MWAKAGENDA AKISAKA KURA ZA WAGOMBEA WA CCM JIMBONI MAKAMBAKO

Mbunge  Mstaafu Sophia Mwakagenda, akiwa jukwaani akimuombea kura  Mgombea Ubunge Jimbo la Makambako Daniel Godfrey Chongolo, pamoja na kura za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa jimbo hilo. Akizungumza kwa kujiamini huku akishangiliwa na wananchi waliojitokeza katika mkutano huo aliwaomba wanamakambako kutofanya kosa siku ya 29.10.2025 kujihimu mapema kwenda kupiga kura kuwapa kura za ndiyo wagombea wote wa Chama cha Mapinduzi, aliwaambia kelele za mpangaji hazimzuii mwenye nyumba kulala alibainisha kuwa kelele za wapinzani zisiwababaishe nchi ipo salama  na maendeleo makubwa yanakuja  wakiamini chama CCM. 

"Nawaombeni wanaccm wenzangu na wasiokuwa wanaccm Mgombea Dkt. Samia, hatanii akisema atawaletea mandelea makubwa wananchi wa Tanzania  anasema kweli hebu tumwamini muone kazi yake mwanamama yoyote hawi muomgo hebu tujitokeze tumpe kura zote",alisema Mwakagenda. Kuhusu Chongolo, aliwaomba waanamakambako wasipoteze muda kufikilia mbunge mwingine huyo anafaa kashika nyadhifa nyingi  Serikalini na nafasi ya juu ya ukatibu Mkuu wa Chama CCM, hashindwi kitu maendeleo nje nje makambako yanakuja.

Mwakagenda akiwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda  jimboni Makambako leo
 

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA