MGEJA ASEMA URAIS SI MAJARIBIO, DKT. SAMIA ANATOSHA
Na Mwandishi Wetu, Kahama na Nzega Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mwanasiasa mkongwe nchini, Ndugu Khamisi Mgeja (anayeongea pichani), amewatahadharisha Watanzania kutofanya makosa kwa kuchagua wagombea wa urais wasiokuwa na uzoefu wa kiuongozi na ambao hawajawahi kufanya kazi yoyote ya serikali, hata katika ngazi za mitaa, akisema kufanya hivyo ni kosa la kujitakia. Mgeja alikumbusha usia wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyewahi kusema kuwa kiongozi bora wa nchi hii hatatoka nje ya CCM, bali atatoka ndani ya CCM. Amesema kuwa kiongozi huyo si mwingine bali ni Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ni chaguo sahihi la Watanzania. Mgeja alitoa kauli hiyo katika mikutano ya kampeni iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora na Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, alipokuwa akinadi wagombea wa ubunge akiwemo Hussein Bashe (Nzega) na Benjamini Ng’ayiwa (Kahama Mjini). Akiwa katika vijiji vya Nyanhembe na Ufala wilayani Kahama, Mgeja aliw...