MATUKIO MBALIMBALI MIAKA YA NYUMA HEBU JIKUMBUSHE

 Leo nimeamua kuwaletea matukio ya picha mbalimbali nilizowahi kuzipiga siku za nyuma baadhi nikiwa papalazi wenzangu tukiwajibika sehemu mbalimbali, kama hawa ni papalazi walikuwa wakipiga picha  tukio la Miss Tanzania miaka ya 2005
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mwanayamala, Rajab Mwilima Mfwakwenda , akiwa katika hafdla ya kuwapongeza wajumbe wake waliofanikisha kuchaguliwa kwake hata hivyo fitna za viongozi wa wilaya ya kinondoni zilizokuwa zikiongozwa na KatibuMmwenezi wa wakati huo aliweza kuvuliwa uanachama kwa madai eti siyo raia wa nchi hiim hata hivyo alilejeshewa uraia wake na kumshitaki aliyemzushia hivyo na sasa hivi anadai mamilioni ya fidia.


Waliokuwa vinara wa upinzani kutoka CUF, wakiktumikia chama cha mapinduzi baada ya kuhama walikokuwa, hata hivyo hivi sasa Tambwe hizza, kalejea upinzani sifahamu Msabaha salum yupo wapi
 Waziri Mkuu Sumaye na Dk Ayoub Lyioba kwenye hafla ya kuchangia waandishi wa habari wanawake
Mgaya kingoba, akichangia katika hafla hiyo
Shayrose Bhanji nae akinunua picha ya Waziri Mkuu ikiwa ni kuchangia
Kingwangala, akiwa na madaktari wenzake katika mgomo waluouitisha miaka hiyo hivi sasa ni naibu waziri wa Afya
Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi koa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe akiwa na mabunda ya fedha alizodai walizikamata kwa majambazi waliowaua katika msitu wapande hata hivyo ilikuja kujulikana badae kwamba waliowaua ni wafanyabishara wa madini kutoka Ifakara mkoani Morogoro
 Akionyesha bastora waliyokuwa nayo watuhumiwa kumbe walikuiwa wakiimiliki kiharari.
 Mgombea wa CCM, urais, Jakaya Kikwete, akiwa na mwalimu wake aliyemfundiusha darasa la tatu na hapa alimkuta katika kijiji cha Matombo mkoani Morogoro akiwa katika kampeni
 Hapa Viwanja vya jangwani baada  ya kumalizika kampeni
Mwenyekiti wa Umoajwa Vijana wa CCM, Dk. John Nchimbi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati huo baada ya kumsindikiza Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji aliyekuwa na ziara ya kikazi nchini, wakiwa uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere
 Mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, akiteta na msaidizi wake january Makamba, hapa wakiwa katika kijiji cha Sapiwe kwenye kampeni huko usukumani
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Abdallah Msika, akisoma tangazo la tahadhali ya ukimwi
 Mpigapicha Athuman hamis na vicky Kamata, wakisikiliza hotuba za mgombea wa ccm
 Mgombea wa CCm, Jakaya Kikwete, akizungumza na mwanaccm, Maryciana Ngwagu wa kijiji cha Inolamagembe, wilaya ya magu sasa mkao wa Simiyu na nyuma yake ni mbuge wa huko Dk. Raphael Chegeni
 Unazikumbuka helfu hizi tatu katika kampeni za wakati huo hapa wakitoka Geita kuelekea Mwanza
 Athuman Hamis na Adam Gile wakiwajibika
 Kikwetw, akisalimiana na mwandishi nguli, wa michezo nchini na mmilikiwa gazeti la Mzawa lenye makazi yake huko Mwanza, James Nhende baada ya kuwasili uwanja wa kirumba Mwanza
 Akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Kirumba
 Wanamuziki Ntuyabaliwe, akiburudisha uwanjani hapo
 Uwanja wa CCM Kirumba unavyoonekana baada ya kupigwa picha kwa juu


 Wapigapicha  wakiwa na marubani na wasaidizi wao toka kushoto , Deus Mhagale,Adam Gille na Athuman Hamis
 Mgombea wa CCM, akienda kuwapa pole wafiwa wa mgombea Mwenza wa Urais chama cha Demokrasia na Maendelea na badae kampeni zilizsimamishwa kwa muda wa siku 90
 Wafanyakazi wa mwananchi wakiwa kwenye bonanza la family Day


 Cholaa, wakiingia ukumbini wakiigiza kama wafungwa na bendi yao ya twanga pepeta katika uzinduzi wa nyimbo zao


 Ali Choki akiingia na Kijiko ukumbini
 Wakifunguliwa pingu chini ya usimamizi wa Ali Choki
 Mbunge Amina Chifupa, alikufa hata kampeni yake ya kupambana na dawa za kulevya haijakolea
Floriani Pango na Jumanne Mkandu Jojo Jumanne waakiwa katika ukumbi wa Mango Gardeni
 Mgombea wa CCm, akizungumza na mtoto wake baada ya kumalizika hafla ya kuchangiwa kampeni zake zilizofanyika Bagamoyo

 Wagombea wa CCm, wakitoka kuchukua fomu kwa ajili ya kujaza waombe kugombea urais, wakiwapungia mikono mashabiki wao
 Marehemu Samuel Sitta na kijana wake Mbunbe wa Kigoma Vijijini wakati huo Zitto Kabwe
Kiajana huyu wakati akijifunza kupiga picha akiwachekesha wenzake ni Edwin Mjwahuzi


            Ni madhubuti?
Waziri Mkuu  Frederick Sumaye (wa pili toka kulia), akiangalia tank la kuhifadhia maji la lita 5000 mara baada ya kufungua warsha ya siku tatu ya Baraza la Taifa la Ujenzi. Warsha hiyo inafanyika Karimjee jijini Dar es Salaam, wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi John Magufuli sasa Rais na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Aquasan Tanzania limited ya Dar es Salaam, Amjad Khan

Mgombea Ubunge jimbo la Ubungo na wagombea wenzake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika (kuchoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uboreshaji wa maisha ya wakazi wa majimbo yao pindi  watakapochanguliwa. Mazungumzo hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam jana, wengine toka kushoto ni  Husseni Yahaya jimbo la Kinondoni na Deo Mushi jimbo la Kawe. 
 Siku waliyokabidhiana madaraka, Sumaye na Lowassa, sasa wapo Chadema
 Wake wa viongozi wa CCM kutoka kushoto, mama karume, Mama Mkapa, Mama Kikwete na Mama Shein
Wafanyakazi wa mwananchi Communications, wakicheza muziki wa wanaummeee, mapanga shaaa

Comments

Popular posts from this blog

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.