu ya VodaStar, Ngayama Matongo baada ya kuilaza timu hiyo kwa magoli 8-1 wakati wa mechi yakirafiki  uliofanyika katika  viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mshambuliaji wa timu ya  VodaStar, Ian Ferrao ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, (kushoto) akipongezwa na Mkurugenzi mtendaji wa Nokia Tanzania, Martin Talbot  kwa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo  wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya kampuni hizo ambapo VodaStar iliichapa Nokia kwa magoli 8-1 mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Nahodha wa timu ya Nokia Tanzania,Charles Domingos(kulia) akiachia shuti kali na kuifungia goli timu yake na lapekee wakati wa mechi yakirafiki iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam kati ya timu yake na VodaStar ambapo VodaStar waliichakaza timu hiyo kwa magoli 8-1.

Mkurugenzi Mkazi wa USAID bwana Andy Karas atembelea walengwa wa TASAF mkoani Iringa.


Na Estom Sanga – Iringa

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada ya Kimataifa la Marekani –USAID-bwana Andy Karas amepongeza jitihada za serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika kuwafikia wananchi wanaokabiliwa na umasikini kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ambao umeanza kuonyesha mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali nchini, jambo linalovutia wadau wa maendeleo kuendelea kusaidia jitihada hizo.

Bwana Karas ameyasema hayo alipokutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli katika halmashauri ya Wilaya ya Iringa ,mkoani Iringa ambako licha ya kuelezwa namna TASAF inavyoendelea kutekeleza Mpango huo, lakini pia alishuhudia namna walengwa wa mpango huo walivyoboresha maisha yao kwa kutumia fedha za ruzuku za mfuko huo.

Amesema hamasa inayoonyeshwa na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kujiletea maendeleo kwa kuanzisha miradi midogo midogo kwa kutumia fedha zinazotolewa na Serikali kupitia TASAF, imelivutia Shirika hilo na kuahidi kuwa litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuboresha utaratibu wa kuwainua wananchi kiuchumi .

Bwana Karas amesema utaratibu wa kuwafikia na kuwasaidia moja kwa moja wananchi wanaoishi katika mazingira magumu ya kiuchumi umekuwa ukitumika katika nchi nyingi duniani na umeonyesha mafanikio makubwa kwa kusisimua shughuli za kiuchumi na kijamii kwa kaya masikini .

Aidha Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID amevutiwa na masharti ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kupitia TASAF hususani katika nyanja za elimu, afya, lishe na uwekezaji kwenye shughuli za kiuchumi kwa walengwa wa Mpango huo kuwa umeamusha ari ya kutokomeza umasikini miongoni mwao.

Akiwa katika kijiji hicho cha Igingilanyi kata ya Nduli bwana Karas alitembelea baadhi ya kaya za Walengwa wa TASAF na kujionea namna walivyonufaika na ruzuku ya Mpango huo kwa kuanzisha miradi midogo midogo ya ufugaji wa kuku na nguruwe na kutumia sehemu ya mapato yao kuboresha makazi kwa kujenga nyumba za matofali na kuezeka kwa mabati.

“ni jambo jema sana mnalolifanya kwa kuwekeza katika elimu ya watoto wenu na kuboresha makazi yenu kwa kutumia ruzuku mnayoipata” alisisitiza bwana Karas.

Bwana Karas pia alionyesha kuvutiwa na utaratibu wa kuanzisha vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana unaofanywa na Walengwa wa Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini ambao alisema ukiimarishwa utatoa fursa kubwa zaidi kwa wananchi hao kukuza shughuli zao za kiuchumi kwa kukopeshana kwa riba ndogo ikilinganisha na ile inayotozwa na taasisi za kibenki.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Miradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF,Bwana Amadeus Kamagenge alimweleza Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID kuwa licha ya Serikali kupitia Mfuko huo kuendelea kutoa ruzuku kwa Kaya Masikini sana katika mikoa yote nchni ,hivi sasa umeanza kujikita zaidi katika kuhamasisha walengwa kuanzisha vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana kwa kuwatumia wataalamu walioko kwenye maeneo yao wakiwemo Maafisa wa Maendeleo ya Jamii, kilimo, Mifugo na biashara ili waweze kuboresha shughuli za kiuchumi kwa walengwa.

“Mkakati huo umeanza kuonyesha mafanikio kwa kuwaongezea walengwa kwa Mpango huo kipato na kuwapa uwezo wa kubuni na kusimamia kwa ufanisi miradi yao midogo midogo wanayoianzisha.

Hata hivyo bwana Kamagenge amesema mafanikio yaliyoanza kupatikana kwa kaya za walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini yameibua kilio kutoka kwa kaya nyingine ambazo hazikuingizwa kuingizwa kwenye Mpango huo kutaka nazo pia zijumuishwe kwenye utaratibu huo. Hadi sasa TASAF inatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika vijiji 9,835 ambayo ni sawa na asilimia 70 ya vijiji na shehia zote Tanzania bara na Zanzibar.


Mkurugenzi M kazi wa Shirika la Misaada la Marekani –USAID-bwana Andy Karas (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa walengwa wa TASAF katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli wilaya ya Iringa baada ya kutembelea nyumba aliyoijenga mlengwa huyo (nyuma yao ) baada ya kupata ruzuku kutoka TASAF.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani USAID bwana Andy Karas akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF katika kijiji cha Igingilanyi wilaya ya Iringa Vijijini ambako akutana na walengwa wa Mpango huo kuona namna wanavyonufaika na Mpango huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID bwana Andy Karas akisoma taarifa kwenye mkutano wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli wilaya ya Iringa Vijijini ambako alitembelea kuona namna walengwa wa Mpango huo wanavyonufaika na ruzuku inayotolewa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.
Baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi wilaya ya Iringa Vijijini wakiwaburudisha wageni kutoka Shirika la Misaada la Marekani –USAID waliotembelea kijiji hicho kuona shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF .
Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani Bwana Andy Karas akisalimiana na mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli wilaya ya Iringa Vijijini wakati alipotembelea kijiji hicho.Katikati yao ni Mkurugenzi wa miradi wa TASAF bwana Amadeus Kamagenge.

BENKI YA KILIMO YATEMBELEA MIRADI YA JKT KITEULE CHA BULAMBA, BUNDA

Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetembelea mradi wa ufugaji wa vifaranga vya samaki unaotekelezwa na kikosi cha 822 Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Rwamkoma wilaya ya Butiama kupitia Kiteule chake cha Bulamba, wilayani Bunda.

Akizungumza lengo la ziara hiyo, mkuu wa msafara huo ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila amesema lengo kubwa la kutembelea Mradi huo ni kujionea juhudi za serikali za kuchagiza mapinduzi ya kilimo hasa katika tasnia ya ufugaji na uvuvi wa samaki nchini.

Bibi Kurwijila aliongeza kuwa tasnia ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa ufugaji wa samaki nchini.

Aliongeza kuwa Benki ya Kilimo imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Samaki na uvuvi nchini ili ziweze kuchangia ukuaji wa uchumi nchini.

Mradi huo wa ufugaji wa samaki unaotekelezwa na JKT Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba ulizinduliwa rasmi mwezi Novembea, 2014 kwa kupandikiza vifaranga vya samaki katika vizimba ndani ya Ziwa Victoria.
Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wakiwemo Economic Social Research Foundation (ESRF) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Ufugaji wa samaki kwa kutumia teknolojia ya vizimba ndani ya Ziwa Victoria, umekuwa maarufu zaidi katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Uganda na Kenya ambapo umepunguza kwa kiasi kikubwa uvuvi haramu katika fukwe za ziwa hilo.
 Afisa Kilimo na Ufugaji wa kikosi cha 822 Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Rwamkoma, Kapteni M. Kinana (kulia) akiongea na Ujumbe kutoka Benki ya Kilimo (hawapo pichani) walipotembelea mradi huo uliopo wilayani Bunda. Kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki wa JKT Kiteule cha Bulamba, Luteni Kelvin Gondo.
 Maafisa wa Jeshi la Kujenga Taifa wanaotekeleza Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwa Vizimba Kiteule cha Bulamba wakifuatilia mkutano wa pamoja kati ya JKT na Ujumbe kutoka Benki ya Kilimo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (kulia) akizungumza wakati walipotembelea Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwa Vizimba Kiteule cha Bulamba uliopo wilaya ya Bunda, Mkoani Mara. Kushoto ni Afisa Uvuvi wa wilaya ya Bunda, Bw. Steven Ochieng’.
 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Bw. Dome Malosha (kulia) akizungumza wakati walipotembelea Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwa Vizimba Kiteule cha Bulamba uliopo wilaya ya Bunda, Mkoani Mara. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Bw. Joseph Mutashubilwa (katikati).
 Afisa Uvuvi wa wilaya ya Bunda, Bw. Steven Ochieng’ (kushoto) akichangia wakati wa mazungumzo hayo. Anayemsikiliza ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (kulia).
Msimamizi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki wa JKT Kiteule cha Bulamba, Luteni Kelvin Gondo akitoa maelezo juu ya maendeleo ya ufugaji wa samaki katika hatua mbalimbali.

MAHAFALI YA KWANZA YA CHUO CHA MANJANO BEAUTY ACADEMY YAFANYIKA JIJINI DAR

 
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama  Sophia Mjema Akizungumza Machache wakati wa Mahafali  ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy .Ambapo amewataka Wanawake Kuchangamkia Fursa ya Urembo kwa kuwa ukuaji wake kwa sasa ni kubwa na inakabiliwa na Upungufu wa Wataalamu hivyo akiwashauri wanawake wengi Kujiunga na Kuiga Mambo Mazuri Yanayofanywa na Chuo cha Manjano Beauty Academy.Akieleza zaidi Alisema Sekta ya Urembo ina Fursa kubwa kwa Ajira kwa sasa,Katika Mahafali hayo  Wahitimu 120 Wametunukiwa vyeti katika  katika nyanja ya urembo.
Mwanzilishi wa Chuo cha  Manjano Beauty Academy Mama Shekha Nasser Akitoa Hotuba yake wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliofanyika Kwenye Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam.Mama Shekha Nasser Amewashukuru wazazi na walezi kwa kuwapeleka Watoto wao kwenye chuo hicho kwa LengoKupata Ujuzi wa Maswala ya Urembo,Aidha Ametaja Changamoto kubwa Alizokabiliana nazo wakati anaanzishi Chuo hicho Ikiwemo ukosefu wa Wataalamu wazawa wa Maswala ya Urembo.
 Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama  Sophia Mjema Akiwa na Wageni Waalikwa wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy 
 Baadhi ya  Wahitimu waliotunukiwa kwenye Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy yaliofanyika Kwenye Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam

 Mshauri wa Maswala ya Kisaikolojia Anti Sadaka Akitoa Neno la Shukrani kwenye Mahafali hayo
 Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama  Sophia Mjema  Akitoa Cheti kwa Mmoja wa Wahitimu Kwenye  Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy..
 Mgeni Rasmi,Uongozi wa Chuo cha Manjano Bauty Academy ,Wageni waalikwa na Wahitimu Wakiwa katika Picha ya Pamoja 

Chuo cha Manjano Beauty Academy  kimetunuku Astashahada (Certificates) na Stashahada (Diploma) kwa wahitimu 120 wa kwanza wa chuo hicho katika nyanja ya urembo na utengenezaji wa nywele.Urembo na mitindo ni moja kati ya sekta zinazoajiri mamilioni ya wanawake kwa sasa, lakini bado sekta hiyo imeendelea kuwa isiyo rasmi.
Wanawake wengi wanaofanya kazi kwenye saluni hawana utaalamu, lakini ndiyo wanaofuatwa na wanaume na wanawake kwa ajili ya kutengenezwa mionekano inayovutia, wanaishi kwa kufanya kazi kubahatisha.


Akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya  Manjano Beauty Academy iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwanzilishi wa Manjano Beauty Academy, Shekha Nasser alisema kuwa maono hayo ndiyo yaliyosababisha yeye kuanzisha Manjano Beauty Academy.Manjano Beauty Academy ni shule kwa ajili ya afya na urembo ambayo ina lengo la kuwawezesha wasichana wa Kitanzania.
“Tunashauri, tunatoa mafunzo na kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya soko kwa kuwapatia ujuzi unaohitajika. Serikali haiwezi kuwaajiri wahitimu wote, hata sekta binafsi haiwezi kwa hivi sasa, kwa hiyo mafunzo haya yanawasaidia wasichana wadogo kuweza kujitengenezea soko kwenye sekta ya urembo,” alisema Shekha.Kwa mujibu wa Shekha, wasichana hao wamekuwa wakipewa mafunzo na wakufunzi bora wanaopatikana katika sekta ya urembo  ambayo yatawatasaidia wao kutimiza malengo yao binafsi pamoja na malengo ya kitaasisi.
 “Naamini kuwa wahitimu hawa watabadilisha sekta ya urembo hapa nchini, kama Korea na Filipino wanavyotambulika ulimwenguni kwa kuwa na bidhaa bora za ngozi na wataalam wa matibabu wenye weledi, huko mbeleni Tanzania itajulikana ni nchi inayotoa bidhaa bora za urembo kwa ngozi za Kiafrika, kuanzia bidhaa za urembo wa uso zinazozalishwa kutokana na Mwani wa baharini toka Zanzibar mpaka bidhaa za poda ambazo zina virutubisho vya Manjano ya asili na vyakutosha,” alisema Shekha ambaye pia ni mwanzilishi wa Shear Illusions.
Mwaka 2015, kupitia bidhaa za LuvTouch Manjano, Shekha alizindua kampeni inayoitwa Manjano Dream Makers iliyokuwa na lengo la kuwawezesha wasichana wenye mafunzo ya kijasiriamali kujikwamua kiuchumi ili kutimiza ndoto zao.
“Katika miaka miwili tangu kuanzishwa kwa taasisi ya Manjano, mtandao wa wanawake wa Manjano Dream-Makers umeweza kuenea katika majiji na miji Saba nchini na kuwasaidia kutengeneza ajira na kutengeneza kipato kwa kuuza bidhaa zao kupitia mfumo wa nyumba kwa nyumba kwa wanawake wasio na ajira,” alisema Shekha. 

Aliongeza kuwa, “Leo tunajivunia kuwa na wasichana 360 katika mtandao wa ‘Manjano Dream-Makers’ wenye matumaini ya kuboresha maisha yao na familia zao kwa kuuza bidhaa za LuvTouch Manjano.

CHAMA CHA MBIO ZA MAGARI TANZANIA (AAT) CHAWAKUMBUKA WAATHIRIKA WA AJALI NA KUJADILIANA NA WADAU NAMNA YA KUZIPUNGUZA

1
Mgeni Rasmi Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Afande Deus Sokoni akifungua mjadala katika Siku ya Kukumbuka waathirika wa Ajali Duniani (The World Day Of Remembrance For Road Traffic Victims 19 November 2017) iliyoandaliwa na kufanyika kwenye ofisi za Chama Cha Mbio za Magari Tanzania AAT Upanga jijini Dar es salaam ikishirikisha wadau kutoka taasisi mbalimbali nchini Tanzania.
Wadau mbalimbali wamekutana na kujadiliana namna ya kupunguza ajali hasa katika kuzipitia sheria za usalama barabarani na kuzifanyia marekebisho pamoja na kuwakumbusha watumiaji wa Barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani, Taasisi zilizoshiriki katika mjadala huo ni WHO, KIkosi Cha Usalama Barabarani, SUMATRA, Chama Cha Mbizo za Magari Tanzania AAT, Chama cha Kutetea Abiria Tanzania CHAKUA, TIRA na wawakilishi Idara ya Habari Maelezo.
2
Mratibu wa Semina hiyo Bw. Alferio Nchimbi akizungumza katika semina hiyo na kukaribisha wadau mbalimbai ili kuchangia michango yao katika mada mbalimbali zilizowasilishwa.
3
Mgeni Rasmi Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Afande Deus Sokoni akisisitiza jambo wakati akijibu maswali katika semina hiyo kulia ni Mratibu wa Semina hiyo Bw. Alferio Nchimbi.
4
Bw. Monday Likwepa Katibu Mkuu wa Chama cha Kutetea Abiria akichangia mada katika semina hiyo.
5
Bi Mary Kessi Mratibu Programu ya Usalama Barabarani WHO akitoa mada katika semina hiyo iliyofanyika kwenye ofisi za Chama cha Mbio za Magari Tanzania (AAT) Upanga jijini Dar es salaam.
6
Afisa Leseni Mwandamizi kutoka SUMATRA Bw. Gabriel Anthony akitoa mada katika semina hiyo.
7
Daktari Bingwa wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharura na Ajali Muhimbili Dk Juma Mfinanga akitoa ufafanuzi kwa upande wa hospitali ya Muhimbili wakati wa semina hiyo.
8
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semiha hiyo
9 10

KABURI LAFUKULIWA MOSHI KUONDOA UTATA WA MWILI WA MTU ALIYEZIKWA BAADA YA KUOKOTWA MTONI

Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
 UTATA umeighubika familia ya Jackson Makundi ambayo kijana wake aliyetambulika kwa jina la Humphrey Makundi,Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo kupotea katika mazingira tatanishi.
 Utata wa kupotea kwa mwanafunzi huyo unatiliwa shaka zaidi na familia hiyo baada ya kufukuliwa kwa kaburi ulimozikwa mwili uliookotwa mto Ghona mita 300 ,jirani na shule hiyo ukidaiwa kushabihiana na wa mwanafunzi huyo.
  Humphrey Makundi, mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Scolastica anatajwa kupotea tangu Novemba 7 mwaka huu akiwa shuleni hapo huku wanafunzi wenzake wakiendelea na mitihani ya kidato cha Pili ya upimaji ya kitaifa .

 Familia ya kijana huyo yenye makazi yake mkoani Dodoma ikalazimika kutumia mitandao ya kijamii kutoa taarifa za kupotea kwake ikidai mazingira ya kutoweka kwake ni ya kutatanisha na baadae kuwasilisha taarifa katika kituo cha Polisi cha Himo .

Kutokana na kuwepo kwa taarifa za kuokotwa kwa mwili huo ,familia iliwasilisha maombi katika mahakama ya Hakimu Mkazi, Moshi na mahakama ikaamuru kufukuliwa kwa Kaburi hilo zoezi lililoanza majira ya saa 8:30 mchana na kudumu kwa zaidi ya saa moja.
Jeshi la Polisi liliongoza zoezi hilo katika makaburi ya Karanga huku likishuhudiwa na ndugu wa mtoto aliyepotea ambapo baada ya mwili kutolewa kaburini hali ya simanzi ilionekana katika nyuso za baadhi ya ndugu wa Mwanafunzi huyo akiwemo baba mzazi wa kijana huyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issa akathibitisha uwepo wa tukio hilo huku akieleza kuwa tayari jeshi la Polisi linawashikilia wati 11 akiwemo mmiliki wa shule hiyo Edward Shayo huku likifanya uchunguzi wa kina kuhusu matukio hayo mawili.
Mwili uliofukuliwa katika makaburi ya Karanga upande wa marehemu wasiokuwa na ndugu ulipelekewa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya KCMC kwa uchunguzi zaidi chini ya uangalizi wa jeshi la Polisi wakishirikiana na madaktari kutoka  KCMC.
Jeshi la Polisi likiwa limezungushia utepe eneo ambalo kuna kaburi ulimozikwa mwili ambao familia ya Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo aliyepotea ,Humphrey Makundi ulitilia shaka.
Kaburi ulimozikwa mwili wa mtu aliyezikwa na Manispaa ya Moshi baada ya kuokotwa Mto Ghona jirani na ilipo shule ya Sekondari .
Askari Polisi wakishirikiana na ndugu wa Mwanafunzi aliyepotea Humphrey Makundi wakifukua Kaburi ulimozikwa mwili wa mtu aliyeokotwa Mto Ghona katika wilaya ya Moshi.
Kaburi likifukuliwa.
Baba mzazi wa Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Scolastica aliyepotea,Jackson Makundi (Katkati) akijadili jambo na wanandugu wakati zoezi la kufukua kaburi likiendelea.
Baba mzazi wa Mwanafunzi Humphrey ,Jackson Makundi (Mwenye suti nyeupe) akitizama mwili (haupo pichani) baada ya kaburi kufukuliwa.
Baba mzazi wa Mwanafunzi Humphrey ,Jackson Makundi (Mwenye suti nyeupe) akionekana akiwa amekaa chini baada ya kutizama mwili uliofukuliwa katika kaburi .
Askari Polisi na Wanandugu wa kijana aliyepotea wakijaribu kusaidia kumnyanyua mzazi wa Mwanafunzi huyo kutoka katika eneo lilipo kaburi lililofukuliwa .
Baba mzazi wa Mwanafunzi Humphrey ,Jackson Makundi (Mwenye suti nyeupe) akisindikizwa kutoka katika eneo la Makaburi ya Karanga katika manispaa ya Moshi.
Mwili uliofukuliwa katika makaburi hayo ukiwekwa katika gari la Polisi kwa ajili ya kwenda kuhifadhiwa katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC.
Gari la Polisi likiwa na mwili uliofukuliwa katika Makaburi ya Karanga.

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA