Posts

Showing posts from April, 2024

WAZIRI WA NISHATI MAVUNDE AWASILISHA BAJETI YAKE BUNGENI LEO

Image
HOTUBA YA MHESHIMIWA ANTHONY PETER MAVUNDE (MB.), WAZIRI WA MADINI AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, baada ya kupokea taarifa iliyowasilishwa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyochambua bajeti ya Wizara ya Madini, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu sasa likubali kupokea, kujadili na kupitisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 pamoja na Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Kawaida na ya Maendeleo ya Wizara ya Madini na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025. 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote, ninamshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa fadhila zake na kuijalia nchi yetu amani na utulivu na kutuwezesha kushiriki katika mkutano huu wa 15 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa unyenyekevu mkubwa, ninamuomba Mwenyezi Mungu atuongoze vyema na kutupa busara na hekima katika kujadili H

MAKALA AWAVAA CHADEMA ASEMA WAMEISHIWA NA MANENO YA KUSEMA SASA WANAENEZA CHUKI NA UBAGUZI

Image
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Amos Makala, akizungumza na wanahabari leo jijini Dodoma , ambapo alidai viongozi wa Chadema wameanza kueneza chuyki na uongo dhidi ya Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema pamoja na kuifahamu katiba lakini wameamua kupotosha  huku wakielewa ukweli kwamba Rais Samia alichaguliwa na wananchi akiwa sambamba na marehemu Dkt John Magufuli. Amewaomba wananchi wawapuze hawana cha kusema sasa kwani Rais Samia anaupiga mwingi sasa hivi kila kona ya nchi anamwagiwa sifa za utendaji kazi uliotukuka acha waandamane watachoka nchi inasonga mbele .  

HOTUBA YA MHESHIMIWA BALOZI DKT. PINDI HAZARA CHANA (MB), WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AKIWASILISHA BUNGEN LEO

Image
HOTUBA YA MHESHIMIWA BALOZI DKT. PINDI HAZARA CHANA (MB), WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 ii iii VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA MHE. BALOZI DKT. PINDI HAZARA CHANA (MB) Waziri wa Katiba na Sheria MHE. JUMANNE ABDALLAH SAGINI (MB) Naibu Waziri wa Katiba na Sheria BI. MARY GASPAR MAKONDO Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria DKT. KHATIBU MALIMI KAZUNGU Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria iv VIONGOZI WA MAHAKAMA YA TANZANIA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA Jaji Mkuu wa Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama MHE. MUSTAPHER MOHAMED SIYANI Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania MHE. EVA KIAKI NKYA Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania PROF. ELISANTE OLE GABRIEL Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama v WAKUU WA TAASISI ZA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA MHE. JAJI DKT. ELIEZER MBUKI FELESHI Mwanasheria Mkuu wa Serikali BW. SYLVESTER ANTHONY