WAFADHILI WARIDHISHWA NA MRADI NA MAENDELEO YA MRADI WA MAJARIBIO WA KUTUMIA TEKNOLOJIA KWA WATOTO WALIO NA FUSA NDOGO
Katibui
Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kulia akiwaonyesha mmoja ya
sehemu zinazotunzwa tablets ambazo zinatumiwa kufundishia wanafunzi
akiwa na wafadhili wa mradi huo
Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kushoto akiwa na wafadhili wa mradi huo wakiangalia namna wanafunzi wanavyojifunza kutumia teknolojia ya Tablets
Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kulia akiteta jambo na wafadhili wa mradi huo |
Wadau wa mradi wa miaka mitano wenye lengo la kutumia teknolojia ya kisasa kuwawezesha
watoto waliona fursa ndogo ya kupata elimu katika umri wa miaka tisa
hadi kumi na mmoja, kujifunza wenyewe stadi za msingi za Kusoma,
Kuandika na Kuhesabu (KKK) wameeleza kuridhishwa kwao na maendeleo ya
majaribio hayo.
Wadau
ambao walikuwa na ziara ya siku moja kutembelea vijiji mbalimbali vya
nradi huo katika wilaya za Muheza na Pangani wadau aho ambao walikuwa
pamoja na Mwakilishi wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Tanzania,
Michael Dunford, Mkurugenzi wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya Kanda ya Afrika Mashariki, Anne
Ndong-Jatta wakiambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi
Zena Said.
Wakitoa
maoni wakati wakipewa maelezo walisema ni wazi mradi umeanza kuonyesha
uwezo wa teknolojia kuamsha ari ya kujifunza na kusoma.
Taarufa
za awali za mradi na ushuhuda tuliouona inaonyesha kuwa mpango huu wa
kiteknolojia una uwezo wa kuwasha mwamko wa elimu miongoni mwa watoto na
wazazi na unapaswa kutiliwa maanani,” alieleza Mhandisi Said wakat wa ziara hiyo.
Pia
Mhandisi Said alisema kuwa ni wazi pia kuwa kuwatambulisha wananchi
katika teknolojia ya kisasa wakiwa na umtri mdogo kunawahakikishia
watoto hao kuwa hawawezi kunyanyaswa hapo baadaye wakiwa wakubwa.
Naye
Ndong-Jatta alisema kuwa mradi unaonyesha haja ya kuangalia uwezekano
wa kupunguza tatizo la kutojua kusoma na kuandika kwa wazazi kama njia
mojawapo ya kuamsha mwamko wa elimu miongoni mwao na kuwawezesha
kuwasukuma watoto kwenda shule.
Zaidi ya watoto 2,500 kutoka katika vituo 142 vilvyopo katika wilaya za Handeni, Korogwe, Lushoto, Mkinga, Muheza na Pangani walipewa tablet mpya aina ya Google Pixel C,
zilizotolewa kwa hisani ya Google. Tableti hizo zimewekewa mifumo ya
elimu kutoka kwa washindi watano wa mwisho wa Global Learning XPRIZE.
Washindi hawa walichaguliwa kutoka katika timu 198 napaneli ya majaji 11
wa kujitegemea na walio wataalamu na kutangazwa mwezi September, 2017
wakati wa wiki ya BarazaKuu la Umoja wa Mataifa
Mradi
huo wa miaka mitano uliotokana na mashindano duniani yenye thamani ya
Dola za Mareka ni milioni 15. Mradihuu wa dunia unatoa changamoto kwa
timu za wa bunifu kubuni na kuandaa zana za kusaidia kuondoa ujinga
duniani na kuwasaidia watoto ambao hawajapata fursa ya kwenda shule
kujifunza wakiwa nyumbani (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga
Raha)
HALMASHAURI YA MJI GEITA YAPITISHA BILIONI 44.9 MWAKA WA FEDHA 2018/19
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly Akizungumza
wakati wa kikao cha kupitisha Bajeti ya fedha ya mwaka 2018/19.
Baadhi ya watumishi na wakuu wa idara wakiwa kwenye Kikao cha kupitisha Bajeti ya fedha ya mwaka 2018/19.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Mji Geita Mheshimiwa Leonard Kiganga
Bugomola,akizungumza wakati wa kikao cha kupitisha bajeti ya mwaka wa
fedha 2018/19.
Meza kuu ikiwa na viongozi mbali mbali wa Serikali na chama cha mapinduzi.
Na,Consolata Evarist,Geita
Baraza
la madiwani wa halmashauri ya mji wa Geita,Wilayani Halmashauri ya Mji
Geita limepitisha makadirio ya bajeti ya matumizi ya ya mwaka wa fedha
2018/2019 kiasi cha shilingi Bilioni 44,983,764,197.00 katika shughuli
mbalimbali za Halmashauri. Kati ya Fedha hizo Jumla ya Tsh
15,585,248,344.00 ni kwa ajili ya shughuli za Maendeleo ikiwa ni Mapato
ya Ndani, Ruzuku ya Serikali na Wahisani mbalimbali. Tshs.
4,765,976,688.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikiwa ni Ruzuku kutoka
Serikali kuu na Mapato ya ndani na Tshs. 24,632, 539,165.00 kwa ajili
ya mishahara.
Aidha
Halmashauri imekisia kukusanya Jumla ya Tsh 5,114,157,735.00 toka vyanzo
vya ndani ambayo fedha hii imejumuishwa katika jumla ya Bajeti ya mwaka
2018/2019. Jumla ya Tsh. 3,030,016,641.00 sawa na 60% zimetengwa kwa
ajili ya Miradi ya Maendeleo.
Akiongeza
katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Geita kwenye kikoa cha kupitisha
bajeti ya Mwaka wa fedha 2018/2019,Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya
mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinali alisema Bajeti hyo imezingatia
vipaumbele vilivyoainishwa kwenye Mwongozo wa kuandaa Bajeti uliotolewa
na Wizara ya Fedha Mwezi, Novemba 2016, Malengo ya Maendeleo Endelevu
(SDGs 2030); Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020, Mpango wa Pili
wa miaka Mitano (FDYPII) 2016/17-2020/21 na Lengo likiwa ni kufikia
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2030.
“Mpango
na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019,kwenye halmashauri hiyo kuwa
imejielekeza katika kufikia vipaumbele vyenye shabaha na malengo
yafuatayo Kuendelea kuboresha na kuimarisha mfumo wa makusanyo ya mapato
ya ndani ili kuongeza mapato ya Halmashauri. Kuboresha Sekta za huduma
za jamii, hususan, Elimu, Afya, Maji, Barabara, Mifugo, Uvuvi, Kilimo,
Misitu, Maendeleo ya Jamii, Ushirika.Kusaidi Sera ya Taifa kufikia
Uchumi wa kati wa uendelezaji wa viwanda.Kuimarisha Utawala bora”Alisema
Modest
Aidha
ameongeza kuwa Halmashauri inategemea kukusanya mapato yake kutoka
kwenye vyanzo mbalimbali kama kodi ya huduma( service levy) kutoka
kampuni ya Mgodi wa Dhahabu Geita na Kampuni nyingine zinazofanya kazi
na Mgodi huo, kodi ya nyumba za kulala wageni, Leseni za biashara,faini
mbalimbali, upigaji chapa mifugo na ushuru wa mifugo, ushuru wa mazao
mbalimbali na matunda.
“Katika
Bajeti ya mwaka 2018/2019. Jumla ya Shilingi 15,585,248,344 zimetengwa
kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo, Kiasi cha shilingi 24,632,539,165 kwa
ajili ya mishahara ya watumishi na Shilingi 4,765,976,688 kwa ajili ya
matumizi mengineyo”. Aliongeza Mhandisi Aporinaly
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Mji Geita Mheshimiwa Leonard Kiganga Bugomola alisema
kwa mwaka wa fedha uliopita Halmashauri ilipanga kukusanya zaidi ya
Shilingi Bilioni 5, ambapo hadi kufikia mwezi Disemba 2017 Halmashauri
imeweza kukusanya kiasi cha Shilingi 2,868,353,850.15 sawa na asilimia
52.
Mh.
Bugomola ameongeza kuwa kutokana na mafanikio ya ukusanyaji uliofikia
nusu ya makadirio ana imani kuwa mpaka kukamilisha mwaka wa fedha
2017/2018 mwezi Juni mwaka huu, Halmashauri itakuwa imefikisha lengo la
makusanyo. Aidha makusanyo hayo yanatoa mwanga wa mafanikio katika
bajeti iliyopitishwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya hiyo,Mwl Herman Kapufi amewasisitiza wajumbe
kuwa na ukusanyaji mzuri wa mapato hili kuweza kutekeleza bajeti kwa
uzuri zaidi.
Katika
Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019, Halmashauri ya Mji Geita
imejielekeza katika kufikia vipaumbele vyenye shabaha na malengo ambayo
ni Kuendelea kuboresha na kuimarisha mfumo wa makusanyo ya mapato ya
ndani ili kuongeza mapato ya Halmashauri, Kuboresha Sekta za huduma za
jamii, hususan, Elimu, Afya, Maji, Barabara, Mifugo, Uvuvi, Kilimo,
Misitu, Maendeleo ya Jamii, Ushirika,
Kusaidia Sera ya Taifa kufikia Uchumi wa kati wa uendelezaji wa viwanda na Kuimarisha Utawala bora.
TGNP Mtandao wakutanisha madiwani 20 kujadili kushirikiana
Zaidi
ya madiwani 20, kutoka mikoa mitano na wilaya Nane wamekutana jijini
Dar Es Salaam, kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana
na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao.
Madiwani
hao ni kutoka Halmashauri za wilaya za Kishapu (Shinyanga), Tarime
(Mara), Mbeya (Mbeya), Morogoro Vijijini (Morogoro) na manispaa za
Ilala, Kinondoni na Ubungo (Dar es salaam).
Madiwani
hao ambao walikutana katika ofisi za TGNP Mtandao, zilizopo Mabibo Dar
Es Salaam, pia walipata nafasi ya kutembelea Kipunguni na kujionea mradi
unaotekelezwa katika eneo hilo.
Pamoja
na kujifunza masuala mbalimbali, Madiwani hao walipata fursa ya
kushirikisha masuala ya kijinsia ambayo bajeti za Halmashauri zao
zimezingatia na jinsi walivyofanikiwa kutenga rasilimali za kuhakikisha
bajeti zao zinakidhi mahitaji ya kijinsia.
Wakiwa
kata ya Kipunguni iliyopo manispaa ya Ilala madiwani hao walikutana na
Diwani wa Kata hiyo na kujifunza jinsi ambavyo wananchi waliopo katika
Kituo cha Taarifa na Maarifa walivyofanikiwa kuleta maendeleo kwa
kushirikiana na viongozi ikiwepo kupambana na ukatili wa kijinsia hasa
ukeketaji.Eneo
hilo maarufu kwa wakazi wa kutoka mikoa ya kaskazini ambako yapo
makabila yanayofanya ukeketaji nalo limekumbwa na tatizo hilo.
Aidha
katika ziara hiyo, waheshimiwa madiwani walipata nafasi ya kujifunza,
faida za mabunge ya jamii, na kujifunza miradi ya maendeleo ya kuwezesha
wananchi kiuchumi ambayo inatekelezwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana
na wananchi wa Kipunguni.
Katika
mabadilishano ya uelewa mmoja wa wajumbe ambaye ni Diwani wa Ijombe
wilayani Mbeya, Stimar Hepa John alisema kwamba wakati umefika kwa
wananchi wengi kutambua shughuli za TGNP Mtandao.
Alisema
awali alikuwa akidhani kwamba asasi hiyo ina mlengo wa kisiasa kiasi
cha kushindwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwao lakini baada ya elimu
hii amebadili uelekeo na kuitaka taasisi hiyo kupeleka elimu Tanzania
nzima.
Alisema,
"Anaona kwamba TGNP ina jukumu kubwa nchini Tanzania na hivyo
inastahili kuwa kila mahali kuwasaidia watanzania kujiimarisha katika
nyanja zote."Diwani
huyo wa Ijombe ambaye pia ni Mkuu wa shule ya sekondari Igawii alisema
pamoja na kubadili mwelekeo aliwataka wabunge kuona kwamba wanapoandaa
miradi hawaandai mbunge mpya bali kusaidia wananchi kujiinua kiuchumi.
Katika mkutano huo walitoa maazimio kadhaa ya kufanyiwa kazi katika halmashauri.Miongoni
mwa maazimio hayo ni namna ya kusimamia Mfuko wa Maendeleo wa wanawake
kuhusu ile asilimia 5 na kutekeleza dhana ya viwanda.
Kwa
mujibu wa Ofisa Programu uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deo Temba mambo
mengine waliyokubaliana ni kushawishi na kufuatilia ongezeko kila
zahanati na vifaa vya kujifungulia na kuhimiza uwekaji wa mikakati ya
kupambana na ukatili wa jinsia na kuunda kamati za ulinzi za mtoto.
Pia
imeelezwa haja ya TGNP Mtandao kuendelea kutoa elimu kwa kusaidiwa na
mabaraza ya halmashauri kuhusu rasilimali fedha na kufuatilia uwekezaji
katika ujenzi wa hosteli kupunguza umbali wa watoto wa kike kutembea
kufuata shule.Mambo
mengine ni kuona kwamba uandaazi wa bajeti unaanzia ngazi ya kijiji au
mtaa badala ya kata na kukosekana kwa sauti za wananchi katika bajeti.
TGNP
Mtandao ni asasi ya kiraia inayo fanya kazi na wanajamii kwa kipindi cha
miaka 25 sasa, kwa kipindi chote hicho kimeshirikiana na taasisi za
serikali, Wizara, Halmashauri na Kamati za Bunge za kisekta kwa ajili ya
majadiliano, mashauriano na mafunzo ya namna ya kuboresha huduma za
jamii kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Ofisa
Programu uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deo Temba akifafanua jambo wakati
akiendesha mjadala kwa Madiwani 20 kutoka mikoa 5 na wilaya 8
walioshiriki mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya
kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao
uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Diwani
wa Kata ya Songwa wilayani Kishapu, Shinyanga, Ngoromole Abdul
akibadilishana uzoefu na madiwani wenzake wakati wa mkutano wa
kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi
katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na
kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Diwani
wa Ijombe wilayani Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa shule ya sekondari
Igawii, Stimar Hepa John akichangia kwenye mjadala wakati wa mkutano wa
kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi
katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na
kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.Diwani
wa Kata ya Mshewe ya Wilaya ya Mbeya vijijini, mkoani Mbeya, Esther
Mbega akishiriki kwenye mjadala wakati wa mkutano wa kubadilishana
uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta
maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Diwani
wa Kata ya Ukenyenge ya wilaya Kishapu mkoani Shinyanga, Anderson
Mandia akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na
kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo
katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi
wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Pichani
juu na chini ni washiriki wakiendelea kujadiliana wakati wa kipindi cha
maswali na majibu katika mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza
jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata
zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano
wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Sehemu
ya Madiwani 20 kutoka mikoa 5 na wilaya 8 walioshiriki mkutano wa
kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi
katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na
kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.
SERIKALI IMETENGA SHILINGI BILIONI 11.4 KUBORESHA WAKALA WA NDEGE ZAKE
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiongea
na wajumbe wa Menejimenti ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) (hawapo
pichani) wakati wa ziara yake kwenye taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Anayemsikiliza ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bwana Tito
Kasambala
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
Richard Mayongela (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) kwenye uwanja wa ndege wa
Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua Wakala wa
Ndege za Serikali
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akipanda
kukagua mojawapo ya ndege za Wakala wa Ndege za Serikali inayosafirisha
viongozi wa ngazi ya juu wa Serikali wakati wa ziara yake kwa Wakala
hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam
Mkaguzi
Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali Mhandisi Bernard Mayila akifafanua
jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta
Nditiye wakati akifanya ukaguzi ndani ya ndege mojawapo inayosafirisha
viongozi wa ngazi za juu wa Serikali wakati wa ziara yake alipotembelea
Wakala hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiteremka
baada ya kukagua mojawapo ya ndege za Wakala wa Ndege za Serikali
wakati wa ziara yake kwenye Wakala hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Dar es
Salaam
……………….
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kuboresha Wakala wa Ndege
za Serikali (TGFA) ambayo inasimamia na kuendesha ndege ambazo
zinasafirisha viongozi wa kitaifa wa Serikali
Hayo
yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa
ziara yake ya kikazi alipotembelea na kukagua utekelezaji wa majukumu ya
Wakala wa Ndege za Serikali ambayo inasimamia na kuendesha ndege ambazo
zinasafirisha viongozi wa kitaifa wa Serikali ambapo alizungumza na
Menejimenti na wafanyakazi na kuwaeleza kuwa Serikali imejipanga
kuboresha Wakala hiyo
Mhandisi
Nditiye alisema kuwa azma ya Serikali ya Awamo ya Tano inayosimamiwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
ni kuhakikisha kuwa Taasisi za Serikali zinafanya kazi zake kwa weledi
na uadilifu ili kufanikisha malengo ya Serikali ya kuwatumikia wananchi.
“Serikali inatambua umuhimu wa Wakala hii na ina imani kubwa nanyi
katika kuhakikisha kuwa mnafanya kazi zenu za kusafirisha viongozi kwa
usalama na kwa uhakika ili waweze kutimiza majukumu yao ya kuwatumikia
wananchi na tayari ina nia ya kuboresha taasisi hii”, amesema Mhandisi
Nditiye.
Naye
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TGFA Bwana Tito Kasambala amemueleza
Mhandisi Nditiye kuwa taasisi yake ina ndege nne ambazo zinatumika
kusafirisha viongozi wa kitaifa wa Serikali katika kutimiza majukumu yao
ya kuwatumikia watanzania na tayari Serikali imetenga shilingi bilioni
11.4 kwenye bajeti ya mwaka wa fedha wa 2017/18 kwa ajili ya shughuli
mbali mbali za Wakala ikiwemo matengenezo ya ndege, mafunzo kwa wanahewa
na ukarabati wa karakana.
Mhandisi
Nditiye amewaeleza wajumbe wa Menejimenti na wafanyakazi wa Wakala hiyo
kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wao na umuhimu wa
wahandisi wa ndege na marubani wa kupata nafasi ya kuendesha ndege na
kozi za mafunzo mbali mbali kuendana na taaluma zao ambapo tayari
makubaliano yamefanyika baina ya Wizara na Shirika la Ndege Tanzania
(ATCL) ya kuwapatia nafasi marubani wa ndege za Wakala wa Ndege za
Serikali nafasi ya kurusha ndege mara kwa mara ili kuendana na matakwa
ya taaluma zao.
Ameongeza
kuwa Serikali inashughulikia suala la miundo ya watumishi wa umma
ambapo Wakala wa Ndege za Serikali ni mojawapo ya taasisi ambayo muundo
wake unafanyiwa kazi ili kuweza kuzingatia taaluma, kada za watumishi na
maslahi yao. “Natumaini wote mnatambua na kuelewa kuwa kipindi cha hapo
nyuma kidogo utumishi wa umma uliingiwa na baadhi ya watu wachache
ambao walikuwa wanafanya ujanja ujanja na kuharibu utumishi wa umma
ambapo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli, Rais wetu, imelifanyia kazi jambo hili na ameunda bodi
maalumu ambayo inafanyia kazi suala la muundo, kada na maslahi ya
watumishi wa umma,” amesema Mhandisi Nditiye.
Aidha,
wafanyakazi wa Wakala wa Ndege za Serikali wamemuomba Mhandisi Nditiye
kuwasilisha ombi lao kwa Serikali la kuwaongezea mishahara yao kuendana
na hali ya soko la ajira ya marubani ilivyo nchini kwa sasa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
DC MATIRO AWARUDISHA KAZINI WATUMISHI WA AFYA WALIOTUMBULIWA ZIARA YA NAIBU WAZIRI MAVUNDE
Watumishi
wa afya 22 katika hospitali ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga
wamerudishwa kazini na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro mara
baada ya kutumbuliwa na uongozi wa hospitali hiyo kutokana na kutoa
malalamiko yao mbele Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Athony
Mavunde alipofanya ziara yake Februari 27,2018.
Watumishi
hao walifukuzwa kazi siku moja baada ya ziara ya Naibu Waziri huyo
kwenye hospitali hiyo ambayo aliifanya Februari 27 mwaka huu mara baada
ya kutoa malalamiko yao juu ya kunyanyaswa na hospitali hiyo ambapo
kesho yake wale waliojifanya wazungumzaji 'kiherehere' wakatimuliwa kazi
na kutolipwa stahiki zao zote.
Akiongea
Machi 1, 2018 na uongozi wa hospitalini hapo mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro alisema mara baada ya kupewa taarifa hizo juu
ya watumishi hao kuwa wametimuliwa kazi baada ya kusema ukweli kwenye
ziara ya Naibu Waziri huyo, jambo hilo limemkera na kuamua kufika kwenye
hospitali hiyo kuwarudisha kazini.
“Kuanzia sasa watumishi wote mliowafukuza kazi wanarudi kazini na
ninatoa siku 14 wawe wameshalipwa haki zao zote wanazodai, ikiwamo
malimbikizo ya mishahara, makato ya NSSF,TUGHE, pamoja na kulipwa
mishahara kiwango cha serikali, na msipofanya hivyo ndani ya siku hizo
tutawachukulia hatua,”alisema.
"Kwanza hospitali hii mmeidharau serikali kwa sababu haiwezekani
kiongozi mkubwa kama yule Naibu waziri anafanya ziara ya kusikiliza na
kutatua kero za watumishi, halafu ninyi kesho yake mnawafukuza kazi, huo
ni utovu wa nidhamu”,alisema Matiro.
Naye mmoja wa watumishi hao walifukuzwa kazi Elizabeth Zabron alisema
baada ya kutoa malalamiko yao juu ya kunyanyaswa kwenye mishahara na
madai mbalimbali, muda mfupi tu baada ya kuondoka Naibu Waziri huyo
wakaona majina ya watu 22 yakiwa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo
wakiitwa kesho kuonana na uongozi wa hospitali hiyo.
Alisema baada ya kwenda kuonana na uongozi huo wakajua tayari kilio chao
kimesikika cha kulipwa mishahara na madai yao, ambapo wakashangaa
wanaambiwa kuwa wamefukuzwa kazi na wanatakiwa kusaini barua hizo bila
ya kuzisoma, ndipo wakagoma na kuamua kwenda kushitaki kwa mkuu huyo wa
wilaya ili wapate haki zao.
Barua hizo kwa ndani zilikuwa zimeandikwa kuwa "unafukuzwa kazi na
hutakiwa kulipwa haki yako yoyote na kutakiwa kuondoka eneo la kazi mara
moja".
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt .Maganga Dohoi
alikiri kuwafukuza kazi watumishi hao na kudai kuwa bodi ya hospitali
hiyo ilikaa na kuagiza watumishi wote wasio na sifa ya kuwa na vyeti vya
kidato cha nne lakini wana taaluma ya uuguzi wafukuzwe kazi, ndipo naye
akafuata maagizo hayo.
Hata hivyo mmoja wa wajumbe wa Bodi ya hospitali hiyo Magezi Magedi
ambaye pia ni ofisa utumishi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga,
alikana kukifahamu kikao cha kufukuza watumishi hao , na kudai kama
suala la kufukuza kazi kuna taratibu zake zinatakiwa kufuatwa na siyo
kuwafukuza hovyo hovyo.
Alisema hospitali hiyo isitumie kivuli cha serikali kufukuza watumishi
hao ikiwa suala la vyeti vya darasa la Saba lilikuwa la watumishi tu wa
serikali.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na watumishi wa
afya katika hospitali ya Kolandoto waliotimuliwa kazi.-Picha na Marco
Maduhu - Shinyanga News blog & Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akionyesha masikitiko namna
walivyotendewa ndivyo sivyo watumishi hao wa afya katika hospitali ya
Kolandoto kwa kutimuliwa kazi kisa wametoa malalamiko yao mbele ya Naibu
waziri wa Kazi,Ajira na Vijana Anthony Mavunde.
Mmoja wa watumishi waliofukuzwa kazi Elizabeth Zabroni akielezea kisa cha kufukuzwa kazi
Emmanuel Makungu naye alidai wamekuwa wakilipwa mishahara lakini
hawapewi Salary Slip wala kusaini popote na kutokujua umeingia mshahara
wa mwezi gani na pia michango ya NSSF wamekuwa wakiambiwa imeingizwa
lakini wakifuatilia hakuna pesa yoyote iliyowekwa pamoja na fedha za
likizo kutopewa, na kubainisha kuwa walipotoa malalamiko yao mbele ya
Naibu Waziri wa Kazi,Ajira na Vijana Antony Mavunde iliwapate haki zao
wakaonekana kuwa kikwazo na kutimuliwa kazi.
Sara Mkem akionyesha kusikitishwa na uongozi wa hospitali hiyo kwa
kuwafukuza kazi kisa wametoa matatizo yao mbele ya Naibu Waziri huyo ili
yapate ufumbuzi, na kuonekana kuwa kero na kutimuliwa kazi, bila hata
ya kujali utu wao pamoja na kulazimishwa kusaini barua bila ya kuzisoma
na kudai uongozi huo una roho ya kinyama kwani huenda ina dhamira ya
kutaka arudi uraiani akauawe na watu wabaya kwa kumkata viungo vyake.
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt Maganga Dohoi akijitetea kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Baadhi ya watumishi waliofukuzwa kazi na uongozi wa hospitali ya
Kolandoto wakiwa kwenye kikao na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro na uongozi wa hospitali hiyo kutatua suala lao la kufukuzwa kazi
mara baada ya kutoa kilio chao kwa Naibu Waziri wa Kazi,Ajira na Vijana
Antony Mavunde juu ya manyanyaso wanaoyapata .
Watumishi wa afya waliofukuzwa kazi katika hospitali ya Kolandoto wakiwa
kwenye kikao cha kutatuliwa matatizo yao na mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro mara baada ya kumpelekea matatizo yaliyowakumba ya
kutimuliwa kazi kinyemela bila ya kufuata sheria za kazi.
Kikao kikiendelea.
Watumishi wa afya katika hospitali ya kolandoto waliofukuzwa kazi kenyemela wakiwa wameshika bango la kutaka haki yao
Ofisa utumishi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga,Magezi Magedi
ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya hospitali hiyo ya Kolandoto akikana
kukifahamu kikao cha kufukuza kazi watumishi hao na wala tangu
achaguliwe kuwa mjumbe wa bodi hiyo hajawahi kuitwa hata kikao kimoja
na kudai kama suala la kufukuza kazi watumishi hao kuna taratibu zake
zinatakiwa kufuatwa, na siyo kuwafukuza hovyo hovyo na kuwalazimisha
kusaini barua bila ya kuzisoma.
Ofisa kazi mkoa wa Shinyanga Revocatus Mabula alisema taratibu za
kuwafukuza kazi watumishi hao zilikiukwa ambapo hawakupewa notes na
walistahili kupewa haki zao zote ndani ya siku 14,kulipwa kiinua
mgongo,malimbikizo ya likizo zao zote pamoja na kusafirishwa mahali
walipotoka makwao na siyo kuambiwa tu wamefukuzwa kazi na hawatolipwa
pesa yoyote.
Katibu
wa Chama Cha Wafanyakazi TUGHE, Tabu Mambo alisema hawajahi kuona
mchango wowote wa watumishi hao waliofukuzwa kazi licha ya kuambiwa kuwa
wanalipiwa na kubainisha kuwa walipokuwa wakifika kuzungumza na
watumishi hao walikuwa wakikosa ushirikiano kutoka kwa viongozi wao, na
wale watumishi ambao walioonekana kuwa wanajua kuongea ndiyo kidogo
walikuwa wakitolewa michango hiyo.
Picha na Marco Maduhu - Shinyanga News blog & Malunde1 blog
Ziara ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mkoani Njombe.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akimsikiliza
mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka alipomtembelea
ofisini kwake kupata taarifa ya Viwanda na uwekezaji katika mkoa huo,
leo tarehe 1 Machi, 2018.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza
jambo na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bibi. Ruth Blasio Msafiri walipofika
ofisi za SIDO Mkoa wa Njombe kuona utendaji wake.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,. Charles Mwijage akikagua eneo
litakalojengwa majengo makubwa kwa ajili ya wajasiriamali na
wafanyabiashara wadogo, Mkoani Njombe leo tarehe 1 Machi, 2018.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, akimsikiliza
meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Njombe kuhusu utaratibu wanaotumia
katika kupima mizigo ya wakulima na wafanyabiashara mkoani Njombe.
Muonekano
wa Kiwanda cha kuchakata Chai cha Unilever kilichopo mkoani Njombe
ambacho kipo katika hatua za mwisho kukamilika kwa ujenzi wake.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akikagua uenzi
wa kiwanda cha Chai cha Unilever, Mkoani Njombe leo tarehe 1 Machi,
2018.
Wadau
na wafanyabiashara wa Mkoa wa Njombe waliokusanyika kumsikiliza Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Hayupo pichani)
na baadae kuuliza maswali kutokana na changamoto wanazokutana nazo na
kupatiwa majibu.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza
wakati wa mkutano na wafanyabiashara kujadili changamoto zianazowakabili
wafanyabiashara katika mkoa wa Njombe Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe
Mhe. Christopher Ole Sendeka na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe
Bibi. Ruth Blasio Msafiri.
TACAIDS KUANZA KAMPENI YA KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA AFYA ZAO-MABOKO
Mratibu
wa mtandao wa viongozi wa dini wanaoishi na virusi vya ukimwi
,(TANERELA),mchungaji Amin Sandewa pichani .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mkurugenzi
mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS ) ,Leonard
Maboko akizungumza jambo ,mjini Kibaha ,Mkoani Pwani ,katika mkutano
ulioandaliwa na tume hiyo ,kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za
ukimwi kwa asasi mwamvuli ya mwaka 2018/2019 .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
TUME
ya Taifa ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS), inatarajia kuanza kampeni za
kitaifa kuhamasisha wanaume kupima afya zao ,ili kujenga tabia ya
kujitokeza kujua afya zao kwani ni asilimia 45 pekee ya kundi hilo
walioaminika kuwa na VVU ndio waliopima kujua hali zao.
Aidha
imeeleza ,kati ya watu kumi wenye maambukizi mapya kwa mwaka ,vijana
wanne sawa na asilimia 40 ugundulika kupata maambukizi hayo.
Pamoja na hayo ,kati ya vijana kumi waliopata maambukizi mapya kila mwaka nane huwa vijana wa kike na wawili ni vijana wa kiume.Mkurugenzi
mtendaji wa TACAIDS ,Leonard Maboko aliyaeleza hayo mjini Kibaha
,Mkoani Pwani ,katika mkutano ulioandaliwa na tume hiyo ,kupitia mipango
ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi mwamvuli ya mwaka 2018/2019 .
Alisema
,kampeni hiyo itakuwa ya miezi sita na itakuwa endelevu hadi hapo
watakapohakikisha wanatokomeza ama kupunguza gonjwa hilo .Maboko
alisema ,wale watakaobainika kuwa na maambukizi mapya watatakiwa kuanza
tiba ya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARVs) mapema ili kuondoa
vifo vinavyotokana na virusi hivyo .
Alielezea
,wanaandaa kampeni hizo kutokana na takwimu za utafiti wa viashiria vya
ukimwi ya mwaka 2016/2017 inayoonyesha idadi ya watu wanaopima na
wanaogundulika kuambukizwa wanaoanza kutumia dawa ni wanawake kuliko
wanaume.
“Asilimia 45 ya wanaume ndio wanaoaminika kuwa wamepima na kujua hali zao ,hali ambayo inaonyesha ni kiwango cha chini “.“Simaanishi wenye ukimwi wote wameshapima kujitambua ,lakini inahitajika hamasa ili tufikie malengo”alisema Maboko.
Hata hivyo Maboko alisema ,maambukizi mapya ya ukimwi yanaongezeka zaidi kwa kundi la vijana hususan wa kike .“Hii
inaonyesha huko kipindi cha nyuma hakukuwa na hali hiyo hivyo haina
budi kundi hilo likatiliwa mkazo ,ili kupunguza ongezeko hilo ”
“Hali
ya maambukizi ya ukimwi Tanzania kwasasa ni asilimia 4.7 kutoka asilimia
5.1 ,hali inapungua lakini inatakiwa tuendelee kupambana na maambukizi
mapya ,na Tanzania bila ukimwi inawezekana” alisema Maboko.Aliwaambia
wajumbe wa mkutano huo ,kuwa asasi mwamvuli zinarahisisha kazi ya
uratibu kwa TACAIDS lakini changamoto waliyonayo ni kutopata ripoti za
asasi hizo .
Nae
mratibu wa mtandao wa viongozi wa dini wanaoishi na virusi vya ukimwi
,(TANERELA),mchungaji Amin Sandewa alisema wanawajengea uwezo wa kielimu
viongozi wa dini wanaoishi na virusi hivyo ili kupambana na ukimwi na
kuwa vielelezo kwa wengine.
Sandewa alisema, ugonjwa huo hauchagui ,muumini,viongozi wa dini wala mwalimu hivyo aliiomba jamii kuachana na unyanyapaa.Meneja
ufuatiliaji na takwimu ,kutoka baraza la Taifa la watu wanaoishi na
virusi vya ukimwi (NACOPHA) ,Rachel Jacob alifafanua wanaratibu shughuli
za masuala ya ukimwi kwa kulenga mtu mmoja mmoja,kundi na mtandao .
Kwa
mujibu wake ,katika kufanikisha shughuli hizo wameshafikia halmashauri
154 nchini kwa kushirikiana na viongozi walioteuliwa ambao wana
maambukizi kwa ajili ya kusaidia kuwafikia watu na vikundi hivyo .
Rachel alibainisha ,kwasasa wana wajumbe 616,984 miongoni mwao asilimia 44 ni wanaume waliojitokeza kuweka wazi afya zao .Alifafanua
zoezi hilo nao wanaendelea nalo ,kuhakikisha kufikia halmashauri zote
hasa kundi la wanaume ambalo bado halina mwamko huo.
Katika mkutano huo ,asasi mwamvuli zilizoshiriki ni pamoja na NACOPHA,TAIFO,BAKWATA,FAJISAM-PENTECOSTE,TANERELA,TEC,BAHAI,National Steering Committe, na TIENAI.
SERIKALI YAAGIZA OPERESHENI YA KUONDOA WAVAMIZI WA KIGENI KATIKA KISIWA CHA IZINGA MKOANI KAGERA
.........................................................................................
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa siku 7 kwa
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kwa kushirikiana na
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Karagwe kufanya Operesheni ya
kuwaondoa wavamizi wa nchi jirani wanaodaiwa kulima na kufiga ndani
kisiwa cha Izinga kilichopo ndani ya Pori la Akiba la Kimisi mkoani
Kagera.
Ametoa
agizo hilo jana wakati wa ziara yake
wilayani Karagwe mkoa wa Kagera muda mfupi baada ya kupokea taarifa na
malalamiko ya kukamatwa kwa mifugo ya Watanzania ndani ya kisiwa cha
Mubali huku kukiwepo mazao yanayodaiwa kulimwa na wananchi wa Rwanda
katika kisiwa kingine cha Izinga.
“Ndani ya siku saba hicho
kisiwa cha Zinga msafishe kila kitu, Mkuu wa Wilaya msaidie mtengeneze kikosi
kiende kule kitoe takataka zote zilizoko kule, inakua ngumu kuadministrate (kutawala)
wengine wa kwetu tunawatoa alafu wa nchi nyingine wamekaa, unatawalaje?”. Aliuliza
kwa mshangao Dk. Kigwangalla.
Alisema watanzania wakienda upande wa Rwanda kuvua samaki ziwa Ihema wanauawa mara moja bila mjadala, wakati kwa upande wa Tanzani raia wa nchi hiyo wapo wengi na wengine wamepewa Uraia wa Kuasili (Citizenship by Naturalisation, CN) na huwa hawafanyiwi vitendo vya unyanyasaji wala mauaji jambo ambalo alisema ipo haja kama nchi kuchukua hatua ili kukomesha vitendo hivyo.
Alisema watanzania wakienda upande wa Rwanda kuvua samaki ziwa Ihema wanauawa mara moja bila mjadala, wakati kwa upande wa Tanzani raia wa nchi hiyo wapo wengi na wengine wamepewa Uraia wa Kuasili (Citizenship by Naturalisation, CN) na huwa hawafanyiwi vitendo vya unyanyasaji wala mauaji jambo ambalo alisema ipo haja kama nchi kuchukua hatua ili kukomesha vitendo hivyo.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, David Kenyata
alisema atatekeleza agizo hilo la Waziri Kigwangalla kwa haraka ndani ya muda
uliotolewa ili kumaliza mgogoro huo.
Katika hatua nyingine
Waziri Kigwangalla alikataa ombi la Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent
Bashugwa la kuiomba Serikali iwamegee wananchi wa vijiji jirani sehemu ya eneo katika
Pori la Akiba Kimisi kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji.
“Ardhi mimi sitatoa, sjui
mlima sjui nini, siwezi kwenda kupeleka hilo ombi kwa Mhe. Rais, kabisa, hicho
ni kitu ambacho hatuwezi kufanya kwa sasa’,” Alisisitiza Dk. Kigwangalla.
Mbunge huyo pia aliiomba
Serikali kuweka uzio wa waya kwa ajili ya kutenganisha mpaka wa hifadhi hiyo na
vijiji kwa madai ya kuepuka ukamataji wa mifugo ya wananchi unaofanywa na
askari wa wanyamapori kwenye ardhi za vijiji na kuingizwa hifadhini na kutozwa
faini, hoja iliyopigwa vikali na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka.
Hata hivyo, Dk. Kigwangalla
alikataa ombi hilo na kusema kuwa mipaka ya hifadhi hiyo ni mikubwa kuwezesha
utekelezaji wa ombi hilo. Alisema Serikali itatengeneza mtandao wa barabara
zinazounganisha hifadhi hiyo na vijiji kwa ajili ya kuimarisha doria na
shughuli za utalii pamoja na kujenga ofisi ndogo za pori hilo katika kila wilaya
inayohusika na pori hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey
Mheluka aliwataka wananchi wanaofanya vitendo vya kuingiza mifugo kwenye pori
hilo wakati wa usiku kuacha mara moja kwa kuwa wakimatwa watachukuliwa hatua
kali za kisheria.
Alisema malalamiko ya
wananchi hao kuwa askari wa wanyamapori wanakamata mifugo yao kwenye maeneo ya
vijiji na kuiingiza hifadhini kwa lengo la kuwatoza faini kuwa sio ya kweli na kwamba
malalamiko yanakuja kwakuwa hukamatwa asubuhi wakiwa wameshatoka kulisha mifugo
hifadhini.
Kisiwa
hicho cha Izinga ambacho kipo katika wilaya ya Karagwe mkoani Kagera
kina ukubwa wa Kilomita za Mraba 12 na kinapakana na nchi Rwanda.
Pori
la Akiba Kimisi liliqnzishwa mwaka 2003 kwa Tangazo la Serikali na 116
na lina ukubwa wa kilomita za mraba 1,030. Pori hilo lina wanyamapori
mbalimbali wakiwemo Tembo, Twiga, Simba na Chui.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Mbunge wa
Jimbo la Karagwe, Innocent Bashugwa kukagua Pori la Akiba Kimisi wakati
wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi
katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera jana.
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na baadhi ya viongozi wa kijiji
cha Mwisheni alipofika kukagua Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya
kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani
Kagera jana.
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Karagwe,
Innocent Bashugwa kukagua Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua
migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya ya Karagwe mkoani
Kagera jana.
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe,
Godfrey Mheluka wakati akikagua Pori la Akiba Kimisi akiwa kwenye ziara yake ya
kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani
Kagera jana.
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akionyesha mpaka wa Pori la Akiba Kimisi wakati
wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya
hiyo mkoani Kagera jana. Kulia ni Mkuu wa Karagwe, Godfrey Mheluka na Mbunge wa
Karagwe, Innocent Bashungwa (kulia kwake).
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Lut.
Col. Michael Mutenjele (kushoto) wakati wakivuka kivuko cha Ruvuvu wakati wa ziara
yake ya kutembelea na kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika
Wilaya hiyo mkoani Kagera jana.
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia baadhi ya mifugo iliyokamatwa
ndani ya Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi
kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya Ngara mkoani Kagera jana. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii).
Comments
Post a Comment