UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Leo ni Miaka Mitano ya Kumbukumbu ya Kifo cha Amina Chifupa Mpakanjia


Ilikuwa June 26.2007 tulipompoteza Mh. Amina Chifupa Mpakanjia. Ikiwa pia ni siku ya upigaji vita matumizi ya madawa ya kulevya.

Amina leo ametimiza Miaka Mitano sasa tangu alipotutoka na ataendelea kukumbukwa kwa ucheshi wake, mbwembwe zake katika utangazaji wake kupitia kipindi cha Chuchuchu, Kwa raha zetu, Bambataa na Leo tena katika Redio ya Clouds FM.

Mpaka anakumbwa na mauti alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).Watanzania wataendelea kumuenzi na  atakumbukwa kwa vita yake dhidi ya wauzaji wa dawa ya kulevya.

Wakati leo tukimkumbuka Bi. Amina Chifupa, serikali nayo inaadhimisha Siku ya Kupambana na Dawa za kulenya Nchini.

                                           Pumzika kwa Amani Amina Chifupa!

Chini ni picha za baadhi ya matukio mbalimbali ambayo Amina chifupa aliweza kushikiriki wakati wa Uhai wake. Picha Hizi zilipigwa enzi hizo

Amina Chifupa alipenda michezo hali iliyompelekea mara kwa mara kutoa misaada mbalimbali ya vifaa vya michezo. Hapa ilikuwa katika ukumbi wa Manispaa ya Temeke, akikabidhi vifaa hivyo kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, John  Nchimbi.

Amina Chifupa akiteta jambo na Mwanasiasa Mkongwe nchini, Alnoor Kassum, katika moja ya shughuli za kitaifa enzi za uhai wake. Hapa ilikuwa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Foundation jijini Dar.

Siku Amina Chifupa alipokula kiapo bungeni mjini Dodoma.

Amina (wa pili kushoto), akiwa na wabunge wenzake siku walipotembelea katika Nyumba ya Vipaji ya THT, wakati ikiwa pale Kinondoni katikati ya Biafra na Moroco.

Amina alikuwa mpenzi wa muziki pia hapa ilikuwa wakati huo ikiitwa Sheraton Hotel kwa sasa ni Serena, Bendi ya Twanga walikuwa wakitumbuiza katika hafla moja.

Amina alipiga vita matumizi ya dawa za kulevya na hapa alikuwa mgeni rasmi katika semina iliyotolewa kwa wanafunzi kuhusu madhara ya dawa hizo.

Amina Chifupa, alipenda sana watoto hali iliyomfanya kujikita katika utoaji wa misaada katika vituo mbalimbali vya kulea watoto yatima na waliokatika mazingira magumu. Hapa ilikuwa baada ya kutoa msaada katika kituo kimoja kilichopo Sinza.
Wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Amina aliweza kuandaa futari na kukaribisha watu mbalimbali. Hapa ilkuwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar, akijadiliana jambo na Bi. Shyrose Bhanji ambaye sasa ni Mbunge wa Afrika Mashariki.


Kwa kuwa Amina Chifupa Mpakanjia alikuwa kipenzi cha watu hali iliyompelekea kujizolea umaarufu mkubwa, siku alipotangulia mbele ya haki ulimwengu mzima ulijua. Bwana alitoa na Bwana almetwa jina lake lihimidiwe, ampumzishe huko aliko mahali pema peponi amiiinaaa

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA