Mabinti 11 wa marais wa Afrika wanaoongoza kwa urembo
Bona Mugabe
Faith Elizabeth Sakwe
Zahra Buhari
Isabel dos Santos
Brenda Biya
Thuthukile Zuma
Aya Abdel Fattah al-Sisi
Ngina Kenyatta
Malika Bongo Ondimba
Ange Kagame
Princess Sikhanyiso Dlamini
BARA la Afrika licha ya
matatizo lukuki yanayolikabili kijamii, uchumi na kisiasa bado limebarikiwa na vitu
vingi ikiwamo wingi wa maliasili kuliko mabara yote duniani.
Ukiachana na maliasili,
miongoni mwa vitu hivyo vingi ilivyobarikiwa ni urembo wa mabinti zake na ambao
wana sifa tofauti tofauti zilizo maalumu na kuwafanya wavutie mbele ya macho ya
hadhara.
Hata hivyo, ni watu wachache
wanaotambua kuwa baadhi ya wakuu wa nchi pia wamebarikiwa kuwa na mabinti
warembo na wasomi.
Hiyo ni pamoja na kwamba
inafahamika wazi katika nafasi zao za uongozi hata kabla hawajawa marais
huwawia rahisi kupata wake warembo wanaokuwa chimbuko la mabinti hao.
Wafuatao ni miongoni mwa
mabinti 10 wa viongozi wakuu wa nchi za Afrika wanaotamba kwa urembo barani
humu:
1. Bona Mugabe
Bona ni binti wa Rais wa
Zimbabwe na Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika (AU), Robert Mugabe. Ameolewa
kwa Simba Chikore. Alisomea uhasibu na masuala ya fedha katika Chuo Kikuu cha
City cha Hong Kong na aliendelea na masomo yake katika masuala ya kibenki na
fedha katika Taasisi ya Usimamizi ya Singapore. Kwa sasa anafanya kazi katika
kampuni ya maziwa ya Alpha & Omega huko Mazowe, Zimbabwe.
2. Faith Elizabeth Sakwe
Ni binti mkubwa wa aliyekuwa
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan na Dame Patience. Kwa sasa ameolewa na
Godswill Osim Edward. Wenzi hao wachanga walichumbiana mwaka jana.
3. Zahra Buhari
Huku akiingia madarakani rasmi
Ijumaa iliyopita, Rais mpya wa Nigeria, Muhammadu Buhari naye ni miongoni mwa
viongozi waliobarikiwa mabinti warembo-Zahra Buhari, ambaye ni mwanafunzi wa
Utabibu katika Chuo Kikuu cha Surrey nchini Uingereza.
4. Isabel dos Santos
Ni binti wa Rais wa Angola,
José Eduardo dos Santos. Akiwa katika umri wa miaka 40, Dos Santos aliwahi
kutajwa kama mwanamke pekee barani Africa aliye bilionea na pia mwenye umri
mdogo; hii ni kwa mujibu wa Forbes. Serikali huhesabu taarifa hizo kama suala
la ufahari wa taifa na ushahidi kwamba taifa hilo lenye watu milioni 21.47 kwa
idadi ya mwaka 2013, limefika mahali pazuri baada ya kutokea katika vita ndefu
ya wenyewe kwa wenyewe.
5. Brenda Biya
Binti wa Rais wa Jamhuri ya
Cameroon pia anasifiwa katika mitandao maarufu ya jamii na hufuatiliwa na kundi
la wafuasi 3,000. Brenda alifungua akaunti yake ya Instagram mwaka 2012 na
huchangia picha zake za uanafunzi kila siku na maisha ya familia, mawazo na
mitazamo.
6. Thuthukile Zuma
Ni binti mdogo kati ya wanne
wa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kutoka kwa aliyekuwa mkewe Nkosazana
Dlamini-Zuma, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU).
Thuthukile ni mnadhimu mkuu katika Idara ya Mawasiliano na Huduma za Posta
Afrika Kusini. Anaonekana mrembo kwa
staili yake ya ukataji nywele fupi.
7. Aya Abdel Fattah al-Sisi
Ni binti pekee wa Abdel Fattah
al-Sisi, mkuu wa zamani wa jeshi la Misri, ambaye kwa sasa ni Rais wa Misri. Ni
mwenye mvuto, heshima na adabu.
8. Ngina Kenyatta
Ni binti wa Rais wa Kenya,
Uhuru Kenyatta. Mrembo huyo, ambaye mara nyingi hugonganisha vichwa katika
mitandao ya kijamii nchini Kenya kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi. Alichukua
jina hilo kutoka kwa bibi yake, Mama Ngina Kenyatta. Anahesabiwa sana kama mtu
mwenye kujichanganya mno na jamii na mwingi wa utata.
9. Malika Bongo Ondimba
Malika Bongo Ondimba(32), ni
binti pekee wa Rais wa Gabon, Ali Bongo Ondimba. Msichana huyo anaelezwa kama
‘mwenye bidii ya kazi’ na familia yake.
10. Ange Kagame
Ange ni mtoto wa pili na binti
pekee wa Rais wa Rwanda, Paul Kagame. Ni mhisani na amekuwa akihusika na
shughuli za uwezeshaji wanawake, elimu, upunguzaji umasikini na kinga za
maradhi.
Ange alichomoza zaidi akiteka
vichwa vya habari duniani wakati alipoambatana na baba yake wakati wa mkutano
wa Marekani na viongozi wa Afrika mwaka jana kwa urembo na urefu kumzidi baba
yake. Ange alizaliwa Septemba 8, 1993, mjini Brussels, Ubelgiji.
11. Princess Sikhanyiso Dlamini
Binti
mfalme Sikhanyiso, alizaliwa Septemba Mosi 1987, ni binti mkubwa wa Mfalme
Mswati III wa Swaziland. Ni mtoto wake wa kwanza kati ya
Comments
Post a Comment