TUME YA MAWASILIANO NCHINI TANZANIA YAWAANDALIA SEMINA WAMILIKI WA BLOG
Afisa Habari wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mabel Masasi, akizungumza kabla ya kuwakalibisha viongo wa Mamlaka ya Mawasilano kuongea na Wamiliki wa Blog nchini warsha hiyo ya siku moja ilifanyika jijini Dar es Salaam leo . Warsha hiyo ilihusu kuelemisha wasiokuwa na ujuzi wa uandishi wa habari kwenda shule kujiendelea na mambo wanayoyaweka katika blog zao. pia zizingatie utaifa kwanza na uzingatie maadili ya kitanzania. hiyo yote kujiepusha na kushtakiwa huku tuendako
Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka hiyo Habby Gunze, Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Profesa John Nkhoma na Mwakilishi kutoka Idara ya habari Maelezo Mr Msigwa.
Maofisa wa Tume ya Mawasiliano wakimsikiliza mkurugenzi alipokuwa akifungua warsha hiyo
Waalikwa wakimsikiliza mkurugenzi alipokuwa akifunguwa warsha hiyo
Habby Gunze, akitoa mada yake
Mkurugenzi Profesa John Nkhoma, akifungua warsha hiyo ya siku moja, waliomzunguka ni wanablog na waandishi wa habari, unaweza kujionea baadhi ya wanablog wanatumia simu kuchukua tukio
Na Oliver
Oswald, Dar es Salaam
MAMLAKA ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema haina mpango wa kuwaumiza au kuwawekea
vikwazo vya kuandika na kuripoti taarifa za uchaguzi waandishi wa habari, bali
itaendelea kuwasisitiza kuzingatia maadili na ukomo wa uandishi.
Kauli hiyo
ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John
Nkoma katika mkutano na wamiliki wa mitandao ya kijamii nchini (Blogger’s)
kuhusu namna ya kuripoti habari kuelekea uchaguzi mkuu ujao hapo mwakani.
Alisema dhumuni
la kukutana na wamiliki hao ni kuendelea kuwakumbusha kuzingatia maadili ya
uandishi kabla ya kutangaza au kuripoti taarifa zao katika mitandao.
“Unajua
kipindi cha uchaguzi mambo mengi yanajitokeza na kila mwandishi hususani wana
blogg huwa katika changamoto kubwa ya kuhakikisha anapata taarifa mpya ili
kuwavuta wasomaji ukizingatia mawasiliano ya habari kwa njia ya mitandao
imezidi kukua kila siku.
“Kutokana na
hilo TCRA tumeona tunakila sababu ya kukutana na wenzetu ili kuwapa elimu ya
kuandika habari zao katika kipindi hicho kwa kuzingatia ukweli halisi wa habari
anayo iripoti na ukomo wa kiuandishi,”alisema Nkoma.
Wakati
huohuo Nkoma aliwasisitiza wamiliki hao kuzingatia suala la ulinganifu wa
habari kabla haijasambaa kwenye mitandao ili kuepusha manung’uniko kutoka kwa
wahusika.
“Uhuru wa
uandishi utaendelea kuzingatiwa ila tahadhari iliyopo ni kukumbuka kulinganisha
taarifa zenu kabla hamjazisambaza kwabi vinginevyo mnaweza kuibua malalamiko
kwa wahusika,”alisema Nkoma.
Wakizungumzia
kuhusu suala la ukomo wa uandishi na ulinganifu wa habari, baadhi ya wamiliki
wa blogg waliohudhuria katika mkutano huo wamesema jambo hilo ni muhimu kwa
kila mwandishi kulitambua na kulifanyia kazi ili kuepuka madhara ya kushtakiwa.
Dues Mhagale
ni mmiliki wa Mhagalle Blogg, alisema ipo haja kwa wamiliki wa blog wasiokuwa
na taaluma ya habari kujifunza ili kutambua na kuelewa kwa umakini maadili ya
uandishi, kwani kutampa mwongozo katika kutoa taarifa sahihi zisizo na
upendeleo.
Alisema sambamba
na hilo pia kila mmiliki wa blog anapaswa kueleza chanzo cha habari anayoitoa
ili kuepuka madhara ya kujumuishwa katika malalamiko.
“Baadhi ya
wanablogg wamekuwa na kawaida ya kuchukua habari kutoka blog nyingine bila
kueleza taarifa hizo amezitoa kutoka kwa nani, hawajui mwisho wa siku anaweza
kujikuta matatizoni bila kuwa na hatia,”alisema Mhagalle.
Mwisho.
Comments
Post a Comment