GUNINITA AMSHITAKI MAKONDA

Kada na Kiongozi wa siku nyingi wa Chamam cha Mapinduzi (CCM), John John Guninitam, akiwa ameambatana na wakili wake wakiingia katika chumba cha mikutano katika ofisi za Idara ya Habari Maelezo leo kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu yeye na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Singida Mghana Msindai kumshitaki aliyekuwa mhamasishaji wa Chipukizi wa umoja wa chama hicho ambaye hivi sasa ni mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kwa kile alichodai kwamba kabla ya kuteuliwa na Rais aliwatukana bila sababu za msingi, istoshe alisema kwamba hivi sasa ccm kimekuwa kimbilio la wahuni wanaodiliki kutukana wakubwa hata waliowatangulia hata kwenye kazi wanaogawiwa sasa, kimekuwa chama cha wasaka tonge ambao hawajawahi hata kuchaguliwa wao ni kuteuliwa tu. Pia amewashutumu washauli wa rais akaisema kwamba hawamshauli vizuri kwani angekuwa yeye angetengua uteuzi wa Makonda, CCM na Serikali ni kama Jeshini, wanaheshimiana kwa vyeo na usinia, haiwezekani itokee siku koplo amke asubuhi na kumtukana kapteni au kampeni kumtukana Kanari hapo itakuwa hakuna jeshi bali ni maasi tu. alaisema Guninita aambaye miaka ya 90 yeye na Sukwa saaid Sukwa walikuwa vinara wa umoja wa Vijana wa Chama hicho.

Haijulikana hawa akina Makonda, wametokea wapi wasioifahamu hata histolia ya chama hicho na umoja huo, anacholalamika Kada huyo iweje hata viongozi wa umoja huo wa sasa mwenyekiti na katibu wake wakae kimya hata kumuonya tu. kama alitumwa watakutana huko mahakamani, amewaomba Massheikh, mapadri na wachungaji wamuombee amshinde makonda ili amfunge ili iwe fundisho kwaq wale wengine wenye tabia za hovyo hovyo kama za huyo Makonda 

 wanahabari wakimsikiliza kwa makini



Guninita na wakili wake Benjamin Mwakangamba


























































Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.