WAZIRI NYALANDU ATANGAZA KUWANIA URAIS WA TZ

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo (Picha na Bashir Nkoromo theNkoromo Blog)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu akisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo
 Mwimbaji wa muziki wa Injili, Frola Nkone akiimba kutumbuiza wakati wa mkutano huo
Mwanamuziki wa muizki wa Injili, Rose Mhando akiimba kutumbuiza wananchi katika mkutano huo wa Nyalandu
Wasanii wa kikundi cha Makomandoo cha mjini Singida wakitumuiza wakati wa mkutano huo
Wadau wakifurahia burudani wakati wa mkutano huo wa Nyalandu
 Steve Nyerere ambaye ni Msanii wa CCM, akizungumza kabla ya kumwaga vimbwanga vyake vya kuingiza sauti za viongozi mbalimbali wakati wa mkutano huo wa Nyalandu.

Nyalandu na Mkewe Faraja Kota wakiingia kwenye Kanisa la KKKT  Usharika wa Ilongelo kwa ajili ya ibada maalum. Pamona nao ni watoto wao Sera na Christopher kabla ya kwenda Uwanjani kutangaza azma yake ya kuwania Urais 2015
Nyalandu na Faraja Kota wakiwa na watoto wao Sera na Christopher katika kanisa hilo 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro  Nyalandu akitoa neno la shukrani baada ya ibada maalum katika katisa la KKKT Usharika wa Ilongelo jimboni humo leo
Waziri Nyalandu akiwa na watoto wake wakati wa ibada maalum iliyofanyilka leo katika Kanisa la KKKT Usharika wa Ilongelo Jimbo la Singida Kaskazini
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akitoa sadaka wakati wa ibada maalum iliyofanyika leo katika Kanisa la KKKT Usharika wa Ilongelo jimboni humo
Mke wa NYalandu, Faraja Kota akipita baada ya kutoa sadaka kwenye kanisa hilo la KKKT Usharika wa Ilongelo
Mwimbaji wa nyimbo za Injili lkatika Kanisa la KKKT Usharika wa Ilongelo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akizungumza na viongozi wa shule ya Kiislam ambayo huhudumia watoto wa dini zote katika kata ya Ilongelo, shule hiyo ina watoto 74.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akisalimia waumini kwenye Kanisa la FPCT  katika jimbo la Ilongelo alipofika kwa ajili ya ibada maalum
Waumini wakiwa katika kanisa la FPCT wakati wa ibada maalum aliyohudhuria Nyalandu leo
Nyalandu na Mkewe wakitoka katika Kanisa la FPCT baada ya kuhudhuria ibada maalum leo asubuhi.



Nyalandu atangaza kugombea urais
*Asema vijana wanakuja na maono mapya
*Amwaga msaada wa Sh mil 30 makanisani
*Asema kazi za wagombea zipimwe kwa moto

MBIO za urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),zimechukua sura mpya baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu kutangaza rasmi nia ya kugombea urais mwaka 2015.

Akizungumza katika mkutano wa kuwashukuru wapiga kura wake kwenye uwanja wa michezo wa Shule ya Msingi Ilongero Wilaya ya Singida Vijijini jana, Waziri Nyalandu alisema muda wa Tanzania kupata maono mapya umefika.
“Muda wa Tanzania kupata maono mapya umefika,nitachukua hatua ya kuelekea Dodoma kuchukua fomu muda ukifika, maelfu ya watu watanisindikiza,wanawake,vijana,wanawake kutoka mikoa mbalimbali.
“Naita zama mpya siku ambayo ndoto yangu itakamilika,Mungu atanyanua vyombo na kushangaza wakubwa.
“Najua tulikuwa wadogo kama Nazareti,lakini Ilongero imekuwa na mchango mkubwa ambao utakuwa si faida kwa wana Singida bali taifa zima la Tanzania,”alisema Waziri Nyalandu.
Alisema kila mtu ambaye ametangaza nia ya kuwania urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lazima kazi zake zipimwe kwa moto.
“Wale wote waliotangaza nia ndani ya chama chetu, kazi zao lazima zipimwe kwa moto na zianikwe hadharani ili mwisho wa siku CCM yenyewe itazipima,”alisema Waziri Nyalandu.
Alisema pindi Rais Jakaya Kikwete atapohitimisha utawala wake, lazima atakabidhi kijiti kwa kizazi kipya.
“Nina uhakika mheshimiwa Rais Kikwete akiondoka madarakani,lazima akabidhi kijiti kwa kizazi chenye fikra….zama za kusimama na kuchukua vijiti zimefika.
“Mwaka mwaka 2015,sisi ndani ya CCM tunatarajia utakuwa mwaka wa mabadiliko na fikra mpya.
“Tuna wajibu wa kubadili fikra zetu,watu wasimamie Tanzania kuchukua hatua, licha ya ukweli kwamba CCM tuna utaratibu na itikadi zetu,tumeondoa zuio kwa vijana wasiwe waoga…tumejipanga kuwashangaza wengi,”alisema Waziri Nyalandu.

WAPINZANI
Alisema muda wa kuwashangaza wengi unaanzia kwa vyama vya upinzani, zikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa
“Katika safari ya miaka 15,Mungu ametusaidia kusonga mbele, safari moja huanzisha nyingine,nawaomba tusonge tena kwa hatua nyingine,mlianzisha safari yangu ya kisiasa nilikuwa kama mzabibu uliotoa matunda, mkaniita ‘Mwanyengu’ maana yake mtoto wa tai la kuishangaza dunia. Safari hii imekuwa ya milima na mabonde kwa pamoja tumeweza,Mungu ameona,Kikwete ameona sawasawa.
“Nikitazama naona nchi hii inahitaji kubadilika kama nyingine zilizopiga hatua,Rais Kikwete amesimama kama jemedali,shujaa,mpambanaji hapa alipofika lazima tupapongezee,”alisema Waziri Nyalandu.
Alisema anatambua atapitia kwenye ushindani mkubwa ndani ya chama ambao utatoa mtu mmoja wa kupeperusha bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Nawambia wale wote wanaoogopa kushindanishwa ni waoga,siku,saa,mwezi na hata mwaka utakapofika chini ya Kikwete,wachukue fomu na kupeleka kazi zao ili zipimwe,”alisema Waziri Nyalandu.

VIONGOZI WAZEE
Alisema viongozi wastaafu waliotawala taifa hili wanapaswa kupewa heshima zote.
“Tunatambua mchango wa wazee wetu walioutoa,wana haki ya kuheshimiwa,lakini zamu ya vijana imefika.
“Vijana tunataka taifa litakaloleta siku njema,ni wajibu wetu tuwatunze ndiyo maana kupitia kwao maisha yetu yamebadilika,”alisema.
Alisema bado anawapenda mno wananchi wa jimbo lake, lakini safari walioinza mwaka 2000,lazima waikamilishe.
“Nalipenda jimbo langu,wapiga kura wangu,lakini tuungane kukamilisha safari hii tuliyoianza miaka 15 iliyopita,”alisema Waziri Nyalandu.

ATOA MAMILIONI
Baada ya kuwasili katika kijiji cha Ilongero, Nyalandu alikwenda moja kwa moja katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika wa Ilongero ambako alishiriki misa na kuchangia Sh milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa.
Katika misa hiyo, alipewa nafasi ya kuzungumza na kusema eneo hilo ni la ushindi kwake.
Pia alitembelea Kanisa la FPTC-Tanzania ambako nako alitoa msaada wa Sh milioni 10 na kiasi kama hicho alitoa kwenye Msikiti kwenye Ijumaa.
Katika mkutano huo, Nyalandu aliambatana na mke wake Faraja Kota,watoto wake Christopher na Serafine na wazazi wake.
Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.