WAZIRI WA NISHATI MAVUNDE AWASILISHA BAJETI YAKE BUNGENI LEO

HOTUBA YA MHESHIMIWA ANTHONY PETER MAVUNDE (MB.), WAZIRI WA MADINI AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, baada ya kupokea taarifa iliyowasilishwa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyochambua bajeti ya Wizara ya Madini, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu sasa likubali kupokea, kujadili na kupitisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 pamoja na Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Kawaida na ya Maendeleo ya Wizara ya Madini na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025. 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote, ninamshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa fadhila zake na kuijalia nchi yetu amani na utulivu na kutuwezesha kushiriki katika mkutano huu wa 15 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa unyenyekevu mkubwa, ninamuomba Mwenyezi Mungu atuongoze vyema na kutupa busara na hekima katika kujadili Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 kwa nia njema ya kuendeleza nchi yetu na kuboresha ustawi na maendeleo ya watanzania. 1 2 3. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kumpongeza na kumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utendaji wake wenye maono, maridhiano, weledi, uwajibikaji na ujasiri kwa manufaa mapana ya Taifa. Aidha, Mheshimiwa Rais amekuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya Sekta ya Madini kwa kutoa miongozo, maagizo na maelekezo mbalimbali kwa ajili ya kuvutia uwekezaji na kuikuza sekta. 4. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee nitumie fursa hii adhimu kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Rais kwa kuniamini na kunipa dhamana ya kusimamia Sekta ya Madini. Ni ahadi yangu kwa Mheshimiwa Rais, na Bunge lako Tukufu pamoja na Watanzania kwamba nitaitumikia nafasi hii kwa uadilifu, uaminifu na kwa uwezo wangu wote ili kuendeleza sekta hii muhimu. 5. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, Mheshimiwa Rais ametuonesha kwa vitendo namna anavyoithamini Sekta ya Madini kwa kushiriki yeye mwenyewe katika shughuli za madini ikiwemo kufanya uhamasishaji mkubwa kwenye uwekezaji. Pia, ameshiriki kwenye hafla za utiaji saini mikataba ya uchimbaji wa madini, ununuzi na uzinduzi wa 2 3 mitambo maalum ya uchorongaji kwa ajili ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kuongeza tija na uwezeshaji katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya shughuli za madini. 6. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Awamu ya Sita tumeshuhudia mafanikio mbalimbali katika Sekta ya Madini ikiwemo: kuendelea kuongezeka kwa Mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa kutoka asilimia 6.7 mwaka 2020, asilimia 7.3 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 9.1 mwaka 2022; ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali uliongezeka kutoka shilingi 588,047,051,190.03 mwaka 2020/2021, shilingi 623,237,296,973.40 mwaka 2021/2022 hadi shilingi 678,042,598,813.92 mwaka 2022/2023. 7. Mheshimiwa Spika, mafanikio mengine ni pamoja na kuongezeka kwa masoko na vituo vya ununuzi wa madini kutoka 41 na 61 mwaka 2020/2021 hadi kufikia 42 na 100 mwaka 2023/2024 ambapo kulifanyika biashara ya madini yenye thamani ya shilingi 2,095,960,697,019.40 na shilingi 1,926,415,580,991.11 mtawalia. Aidha, Serikali imenunua mitambo mitano (5) ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kuigawanya kwenye maeneo mbalimbali ya uchimbaji mdogo wa madini nchini. 8. Mheshimiwa Spika, ili kuendeleza Madini Muhimu na Madini Mkakati, Serikali imetoa leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini Tembo (Heavy Mineral Sands) kwa 3 4 mradi wa Tajiri uliopo Wilaya ya Pangani, Mkoa wa Tanga pamoja na Leseni ya Ujenzi wa Kiwanda cha Kusafisha Madini ya Metali Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga. 9. Mheshimiwa Spika, namshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miongozo yake mbalimbali anayoitoa yenye lengo la kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango endelevu na kuwanufaisha watanzania na Taifa kwa ujumla. 10. Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi madhubuti na maelekezo anayoyatoa ili kufanikisha utendaji kazi Serikalini. Nimshukuru zaidi kwa hotuba yake iliyojaa maono mazuri aliyoiwasilisha hapa bungeni ambayo inatoa mwelekeo wa utekelezaji wa kazi za Serikali. Hotuba hiyo kwa kiasi kikubwa imeonesha mapitio ya uendeshaji wa shughuli za Serikali katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020. 4 5 11. Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko (Mb.), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kwa kuaminiwa na kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kushika nyadhifa hizo. Aidha, nimshukuru kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuisimamia na kuijenga Sekta ya Madini kwa ubunifu na uadilifu mkubwa alipokuwa Waziri wa Madini. 12. Mheshimiwa Spika, Viongozi hawa wote wamekuwa tayari kushirikiana nasi muda wote, kutusikiliza na kutupa maelekezo na miongozo mbalimbali ambayo yametusaidia sana katika kutekeleza majukumu ya Wizara kwa ufanisi zaidi. 13. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kukupongeza wewe binafsi kwa kuendelea kuliongoza Bunge kwa ustadi, umahiri, hekima, busara na ubunifu mkubwa. Aidha, niwapongeze Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb.), Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuendelea kushirikiana nawe katika kuliongoza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa weledi mkubwa. Ni dhahiri kuwa mmeonesha ukomavu mkubwa wa kisiasa wakati wote wa kuendesha vikao vya Bunge. Tuna imani kuwa mtaendelea kuliongoza Bunge kufanya maamuzi sahihi na yenye tija kwa maslahi mapana ya Taifa na kulifanya Bunge letu liendelee kuheshimika ndani na nje ya nchi yetu. 5 6 14. Mheshimiwa Spika, naomba niwapongeze Mheshimiwa Dkt. David Mathayo David (Mb.), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mheshimiwa Kilumbe Shabani Ng'enda (Mb.), Makamu Mwenyekiti wa Kamati kwa kuchaguliwa kuiongoza Kamati hii. Aidha, nawapongeza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa kuteuliwa kuwa wajumbe wa Kamati hiyo. Tunaipongeza Kamati kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa ushauri na maelekezo mbalimbali ambayo yanasaidia kuongeza ufanisi na umakini wa utendaji kazi wa Wizara. Vilevile, ninaishukuru Kamati kwa kujadili kwa kina Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fungu 100, kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na kuyapitisha kwa kauli moja. Napenda kuliahidi Bunge lako Tukufu kuwa nitaendelea kuipa Kamati ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inaendelea kuimarika na kuwanufaisha watanzania. 15. Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani na pongezi kwa Bunge lako Tukufu kwa kazi nzuri ambazo limekuwa likifanya katika kuisimamia na kuishauri Serikali, ikiwemo Wizara ya Madini. Kupitia kwako, naliomba Bunge liendelee kutupatia ushirikiano ili kuiendeleza sekta hii muhimu katika kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya Taifa. Aidha, napenda kuwapongeza Waheshimiwa 6 7 Mawaziri na Naibu Mawaziri wote kwa kuaminiwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongoza Wizara mbalimbali. Pia, ninawashukuru wote kwa ushirikiano wanaonipa katika kutekeleza majukumu ya kusimamia Sekta ya Madini. 16. Mheshimiwa Spika, kipekee kabisa, nitumie fursa hii kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini kwa kuendelea kunipa ushirikiano kama Mbunge wao na kunivumilia ninapokuwa nikitekeleza majukumu mengine ya kitaifa kama Waziri wa Madini. 17. Mheshimiwa Spika, napenda nimshukuru kwa dhati kabisa Dkt. Steven Lemomo Kiruswa (Mb.), Naibu Waziri wa Madini, kwa ushirikiano anaonipa katika kutekeleza majukumu ya Wizara. Aidha, napenda kumshukuru Bw. Kheri Abdul Mahimbali, Katibu Mkuu, Bw. Msafiri Lameck Mbibo, Naibu Katibu Mkuu na Dkt. AbdulRahman Shabani Mwanga, Kamishna wa Madini kwa uchapakazi wao mahiri na ushirikiano wanaonipatia katika kutekeleza majukumu ya Wizara. Pia, niishukuru Menejimenti ya Wizara pamoja na Wenyeviti wa Bodi, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini pamoja na wafanyakazi wote kwa ushirikiano na utendaji kazi mzuri katika kutekeleza majukumu yao. 7 8 18. Mheshimiwa Spika, naishukuru sana familia yangu mke wangu Jacquelyne Moses Lupasa na watoto wangu Atarah na Allan kwa upendo, uvumilivu, ushirikiano na maombi yao wakati wote ninapotekeleza majukumu yangu. Wamekuwa wavumilivu na wenye ushirikiano mkubwa kwa kipindi chote ninapokuwa ninatekeleza majukumu ya ubunge na uwaziri na wamekubali kubeba baadhi ya majukumu ya familia. 19. Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa naungana na wenzangu kutoa pole kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, familia na watanzania wote kwa ujumla kwa kuondokewa na Viongozi wetu mashuhuri, shupavu, walioipenda na kuitumikia nchi hii ambao ni Hayati Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu na Dkt. Ibrahim Msabaha aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani. 20. Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa niungane na watanzania wengine kutoa pole kwa wananchi wa Jimbo la Mbarali kwa kuondokewa na aliyekuwa Mbunge wao Mheshimiwa Francis Mtega na wananchi wa Jimbo la Kwahani kwa kuondokewa na 8 9 aliyekuwa Mbunge wao Mheshimiwa Ahmed Yahya Abdulwakil. Mwenyezi Mungu awarehemu. 21. Mheshimiwa Spika, kufuatia majanga mbalimbali yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha na ajali za barabarani naomba kutoa pole kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watanzania wote kwa ujumla kutokana na vifo, majeraha, upotevu na uharibifu wa mali na miundombinu. Majanga hayo ni pamoja na maporomoko ya udongo yaliyotokea huko Hanang na mafuriko ya Rufiji. 22. Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa salamu za shukrani na pole, naomba sasa nijielekeze katika maeneo mahsusi ya hotuba hii ambayo ni: Mwenendo wa Biashara ya Madini Duniani; Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024; na Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2024/2025. B. MWENENDO WA BIASHARA YA MADINI DUNIANI 23. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha kuanzia Julai, 2023 hadi Machi, 2024, bei ya madini ya dhahabu kwa wakia ilipanda hadi kufikia wastani wa Dola za Marekani 2,138.01 ikilinganishwa na bei ya wastani wa Dola za Marekani 1,854.54 katika kipindi cha Julai 2022 hadi Machi 2023. Kuongezeka kwa bei ya dhahabu kunatokana na 9 10 sababu mbalimbali ikiwemo mahitaji makubwa ya madini hayo duniani. 24. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa madini ya almasi, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024, mwenendo wa biashara ya madini hayo duniani umeendelea kusuasua kutokana na mdororo wa uchumi uliosababishwa na madhara ya vita kati ya Urusi na Ukraine. Madini hayo yameshuka bei duniani kwa asilimia 19 kwa mwezi Machi, 2024. Aidha, wastani wa mauzo ya madini ya almasi katika kipindi husika ni karati 201.71 yenye thamani ya dola za Marekani 43,231,183.71 ikilinganishwa na karati 271.74 yenye thamani ya dola za Marekani 50,824,739.77 katika kipindi cha Julai 2022 hadi Machi, 2023. Hatua zilizoanza kuchukuliwa na wazalishaji mbalimbali wa almasi duniani ni kupunguza uzalishaji wa almasi ili kuimarisha bei ya madini hayo. 25. Mheshimiwa Spika, napenda kulifahamisha Bunge lako Tukufu kwamba nchi yetu ni miongoni mwa nchi zilizobarikiwa kuwa na madini mkakati ambayo uhitaji wake ni mkubwa kwenye nishati safi na salama na teknolojia nyingine za kisasa duniani. Aidha, uhitaji huu unatokana na utekelezaji wa azimio la pamoja la dunia la kupunguza hewa ya ukaa ifikapo 2050 (Net Zero Emission). Miongoni mwa madini mkakati yanayopatikana nchini ni pamoja na 10 11 lithium, cobalt, nikeli, shaba, aluminium, zinki, kinywe na rare earth elements (REE). 26. Mheshimiwa Spika, ili nchi yetu iweze kunufaika na madini hayo, Wizara imeandaa mkakati wa uendelezaji wa madini muhimu na madini mkakati hapa nchini. Mkakati huo unalenga kuhakikisha kwamba madini hayo yanaongezwa thamani hapa nchini ikiwemo kuzalisha bidhaa zinazohitajika katika soko kama vile betri za magari ya umeme na hivyo kuongeza manufaa kwa nchi ikiwemo kuongeza mapato ya Serikali na ajira kwa watanzania.

Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa, akimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, mazungumzo hayo yalifnyika ndani ya ukumbi wa bunge leo.
Mbunge Asenga akichangia bungeni leo

Naibu Waziri Silinde, akijibu baadhi ya maswali ya wabunge


Naibu Waziri Maryprisca Mahundi, akijibu maswali ya wabunge
Mbunge wa Nyanghwale, Nassoro Amar, akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wanaotoka jimboni kwake baada ya kutembelea bungeni leo
Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko, akizungumza na Naibu Spika Zungu leo Bungeni

 Mbunge wa Viti Maalum, Bernedetha Mushashu, akisikiliza kwa makini watoa mada katika warsha ya Nishati iliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa leo

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.