Posts

MAADHIMISHO YA MIAKA 62 YAFANA JIJINI DODOMA

Image
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati akimpatia kioaza sauti Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, afafanue jambo Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati *Rais Samia atunukiwa Tuzo ya Ubinadamu; *Ombi la ruzuku kwa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania lafanyiwa kazi; Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (Tanzania Redcross Society) katika utoaji huduma mbalimbali za kibinadamu hususan nyakati za dharura. Dkt. Biteko amesema hayo leo (Mei 11, 2024) Jijini Dodoma alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgemi rasmi katika maadhimisho ya miaka 62 ya Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania ambapo amesema huduma zinazotolewa na chama hicho zinazingatia sheria na kanuni na taratibu za kuanzishwa kwa chama hicho ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bila upendeleo

TANZANIA KUPOKEA WANAJESHI 300 KUTOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA

Image
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Luteni Jenerali Salum Haji Othman amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM), ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Baraza hilo,Navy Captain Robert Recchie  Upanga,  Jijini Dar Es Salaam . Katika mazungumzo hayo Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda,ameukaribisha Ujumbe huo hapa nchini na kuwaeleza kutumia fursa waliyoipata kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii  vilivyoko hapa nchini. Naye Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) Navy Captain Robert Recchie, amelishukuru JWTZ kwa mapokezi na maandalizi ya hali ya juu kuelekea kwenye Mkutano wa 79 wa Baraza hilo Duniani. Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 14 Mei 2024 Jijini Dar Es Salaam ukiwashirikisha zaidi ya Wajumbe 300 kutoka Majeshi mbalimbali Duniani.  

WAZIRI AWESO AWASILISHA BUNGENI OMBI LA KUPITISHIWA BAJETI YA WIZARA HAKE

Image
HOTUBA YA WAZIRI WA MAJI MHE. JUMAAJUMAA HAMIDU AWESO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA MAJI KWA MWAKA 2024/25 1. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Mheshimiwa Jackson Gedion Kiswaga (Mb) kuwasilisha taarifa ya Kamati iliyochambua utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Maji ya mwaka 2023/24 na kupokelewa na Bunge lako Tukufu, ninaomba sasa kutoa hoja kwamba, Bunge lako likubali kupokea, kujadili na kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2024/25. 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kutupatia afya njema na kutuwezesha kukutana kwa siku ya leo. Aidha, kwa moyo wa unyenyekevu mkubwa ninamuomba Mwenyezi Mungu atujalie busara, hekima na kutuongoza vema wakati wa kujadili wasilisho la hotuba yangu pamoja na bajeti kuu ya Serikali kwa nia thabiti ya kujenga taifa letu na kuende