DAWASA NA NEEMA YA MAJI KWA WAKAZI WA DAR YAWADIA
Mafundi wakiendelea na kazi ya kulaza mabomba ya Maji eneo la Mbezi Beach
jijini Dar es salaam. Mabomba hayo ambayo sasa yamekamilika kwa urefu wa
kilometa 54.8 kati ya 55.9 yatatumika kusafirisha maji kutoka mtambo wa
kuzalisha maji wa Ruvu Chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
Ramani inayoonyesha kipande cha kilomita 1.2 eneo la Mbezi Tangi Bovu ukamilike usimikaji wa bomba hilo hilo kutoka Bagamoyo hadi Chuo Kikuu cha Ardha mjini Dar.
Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa DAWASA Romanus Mwangingo, akizungumza na wanahabri kuhusu kukamilika kwa utandikaji wa bomba hilo ambalo mpaka kukamilika kwake litakuwa limetumia kiasi cha Sh Bilioni 141. Dawasa wamefanya kazi kubwa ya usimamizi wa kazi hiyo amabayo iliingia ugumu baada ya wananchi zaidi ya 17 kufungua kesi kupinga kuhamishwa katika eneo linamopita bomba hilo wakidai mradi umewakuta. Hata hivyo baadhi yao walijiondoa katika kesi hiyo na wale waliobaki sheria ilichukua mkodo wake na Dawasa kuibuka kidedea mungu awape nini Dawasa sasa wakazi wa Dar watalajie kuogelea kwenye maji hayo. kazi kwao kulipa bili.
Afisa habari wa DAWASA, Meck Mdaku, akiwa katika eneo la mradi huo leo
Mwangingo, akizungumza na Meneja habari wa DAWASA, Nelly Msuya (kushoto), katika eneo la mradi huo
Mafundi wakianza kufukia bomba hilo baada ya kulisimika chini
Meneja wa kituo cha utandikaji bomba hilo wa Kampuni ya Gauff Consultants Thorsten Seits (kulia), akizungumza na wanahabari katika eneo hilo leo. na Kulia ni Meneja Mradi wa Kampuni hiyo Mhandisi Eric Omuruli
Akiwafafanulia jambo wanahabari

Huduma ya
Usambazaji wa Maji Safi katika jiji la Dar es salaam inatarajiwa kuimarika kwa
kuwafikia wananchi wengi zaidi mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu kufuatia
kukamilika kwa kilometa 54.8 za mradi wa Ujenzi wa Bomba kubwa la kusambazia Maji
kutoka chanzo cha Maji cha Ruvu Chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
Mradi huo unajengwa
na Kampuni ya JBG Gauff Ingenieure kwa gharama ya shilingi Bilioni 141 ambazo
zimetolewa na Serikali ya Tanzania na una jumla ya urefu wa kilometa 55.9.
Akizungumzia mradi
huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Usimamizi na Ufundi wa DAWASA,
Romanus Mwang’ingo(kulia pichani) amesema kuwa mpaka sasa ujenzi wa bomba hilo kuelekea
matangi ya kuhifadhia maji ya Chuo Kikuu cha Ardhi umefika eneo la Mbezi Beach
jijini Dar es salaam na huku ikiwa imebakiza kilometa 1.1.
Amesema ujenzi wa mradi huo kutoka mtambo wa Ruvu
Chini ndiyo utakuwa suluhisho la tatizo la maji katika jiji la Dar es Salaam na
maeneo ya mkoa wa Pwani na kuongeza kuwa utakapokamilika utazalisha lita milioni
270 kwa siku kutoka lita milioni 182 ambazo zote zitasukumwa kuja jijini Dar es
salaam.
Aidha, amesema kasi ya mkandarasi ya kulaza
bomba hilo inaridhisha licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali
zinazochelewesha kazi hiyo zikiwemo za ufinyu wa eneo linapojengwa bomba hilo
kuwezesha mitambo kufanya kazi vizuri katika eneo la mbezi Beach, mvua
zinazoendelea kunyesha ,changamoto ya makazi ya watu kuwa ndani ya mradi ambapo
kulikuwa na kesi 17 Mahakamani zikihusisha madai mbalimbali ya wananchi katika
maeneo hayo.
“Ni kweli zipo
changamoto zilizosababisha mradi kukawia kumalizika zikiwemo za wananchi
kufungua kesi 17 Mahakama ya Ardhi, hadi
sasa DAWASA tumeshinda kesi 14 ndiyo
maana tumepata haki ya kutumia njia hii kukamilisha upanuzi wa mradi” Amesema
Mwang’ingo.
Ameongeza kuwa lengo
la mradi huu nikuongeza uzalishaji wa maji na kuboresha huduma kwa wakazi wa
maeneo ya uwekezaji (EPZ) Bagamoyo, Chasimba, Buma, Zinga, Kerege na Mpiji mkoa
wa Pwani.
Maeneo mengine
yatakayonufaika na mradi huo kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni Bunju, Wazo,
Salasala, Madale na Kinzudi Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani,
Mikocheni, Mlalakua, Masaki, Sinza, Kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni,
Kigogo na Vingunguti.
Kwa upande wake
Meneja Mradi wa Kampuni inajenga bomba hilo nchini Muhandisi Eric Omuruli
akizungumzia mradi huo amesema kuwa yeye kama Meneja mradi atahakikisha
anashughulikia changamoto zilizopo ili kukamilisha kwa wakati.
Amesema kuwa licha
ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika eneo la mradi hasa eneo la Mbezi
Beach jijini Dar es salaam kampuni ya JBG Gauff Ingenieure inafanya kila
linalowezekana ili mradi huo ukamilike mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.
“Tumejipanga
kufanya kazi hadi usiku kupunguza muda,kazi iliyobaki ni ndogo, tunawahakikishia
DAWASA tutaimaliza kazi hii mwishoni mwa mwezi huu” Amesisitiza.
Afisa habari wa DAWASA, Meck Mdaku, akiwa katika eneo la mradi huo leo
Mwangingo, akizungumza na Meneja habari wa DAWASA, Nelly Msuya (kushoto), katika eneo la mradi huo
Mafundi wakianza kufukia bomba hilo baada ya kulisimika chini
Meneja wa kituo cha utandikaji bomba hilo wa Kampuni ya Gauff Consultants Thorsten Seits (kulia), akizungumza na wanahabari katika eneo hilo leo. na Kulia ni Meneja Mradi wa Kampuni hiyo Mhandisi Eric Omuruli
Akiwafafanulia jambo wanahabari
The best Of Eric Omuruli
ReplyDelete