HOTUBA YA MHESHIMIWA BALOZI DKT. PINDI HAZARA CHANA (MB), WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AKIWASILISHA BUNGEN LEO

HOTUBA YA MHESHIMIWA BALOZI DKT. PINDI HAZARA CHANA (MB), WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 ii iii VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA MHE. BALOZI DKT. PINDI HAZARA CHANA (MB) Waziri wa Katiba na Sheria MHE. JUMANNE ABDALLAH SAGINI (MB) Naibu Waziri wa Katiba na Sheria BI. MARY GASPAR MAKONDO Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria DKT. KHATIBU MALIMI KAZUNGU Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria iv VIONGOZI WA MAHAKAMA YA TANZANIA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA Jaji Mkuu wa Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama MHE. MUSTAPHER MOHAMED SIYANI Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania MHE. EVA KIAKI NKYA Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania PROF. ELISANTE OLE GABRIEL Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama v WAKUU WA TAASISI ZA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA MHE. JAJI DKT. ELIEZER MBUKI FELESHI Mwanasheria Mkuu wa Serikali BW. SYLVESTER ANTHONY MWAKITALU Mkurugenzi wa Mashtaka DKT. BONIPHACE NALIJA LUHENDE Wakili Mkuu wa Serikali BW. FRANK KANYUSI FRANK Kabidhi Wasii Mkuu vi WAKUU WA TAASISI ZA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA MHE. JAJI MSTAAFU MATHEW P. MWAIMU Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora MHE. JAJI PROF. PAUL FAUSTIN KIHWELO Mkuu wa Chuo Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto BW. GEORGE MANDEPO Katibu Mtendaji, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania PROF. SIST MRAMBA Mkuu wa Chuo, Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania vii i YALIYOMO ORODHA YA VIFUPISHO ---------------------------V A. UTANGULIZI ---------------------------------1 B. DIRA NA DHIMA -----------------------------7 C. MUUNDO NA MAJUKUMU YA WIZARA--7 D. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024 -------------------------9 E. MWENENDO WA BAJETI NA FEDHA ZILIZOPOKELEWA NA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024-------- 14 (i) Makusanyo ya Maduhuli------------------- 14 (ii) Bajeti Iliyoidhinishwa----------------------- 14 (iii) Fedha zilizopokelewa na Wizara na Taasisi ------------------------------------------------- 15 F. UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU KWA KUZINGATIA VIPAUMBELE-------------- 16 (a) Kuratibu Mchakato wa Katiba Mpya----- 16 (b) Kuratibu na kusimamia masuala ya upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi kote nchini ------ 17 ii (c) Kusimamia Mfumo wa Haki na Utoaji Haki ------------------------------------------------- 23 (d) Kufanya marekebisho ya Sheria za Uchaguzi na Demokrasia ------------------ 24 (e) Kuwasilisha taarifa kwenye vikao na majukwaa ya Haki za Binadamu na Watu katika ngazi ya Kikanda na Kimataifa --- 25 (f) Kutekeleza Programu ya Kutumia Lugha ya Kiswahili katika utoaji Haki Nchini ------ 27 (g) Kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mikataba mitatu ya Haki za Binadamu ambayo Serikali imeridhia----------------- 27 (h) Kuendelea kuimarisha mifumo ya utoaji haki ili haki ipatikane kwa wote na kwa wakati ----------------------------------------- 33 (i) Kuimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala kwa kuanzisha na kuendesha Kituo cha Kimataifa cha Utatuzi wa Migogoro---------------------------------- 36 (j) Kuimarisha Mfumo wa Elimu ya Sheria- 37 (k) Kuratibu mapitio na marekebisho ya sheria ------------------------------------------------- 43 (l) Kuandaa Sera Mahsusi Zinazosimamia Mifumo ya Utoaji Haki --------------------- 46 (m) Kuendelea Kuimarisha Mfumo wa Uangalizi wa Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi ----- 47 iii (n) Kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za sheria nchini ------ 49 (o) Kuendelea na Utekelezaji wa Mkakati wa Pili wa Taifa wa Haki Mtoto 2020/2021- 2024/2025 ----------------------------------- 51 (p) Kutoa Elimu kwa Umma kuhusu majukumu ya Tume na Kamati za Maadili ya Maafisa Mahakama ngazi ya Mikoa na Wilaya----------------------------------------- 52 (q) Kufanya Tafsiri, Uandishi, Uhakiki wa Mikataba na Urekebu wa sheria---------- 53 (r) Kuendesha Mashtaka ya Jinai ------------ 57 (s) Uratibu na Usimamizi wa Shughuli za Upelelezi wa Makosa ya Jinai ------------- 60 (t) Kushughulikia Urejeshwaji wa Wahalifu na Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Makosa ya Jinai ------------------- 62 (u) Kuwaachilia Huru Wagonjwa wa Afya ya akili walio chini ya uangalizi wa Taasisi ya Afya ya Akili Isanga ------------------------- 62 (v) Kuimarisha Utekelezaji wa Programu ya Kutenganisha Shughuli za Mashtaka na Upelelezi -------------------------------------- 63 Kushughulikia Uendeshaji wa Mashauri ya Madai na Usuluhishi ----------------------- 64 iv (w) Kuratibu Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu, Usimamizi wa Ufilisi na Udhamini ------------------------------------- 67 (x) Utekelezaji wa Masuala ya Kisheria katika ngazi ya Kikanda na Kimataifa ----------- 70 (y) Ujenzi wa Majengo ya Ofisi ---------------- 75 (z) Kuimarisha Mfumo wa Kisheria na Kiutendaji ili kuchangia Mapambano Dhidi ya Rushwa ----------------------------------- 76 (aa) Kuboresha Utendaji na Maendeleo ya Rasilimaliwatu iliyo chini ya Wizara ----- 78 G. CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA NA MIKAKATI YA KUKABILIANA NAZO ---- 84 H. MPANGO NA BAJETI YA WIZARA NA TAASISI ZAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 --------------------------------- 86 v Orodha ya Vifupisho AZAKI Asasi za Kiraia BSAAT Building Sustainable Anti-Corruption Action in Tanzania (Mradi wa Kujenga Uwezo Uendelevu wa Kupambana na Rushwa Tanzania) DHIS2 District Health Information Software Version 2 EAC East African Community (Jumuiya ya Afrika Mashariki) ESAAMLG Eastern and Southern Africa AntiMoney Laundering Group (Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Kudhibiti Fedha Haramu) FATF Financial Action Task Force (Umoja wa Kudhiti Fedha Haramu Duniani) GoTHoMIS Government of Tanzania Health Operation Management Information System GovESB Government Enterprise Service Bus (Basi Mtandao la Serikali) IJA Institute of Judicial Administration (Chuo cha Uongozi wa Mahakama) vi IRLI Irish Rule of Law International LRMIS Law Reform Management Information System LST Law School of Tanzania (Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendendo) NHIF National Health Insurance Fund (Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya) OAGMIS Office of Attorney General Management Information System OTM Ofisi ya Taifa ya Mashtaka PPRA Public Procurement Regulatory Authority (Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma) RITA Registration, Insolvency and Trusteeship Agency (Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini) SADC Southern African Development Community (Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika) TAKUKURU Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa vii TCRA Tanzania Communications Regulatory Authority (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania) TEHAMA Teknolojia ya Habari na Mawasiliano THBUB Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora TTS Transcription and Translation System (Mfumo wa Unukuzi na Tafsiri) UNAFRI United Nations African Institute for the Prevention of Crime and the Treatment of Offenders UNCAC United Nations Convention Against Corruption (Mkataba wa Kimataifa wa Kupambana na Rushwa) UNICEF United Nations International Children's Emergency Fund () UPR Universal Periodic Review (Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu wa Mapitio Katika Kipindi Maalum) viii 1 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa zilizowasilishwa leo katika Bunge lako na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti zilizochambua Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria na Mfuko wa Mahakama, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako sasa likubali kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya utekelezaji wa kazi kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024, Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Katiba na Sheria na taasisi zilizochini ya Wizara pamoja na Mahakama ya Tanzania kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025. 2. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa fadhili zake ikiwemo kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana hapa leo kwa ajili ya kujadili taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Mwelekeo wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025. 3. Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima naomba kutumia fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini na kuniteua kuiongoza Wizara ya Katiba na Sheria. Ninaahidi kuitumikia nafasi hii kwa uaminifu na uadilifu ili kuwaletea maendeleo wananchi na Taifa kwa ujumla. 2 Pongezi 4. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa umahiri wake anaouonesha katika kuiongoza nchi yetu. Aidha, katika kipindi cha uongozi wake, tunashuhudia maendeleo na mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Sheria, ambapo tumeshuhudia kuimarika kwa mfumo wa utoaji haki, huduma za msaada wa kisheria, kukuza na kulinda haki za binadamu na watu pamoja na misingi ya utawala bora. Naomba niungane na Waheshimiwa Wabunge na Wananchi wenzangu kuendelea kumuombea Rais wetu kwa Mwenyezi Mungu amjaalie kila la kheri katika kuliongoza Taifa letu la Tanzania. 5. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii pia kutoa pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi; na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko (Mb), Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati kwa uongozi wao mahiri katika kulitumikia Taifa letu. 3 6. Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwasilisha hotuba ambayo imefafanua utendaji wa Serikali kwa mwaka 2023/2024 na kutoa mwelekeo wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025. Aidha, nawapongeza Mawaziri wote waliowasilisha hotuba za Wizara wanazozisimamia kwa mawasilisho yao mazuri. 7. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie nafasi hii kukupongeza wewe binafsi pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuliongoza Bunge kwa umahiri na weledi mkubwa. Aidha, kwa namna ya pekee naomba kutumia nafasi hii kukupongeza Mheshimiwa Spika kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani. 8. Mheshimiwa Spika, naomba kutumia fursa hii kuwapongeza Mawaziri walioteuliwa na Mheshimiwa Rais kutekeleza majukumu katika Wizara mbalimbali katika kipindi cha kuanzia Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 ambao ni- Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji; Mhe. Jerry William Silaa (Mb), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). 4 Vilevile, nichukue nafasi hii kumpongeza Mhe. Jumanne Abdallah Sagini (Mb), kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria; Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mhe. Zainab Athumani Katimba (Mb), Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI. Ninawatakia kila la heri viongozi wote walioteuliwa katika utekelezaji wa majukumu yao mapya. Salamu za Pole 9. Mheshimiwa Spika, Wizara imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mhe. Ali Hassan Mwinyi, aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu wa Zanzibar na Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naungana na Waheshimiwa wabunge wenzangu kutoa salamu za pole kwa familia za marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na watanzania wote. Aidha, Wizara inawapa pole wananchi wa jimbo la Mbarali kwa kifo cha Mhe. Francis Leonard Mtega, aliyekuwa Mbunge wao. Vilevile, Wizara inawapa pole wananachi wa jimbo la Kwahani, Zanzibar kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wao Mhe. Ahmed Yahya Abdulwakil. Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi, AMINA. 10. Mheshimiwa Spika, nchi yetu kwa nyakati tofauti imekumbwa na ajali na maafa katika maeneo mbalimbali yaliyosababisha vifo, majeruhi, 5 uharibifu wa mali na mazingira. Itakumbukwa pia mnamo tarehe 3 Desemba, 2023 kulitokea maafa ya maporomoko ya matope katika mji wa Katesh mkoani Manyara, yaliyosababisha athari kubwa kwa wananchi ikiwemo vifo kwa baadhi ya Wananchi wenzetu, athari katika makazi, mali na rasimali nyingine. Kwa namna ya pekee natoa pole kwa waathirika wa maporomoko hayo. Aidha, naomba kutoa pole kwa waathirika na manusura wote wa matukio yote yaliyotokea nchini katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2023/2024. Shukrani 11. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kuwashukuru Viongozi wenzangu wa Wizara ya Katiba na Sheria akiwemo Mhe. Jumanne Abdallah Sagini (Mb.), Naibu Waziri wa Katiba na Sheria; Bi. Mary Gasper Makondo, Katibu Mkuu; na Dkt. Khatibu Malimi Kazungu, Naibu Katibu Mkuu kwa ushirikiano wanaonipatia katika utekelezaji wa shughuli za Wizara. 12. Mheshimiwa Spika, aidha, napenda kumshukuru Mhe. Prof. Ibrahimu Hamisi Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama; Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (Mb.), Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Mhe. Mustapher Mohamed Siyani, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania; Prof. Elisante Ole Gabriel, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Katibu wa Tume ya Utumishi wa 6 Mahakama; na Mhe. Eva Kiaki Nkya, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. 13. Mheshimiwa Spika, sambamba na hao, napenda pia kuwashukuru Wakuu na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Wizara wakiwemo Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Prof. Paul Faustin Kihwelo, Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto; Prof. Sist Mramba, Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania; Mhe. Balozi Prof. Kennedy Godfrey Gastorn, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Bw. Sylvester Anthony Mwakitalu, Mkurugenzi wa Mashtaka; Dkt. Boniphace Nalija Luhende, Wakili Mkuu wa Serikali; Bw. Frank Kanyusi Frank, Kabidhi Wasii Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini; Bi. Irene Lesulie, Naibu Kabidhi Wasii Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini; Bw. George Nathaniel Mandepo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania; Mhe. Jaji Mstaafu Mathew P. Mwaimu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora; Bw. Mohamed Khamis Hamad, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora; na Bw. Patience Kilanga Ntwina, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. 14. Mheshimiwa Spika, naomba kuwashukuru Wakurugenzi na Watumishi wote wa Wizara na Taasisi zake. Aidha, kwa namna ya pekee, 7 naishukuru familia yangu kwa ushirikiano wanaoendelea kunipatia kwa kunivumilia na kunitia moyo wakati ninapokuwa natekeleza majukumu yangu ya kulitumikia Taifa. Pia, naomba nichukue fursa hii kwa namna ya kipekee kabisa kuwashukuru wadau wote wa wizara kwa ushirikiano wanaotupatia katika utekelezaji wa majukumu ambayo Wizara imekasimiwa na Serikali. 15. Mheshimiwa Spika, mwisho ila siyo kwa umuhimu, naomba kuwashukuru wananchi wa Mkoa wa Njombe, kwa ushirikiano wanaoendelea kunipa katika kuwawakilisha na kuwatumikia katika Bunge hili Tukufu pamoja na kuratibu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo katika Mkoa wa Njombe. B. DIRA NA DHIMA 16. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Katiba na Sheria inaongozwa na Dira ambayo ni “Katiba na Sheria wezeshi kwa maendeleo ya Taifa”. Aidha, Dhima ya Wizara ni “kuwa na mfumo madhubuti wa kikatiba na kisheria wenye kufanikisha utekelezaji wa sera na mipango kwa maendeleo ya Taifa”. C. MUUNDO NA MAJUKUMU YA WIZARA 17. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Katiba na Sheria inajumuisha Mhimili wa Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, 8 Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA). Taasisi nyingine ni Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. 18. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Hati Idhini iliyotolewa kupitia Tangazo la Serikali Na. 534/2021 majukumu ya Wizara ya Katiba na Sheria ni: - (i) Kutunga sera zinazohusu masuala ya kisheria na kusimamia utekelezaji wake; (ii) Kushughulikia masuala ya kikatiba; (iii) Kusimamia mfumo wa haki na utoaji haki; (iv) Uandishi wa sheria; (v) Kuendesha mashtaka ya jinai; (vi) Kushughulikia uendeshaji wa mashauri ya madai na usuluhishi; (vii) Usuluhishi wa migogoro ya kibiashara, sheria za kimataifa na mikataba; (viii) Kuratibu masuala ya haki za binadamu na utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria; 9 (ix) Kuratibu usajili wa matukio muhimu ya binadamu, ufilisi na udhamini; (x) Kuratibu tathmini na maboresho ya sheria; (xi) Kuratibu ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa sheria za utajiri asili na maliasilia za nchi; (xii) Kushughulikia urejeshwaji wa wahalifu na masuala ya ushirikiano wa kimataifa kwenye makosa ya jinai; (xiii)Kuboresha utendaji na maendeleo ya rasilimali watu iliyo chini ya Wizara; na (xiv) Kuratibu majukumu ya taasisi, mipango na miradi chini ya Wizara. D. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024 19. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2023/2024 umezingatia Dira na miongozo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambayo ni pamoja na; Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (2030); Mpango wa Maendeleo wa Afrika (2063); Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025; Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/2022-2025/2026); Ilani ya Uchaguzi 10 ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2020; Ahadi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizozitoa wakati akifungua Bunge la 11 mwaka 2021; maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Serikali pamoja na Mipango Mikakati ya Wizara na taasisi zake wa mwaka 2021/2022-2025/2026. 20. Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2023/2024, Wizara ilibainisha masuala ya kipaumbele kama ifuatavyo: (i) Kuratibu Mchakato wa Katiba Mpya; (ii) Kutekeleza Mkakati wa Kutoa Elimu ya Katiba kwa umma; (iii) Kutekeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) kwa wananchi kote nchini; (iv) Kufanya marekebisho ya Sheria za Uchaguzi na Demokrasia; (v) Kuwasilisha taarifa kwenye vikao 16 na majukwaa ya Haki za Binadamu na Watu katika ngazi ya Kikanda na Kimataifa; (vi) Kutekeleza Programu ya Kutumia Lugha ya Kiswahili katika utoaji Haki Nchini; (vii) Kuwasilisha taarifa tatu (3) za nchi kuhusu Utekelezaji wa Mikataba mitatu 11 ya Haki za Binadamu ambayo Serikali imeridhia; (viii) Kuendelea kutafsiri Sheria za nchi kutoka lugha ya Kingereza kuwa katika lugha ya Kiswahili; (ix) Kuendelea kuimarisha mifumo ya utoaji haki ili haki ipatikane kwa wote na kwa wakati; (x) Kuimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala kwa kuanzisha na kuendesha Kituo cha Kimataifa cha Utatuzi wa Migogoro; (xi) Kuimarisha mfumo wa elimu ya sheria; (xii) Kuratibu mapitio na marekebisho ya sheria za sekta ya sheria; (xiii) Kuandaa sera mahsusi zinazosimamia mifumo ya utoaji haki; (xiv) Kuendelea kuimarisha mfumo wa uangalizi wa utajiri asili na maliasilia za nchi; (xv) Kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za sheria nchini; (xvi) Kuendelea na ujenzi wa vituo jumuishi vya taasisi za sheria; 12 (xvii) Kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya kikatiba na utawala wa sheria; (xviii) Kuendelea kuhamasisha matumizi ya njia mbadala za utatuzi wa migogoro ambazo ni usuluhishi, upatanishi, maridhiano na majadiliano ili kurahisisha na kuharakisha upatikanaji wa haki nchini; (xix) Kuimarisha mifumo ya kuhamasisha, kuzingatia na kulinda haki za binadamu na watu; (xx) Kuendelea na utekelezaji wa Mkakati wa Pili wa Taifa wa Haki Mtoto 2020/2021- 2024/2025; (xxi) Kuendelea kuimarisha Usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu pamoja na shughuli za ufilisi na udhamini; (xxii) Kutoa Elimu kwa Umma kuhusu majukumu ya Tume na Kamati za Maadili ya Maafisa wa Mahakama ngazi ya Mikoa na Wilaya; (xxiii) Kufanya Tafsiri, Uandishi na Urekebu wa sheria; 13 (xxiv) Kutoa ushauri wa kisheria na kufanya Upekuzi na Marejeo ya Mikataba; (xxv) Kuimarisha uendeshaji mashtaka na usimamizi wa kesi za jinai; (xxvi) Kuimarisha uratibu na usimamizi wa upelelezi wa makosa ya jinai; (xxvii) Kuimarisha mfumo wa utaifishaji mali, usimamizi na urejeshwaji wa mali zinazohusiana na uhalifu; (xxviii)Kuimarisha utekelezaji wa programu ya kutenganisha shughuli za Mashtaka na Upelelezi; (xxix) Kuratibu, kusimamia na Kuiwakilisha Serikali na Taasisi zake katika kuendesha mashauri ya madai na usuluhishi yaliyofunguliwa na au dhidi ya Serikali katika mahakama na mabaraza mbalimbali ndani na nje ya nchi; na (xxx) Kufanya uchunguzi kuhusu masuala ya haki za binadamu na utawala bora. 14 E. MWENENDO WA BAJETI NA FEDHA ZILIZOPOKELEWA NA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024 (i) Makusanyo ya Maduhuli 21. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2023/2024, Wizara pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara ilipanga kukusanya maduhuli ya jumla ya Shilingi 12,676,201,000.00 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo ni pamoja na ada ya watoa huduma za msaada wa kisheria, ada za kusajili mashauri, ada za mawakili na faini zinazotokana na mashauri mbalimbali pamoja na pango la ofisi. Katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 Wizara imekusanya jumla ya Shilingi 7,515,601,174 sawa na asilimia 59.29 ya lengo la makusanyo ya maduhuli kwa mwaka 2023/24 ambayo ni sawa ya asilimia 71.15 ya lengo la kipindi cha miezi kumi kama ilivyoainishwa katika Kiambatisho Na.1. (ii) Bajeti Iliyoidhinishwa 22. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2023/2024, Wizara iliidhinishiwa na Bunge jumla ya Shilingi 383,619,511,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo Shilingi 97,815,618,000.00 ni kwa ajili ya mishahara ya Watumishi, Shilingi 176,148,324,000.00 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na Shilingi 109,655,569,000.00 ni 15 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Kati ya fedha za maendeleo Shilingi 44,112,800,000.00 ni fedha za ndani na Shilingi 65,542,769,000.00 ni fedha za nje (Kiambatisho Na.2). (iii) Fedha zilizopokelewa na Wizara na Taasisi 23. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, Wizara imepokea jumla ya Shilingi 273,632,590,744.49 sawa na asilimia 71.33 ya Shilingi 383,619,511,000.00 zilizoidhinishwa na Bunge katika mwaka 2023/2024. Kati ya fedha zilizopokelewa, Shilingi 75,993,267,798.68 ni kwa ajili ya mishahara, Shilingi 157,498,293,263.99 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na Shilingi 40,141,029,681.52 ni fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Fedha ya miradi ya maendeleo inajumuisha Shilingi 9,712,560,484.37 fedha za ndani na Shilingi 30,428,469,197.15 ni fedha za nje. Muhtasari wa mchanganuo wa Bajeti iliyoidhinishwa na kiasi cha fedha zilizopokelewa na Wizara na Taasisi kwa kipindi hicho zimeainishwa katika Kiambatisho Na. 3a na 3b. 16 F. UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU KWA KUZINGATIA VIPAUMBELE 24. Mheshimiwa Spika, kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/2024, Wizara na Taasisi zake ilibainisha masuala mahsusi ya kipaumbele ambayo yametekelezwa kama ifuatavyo:- (a) Kuratibu Mchakato wa Katiba Mpya 25. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili, 2024, Wizara imeendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya kikatiba na utawala wa sheria kwa umma kupitia vyombo vya habari vikiwemo redio, televisheni, mitandao ya kijamii na tovuti ya Wizara. Aidha, jumla ya wananchi 267,323 wamefikiwa na elimu ya katiba na uraia kwa umma kupitia maadhimisho ya kitaifa ikiwa ni pamoja na Wiki ya Sheria, Wiki ya Msaada wa Sheria, makongamano, warsha, semina na midahalo. Pia, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa elimu imeainisha masula ya kikatiba yanayohitajika kujumuishwa kwenye mitaala ya elimu. 26. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha mfumo wa utoaji elimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge na Uratibu kwa upande wa Tanzania Bara, na Afisi ya Rais - Katiba, Sheria, 17 Utumishi na Utawala Bora na Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeandaa rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Kutoa Elimu ya Katiba na Uraia kwa Umma. Mkakati huo unalenga kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa Katiba ikiwa ni pamoja na kufahamu haki na wajibu wao kwa Taifa na kuwawezesha kushiriki katika mijadala ya kikatiba. Rasimu hiyo itajadiliwa na kufanyiwa uamuzi ndani ya Serikali kabla ya kuanza kutumika. (b) Kuratibu na kusimamia masuala ya upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi kote nchini 27. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha upatikanaji wa elimu ya sheria na huduma za kisheria nchini, Wizara inaendelea na utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign). Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili, 2024, Wizara imefikia Mikoa mitatu (3) ya Ruvuma, Simiyu na Singida na kufanya jumla ya Mikoa Sita (6) ya Dodoma, Manyara, Shinyanga, Ruvuma, Simiyu na Singida kufikiwa tangu Kampeni hii izinduliwe rasmi tarehe 27 Aprili, 2023 na Mheshimiwa Kassimu Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Halmashauri 42, Kata 452 na Vijiji/Mitaa 1,348 imefikiwa. Aidha, jumla ya 18 wananchi 415,597 (Wanaume 216,589 na Wanawake 199,008) wamefikiwa katika ngazi za vijiji na maeneo ya vizuizi. 28. Mheshimiwa Spika, kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, jumla ya wananchi 2,775 (Wanaume 1,258 na Wanawake 1,517) walisajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa kupitia Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini – RITA. Aidha, katika Kampeni hiyo, Wakala ilitoa elimu kwa wananchi 14,156 kuhusu usajili wa vizazi, vifo, ndoa, talaka na umuhimu wa kuandika wosia. 29. Mheshimiwa Spika, kupitia Kampeni hii, migogoro 4,546 iliyohusu ardhi (1,828), ndoa (486), mirathi (393), ukatili wa Kijinsia (393), matunzo ya watoto (518), masuala ya kijinai (168), masuala ya madai (330), migogoro ya ajira (231), migogoro mingine ya kisheria (199) ilipokelewa ambapo kati ya hiyo migogoro 516 ilitatuliwa na kuhitimishwa kwa njia ya usuluhishi na upatanishi. Migogoro 4,030 inaendelea kufanyiwa kazi katika mamlaka mbalimbali za kimahakama na kiutawala. 30. Mheshimiwa spika, Kampeni ya Mama Samia ya Msaada wa Kisheria imesaidia kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu masuala ya kisheria ikiwemo haki na wajibu wao, utatuzi wa migogoro ya ardhi, madai, jinai, masuala ya haki za binadamu na utawala bora, ulinzi wa haki za 19 makundi mbalimbali kama wanawake na watoto na kuimarisha ulinzi na amani miongoni mwa jamii; kuleta utangamano katika familia na tija katika jamii kwa wananchi kushiriki zaidi katika shughuli za kujiongezea kipato katika uzalishaji kwa kupunguza muda mwingi wanaotumia kufuatilia migogoro katika Mahakama. 31. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kupokea maoni kuhusu uimarishwaji wa huduma ya msaada wa kisheria, ikiwa ni pamoja na maoni ya Bodi ya Taifa ya Ushauri wa Msaada wa Kisheria, kuhusu uboreshwaji wa Sheria ya Msaada wa Kisheria, Sura ya 21 na Kanuni zake za Mwaka 2018. Aidha, Wizara imefanyia kazi maoni yaliyotolewa na wadau na Bodi ya Taifa ya Ushauri ya Msaada wa Kisheria. Baadhi ya marekebisho yaliyofanyika kutokana na maoni ya wadau ni kufutwa kwa ada ya usajili kwa Wasaidizi wa Kisheria; na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania kutumia wanafunzi wake kutoa huduma ya msaada wa kisheria katika maeneo wanayokwenda kufanya mazoezi ya uwandani. Aidha, Wizara inaendelea kufanyia kazi maoni na mapendekezo mengine yaliyopo. 32. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha uratibu na ufuatiliaji wa huduma za msaada wa kisheria, Wizara kwa kushirikiana na Wadau wa Msaada wa Kisheria nchini, ilifanya Kongamano la Msaada wa Kisheria la Mwaka 2023 katika Mkoa 20 wa Dodoma. Lengo kuu la kongamano hili lilikuwa ni kuendelea kuwaweka pamoja wadau wa msaada wa kisheria na Serikali na kujadiliana namna bora ya kuimarisha upatikanaji haki kwa wananchi kupitia huduma za msaada wa kisheria nchini. Kongamano hili lilihudhuriwa na washiriki 122 (wanawake 80 na wanaume 42). 33. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki katika Kongamano la Kikanda la Nchi za Asia, Pasifiki na Afrika lililofanyika nchini India. Kongamano hili lilihudhuriwa na Mawaziri wa Sheria, Majaji Wakuu na Maafisa wengine wa Serikali na Taasisi zisizo za kiserikali. Katika kongamano hili, uzoefu ulionesha kwamba baadhi ya nchi zimejikita katika kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa mashauri ya jinai pekee na nyingine zikijikita katika masuala ya madai pekee. Aidha, kwa nchi zenye Mfuko wa Msaada wa Kisheria, uzoefu ulionesha kuwa nchi hizo zina uwezo wa kutanua wigo wa huduma za msaada wa kisheria katika maeneo ya pembezoni. Hivyo, Wizara kwa kushirikiana na wadau inafanya tathmini ili kuona uwezekano wa kuwa na Mfuko wa Msaada wa Kisheria nchini. 34. Mheshimiwa Spika, Wizara ilifanya Kongamano la Mtandao wa Huduma za Msaada wa Kisheria wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kongamano hili lilihudhuriwa na washiriki 50 (Wanaume 17 na Wanawake 33) 21 kutoka nchi za Kenya, Tanzania Bara na Zanzibar, Rwanda, Burundi na Uganda. Kupitia Kongamano hili wajumbe walijadili na kuainisha fursa zilizopo katika upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria katika maeneo yao. 35. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili 2024, Wizara ilishiriki kutoa elimu ya sheria na huduma za msaada wa kisheria wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria, Siku 16 za Kupinga Ukatili na Siku ya Maadili na Haki za Binadamu na maadhimisho ya siku ya wanawake duniani. Kupitia maadhimisho hayo, jumla ya wananchi 406 (Wanaume 260 na wanawake 146) walifikiwa na kupatiwa elimu ya sheria katika masuala ya ardhi, ukatili wa kijinsia, mirathi na wosia, haki na wajibu. Aidha, jumla ya vipeperushi na vijitabu 670 kuhusu masuala ya mirathi, wosia, talaka, ardhi, haki za wanawake na watoto, msaada wa kisheria, na utajili asilia viligawiwa kwa wananchi bure wakati wa maadhimisho hayo. Aidha, wanafunzi 200 wa Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma walijengewa uwezo kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia kwa lengo la kujilinda wao binafsi na kushughulikia masuala hayo katika jamii zinazowazunguka. 36. Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea kujenga uwezo kwa wadau mbalimbali kuhusu masuala ya msaada wa kisheria. Jumla ya wadau 366 kutoka makundi mbalimbali walijengewa 22 uwezo. Makundi hayo yanajumuisha Watendaji wa Halmashauri, Kata, Mitaa na Vijiji 44, Wajasiriamali wanawake 40, Waandishi wa Habari na Wanahabari 28, Wasaidizi wa Kisheria 92, Viongozi wa dini na viongozi wa kimila 74, wajumbe wa Mabaraza ya Kata 48 na Wasajili wasaidizi wa watoa huduma za msaada wa kisheria 40. Mafunzo haya kwa pamoja yalilenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi kupitia wasaidizi wa kisheria na watendaji katika ngazi za kijamii. Aidha, waandishi wa habari na wanahabari walijengewa uwezo kuhusu namna ya kutoa taarifa za masuala ya ukatili wa kijinsia na kufuatilia upatikanaji haki kwa manusura. 37. Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea kuimarisha mfumo wa usajili wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria na Wasaidizi wa kisheria nchini kwa lengo la kuhakikisha huduma za usajili zinaboreshwa, kuwa na takwimu sahihi za wanufaika wa huduma za msaada wa kisheria, kuwa na mfumo thabiti wa taarifa za wadau wanaoshughulika na masuala ya wananchi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma mahali walipo kwa haraka na kwa ufanisi. Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili, 2024, jumla ya Mashirika 99 ya watoa huduma ya msaada wa kisheria na Wasaidizi wa Kisheria 589 walisajiliwa katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara. Idadi hii inafanya kuwa na jumla mashirika 270 na wasaidizi wa kisheria 2,114 waliosajiliwa nchi nzima. 23 (c) Kusimamia Mfumo wa Haki na Utoaji Haki 38. Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha usimamizi wa mifumo na masuala ya usalama na kuwezesha upatikanaji haki, Wizara inafanya mapitio ya Sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa na Mashahidi, Sura ya 446 kwa lengo la kuiboresha ili kuhakikisha ulinzi na usalama wa watoa taarifa na mashahidi. Vilevile, Wizara imefanya tathmnini ya kuanzisha mfuko wa kuwalinda mashahidi na watoa taarifa kwa lengo la kuwa na mfumo bora wa kitaasisi utakaohakikisha ulinzi na usalama wa mashahidi na watoa taarifa. 39. Mheshimiwa Spika, katika kufanya mapitio ya Mfumo wa Haki Jinai, Wizara imechambua taarifa ya Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai Nchini, baada ya uchambuzi huo Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume tajwa umeandaliwa ambao umejumuisha majukumu ya Wizara pamoja na wadau wengine zikiwemo taasisi zilizo chini ya Wizara. Vilevile, Wizara imeandaa Mpango Kazi wa kusimamia utekelezaji wa mapendekezo ya Tume na Mpango Kazi wa Marekebisho ya Sheria ambazo Tume ilipendekeza sheria hizo kufanyiwa marekebisho ili zikidhi matakwa ya utoaji haki. Mipango Kazi hiyo imewasilishwa kwenye Kamati ya Kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya Tume. 24 40. Mheshimiwa Spika, katika wa fedha 2023/2024, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliandaa Miongozo mbalimbali kwa ajili kuboresha utendaji wa Mawakili wa Serikali. Miongozo hiyo ilizinduliwa tarehe 22/5/2024 na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Miongozo hii ni Mwongozo wa Uandishi wa Sheria (Legislative Drafting Manual), Mwongozo wa Utengenezaji wa Sheria Ndogo za Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mwongozo wa Upekuzi na Usimamizi Mikataba (Contract Manual), Mwongozo wa Utoaji wa Ushauri wa Kisheria, Mwongozo wa Kamati za Ushauri za Mikoa na Wilaya, Istilahi za Kisheria na Tafsiri ya Majina ya Sheria Kuu. (d) Kufanya marekebisho ya Sheria za Uchaguzi na Demokrasia 41. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa Kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliwezesha kutungwa kwa Sheria ya Marekebisho Mbalimbali ya Sheria za Sekta (The Legal Sector Laws (Miscellaneous Amendments) Act No. 11 of 2024) ambayo pamoja na masuala mengine ilirekebisha Sheria za zinazogusa masuala ya demokrasia. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge na Uratibu; Ofisi ya Rais - Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar; Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa; na Tume ya Taifa 25 ya Uchaguzi imewezesha kutungwa na kufanya marekebisho ya sheria za uchaguzi na demokrasia ambazo ni: (i) Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani (Na. 1) ya Mwaka 2024; (ii) Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (Na. 2) ya Mwaka 2024; na (iii) Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa (Na. 3) ya Mwaka 2024 (The Political Parties Affairs Laws Amendment Act No. 03 of 2024). (e) Kuwasilisha taarifa kwenye vikao na majukwaa ya Haki za Binadamu na Watu katika ngazi ya Kikanda na Kimataifa 42. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu ushiriki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika vikao na majukwaa ya haki za binadamu na watu ya kikanda na kimataifa ambapo taarifa za jitihada na mafanikio ya Serikali za kulinda na kukuza haki za kiraia, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni ziliwasilishwa katika vikao vifuatavyo:- (i) Kikao cha 53 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika tarehe 19 Juni hadi 14 Julai 2023 Geneva-Uswisi ambapo Serikali 26 iliwasilisha maelezo kuhusu mabadiliko ya tabianchi na haki ya kupata chakula kwa kueleza mifumo na sera zilizopo katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ya Mwaka 2030; (ii) Kikao cha 54 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika tarehe 11 Septemba hadi 13 Oktoba, 2023 Geneva-Uswisi ambapo Serikali iliwasilisha maelezo kuhusu namna inavyotekeleza haki ya maji safi na salama, haki za wazee, namna inavyosimamia kemikali hatarishi, haki ya maendeleo, na kujumujisha masuala ya jinsia katika kazi zote za Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwa kuwa na Sera, Sheria, mikakati, Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025 kwa lengo la kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ya Mwaka 2030; na (iii) Kikao cha 55 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika kuanzia tarehe 24 Machi hadi 6 Aprili, 2024 Geneva Uswisi na Serikali ilieleza namna ambavyo inalinda, inahifadhi na kukuza haki za binadamu kuhusu watu wenye ulemavu wakiwemo watu wenye ualbino, uhuru wa kushirikiana, haki ya 27 kuishi katika mazingira safi na salama na suala la mabadiliko ya tabia nchi. (f) Kutekeleza Programu ya Kutumia Lugha ya Kiswahili katika utoaji Haki Nchini 43. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inaendelea na uhakiki wa sheria zilizokamilika na kutafsiriwa kwa mara ya kwanza ambapo jumla ya Sheria Kuu 258 zimekamilika tafsiri ya awali. Hivyo, Mpango kazi umeandaliwa kwa ajili ya kuzifanyia uhakiki na kuzitangaza Sheria hizo ili zianze kutumika. Aidha, zipo Sheria 46 ambazo zimetafsiriwa na tafsiri yake imetumia lugha ya kitaalam zaidi (mfano Sheria ya Famasi Sura ya 311). Hivyo, Wizara ya Katiba na Sheria inaendelea kushirikiana na Wizara za Kisekta ili sheria hizo zitafsiriwe kwa Kiswahili sanifu. (g) Kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mikataba mitatu ya Haki za Binadamu ambayo Serikali imeridhia 44. Mheshimiwa Spika, Wizara imeandaa rasimu ya taarifa ya Nchi kuhusu Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu wa Mwaka 2006, Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu wa Mwaka 1981 na Itifaki ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu 28 kuhusu Haki za Wanawake wa Afrika wa Mwaka 2003. 45. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoa elimu kwa wadau na wananchi kuhusu haki za binadamu kwa lengo la kujua haki, uhuru na wajibu wao kwa mujibu wa Sheria za kitaifa, kikanda na kimataifa. Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili 2024, elimu imetolewa kama ifuatavyo:- (i) Wizara iliandaa Kikao Kazi kuhusu Mfumo wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kilichofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 20 Julai, 2023 mkoani Morogoro ili kuwajengea uwezo wadau 49 kutoka katika Wizara na Idara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Washiriki walijengewa uwezo katika masuala ya haki za binadamu ikiwemo uaandaji na uwasilishaji wa taarifa za nchi za utekelezaji wa mikataba na itifaki ambazo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeridhia. (ii) Wizara ilishiriki katika Maonesho ya Kitaifa ya Siku ya Wakulima Nanenane kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti, 2023 mkoani Mbeya ambapo ilitoa elimu kwa washiriki 221 (Wanawake walikuwa 122 na Wanaume 99) kuhusu haki za binadamu na wajibu wa jamii kwa mujibu wa Ibara ya 12 hadi 30 ya Katiba 29 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 pamoja na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa iliyoridhiwa na Serikali na haki hizo kuwepo kwenye Katiba na Sheria za Tanzania. (iii) Wizara ilishiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa yaliyofanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 05 hadi10 Desemba, 2023. Maadhimisho hayo yalifanyika kuanzia tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2023 ambapo wananchi 113 (Wanaume 77, Wanawake, 24 na Watoto 12) walipatiwa elimu kuhusu haki za binadamu na watu, unyanyasaji wa kijinsia, migogoro ya ardhi, migogoro ya ndoa na masuala ya mirathi. (iv) Wizara ilitoa elimu kuhusu haki za binadamu kwa umma kwa jumla ya wananchi 107 (Wanawake 68 na Wanaume 39) katika Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 11 Machi, 2024 mkoani Dodoma. 46. Mheshimiwa Spika, katika kusimamia hifadhi ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora nchini, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeendelea kupokea na kushughulikia malalamiko yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora. Katika kipindi cha Julai, 2023 hadi 30 Aprili, 2024 THBUB ilikuwa inachunguza jumla ya malalamiko 964, katika kipindi hicho malalamiko 141 yalifungwa. Aidha, malalamiko 823 yanayoendelea na uchunguzi ambapo kati ya hayo malalamiko 336 yanahusu uvunjwaji wa haki za binadamu, malalamiko 450 yanahusu ukiukwaji wa misingi ya utawala bora na malalamiko 37 yanahusu makundi maalum. 47. Mheshimiwa Spika, Wizara kupita THBUB imeendelea kutoa Elimu kwa Umma kuhusu masuala ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora. Jumla ya vipeperushi 3,110 vilitolewa kwa wananchi waliotembelea katika Ofisi za Tume, maadhimisho ya Wiki ya Wakulima, Wiki ya Sheria na Semina za Viongozi wa Vilabu vya haki za binadamu. Aidha, vipindi 21 viliandaliwa na kurushwa hewani kupitia redio na televisheni. Pia, matamko manne (4) kuhusu haki za binadamu yalitolewa, matamko hayo yalihusu:- (i) Usafirishaji haramu wa binadamu duniani, tamko hilo lilitolewa tarehe 30 Julai, 2023 wakati wa Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu usafirishaji haramu wa binadamu duniani; (ii) Kutambua mchango wa wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo, tamko hilo lilitolewa tarehe 31 Julai, 2023 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke wa Afrika; 31 (iii) Viashiria vya uvunjifu wa amani na umoja wa kitaifa wakati wa mjadala kuhusu uwekezaji wa Kampuni ya DP World nchini; na (iv) Watu wenye ulemavu na masuala ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora, tamko hilo lilitolewa tarehe 03 Desemba, 2023 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu. 48. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/2024, Wizara kupitia THBUB ilifanya kikao kazi pamoja na wadau 53 kutoka Asasi za Kiraia (AZAKI) na taasisi za Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar. Lengo la kikao hicho lilikuwa kupata maoni kuhusu utekelezaji wa Itifaki ya Maputo pamoja na kuangalia jinsi Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali nchini ilivyoangaza utekelezaji wa Itifaki ya Maputo ya mwaka 2003. Majadiliano kuhusu Itifaki hiyo yalijikita katika hoja ya iwapo kuna hajaya nchi yetu kuwa na Sheria Mahsusi inayohusu itifaki hii, ambayo nchi iliiridhia mwaka 2007 au sheria zilizopo zinajitosheleza. Tume inaendelea na uchambuzi ili ishauri ipasavyo kuhusu suala hili. 49. Mheshimiwa Spika, Tume kwa kushirikiana na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Kanda ya Afrika 32 Mashariki, ilifanya semina moja (1) ya mafunzo ya haki za binadamu kwa viongozi wa vilabu vya haki za binadamu na walezi wake kutoka vyuo vikuu na vyuo vya kati ambapo jumla washiriki 70 walijengewa uwezo kuhusu masuala ya haki za binadamu na wajibu. 50. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia THBUB ilifanya makongamano mawili (2) kwa kushirikiana na Taasisi za elimu na wadau wa Haki za Binadamu ikiwemo Chuo Kikuu cha Iringa ambapo jumla ya wanachuo 300 na wakufunzi watatu (3) walishiriki. Kupitia makongamano hayo, wanachama wapya 178 walijiunga na Klabu ya Haki ya Binadamu na Utawala bora. Aidha, kongamano la pili lilifanyika na Wadau wa Haki za Binadamu katika kuadhimisha Miaka 75 ya Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu. Kupitia Kongamano hilo, jumla ya washiriki 105, walijengewa uelewa katika masuala mbalimbali ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora. 51. Mheshimiwa Spika, katika kipindi husika, Wizara kupitia THBUB, ilifanya ufuatiliaji wa ufanisi wa taratibu za kushughulikia malalamiko katika taasisi za Serikali za utoaji haki zisizo za kimahakama katika Mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Mwanza na Unguja. Taasisi zilizotembelewa ni pamoja na Ofisi ya Kazi Mkoa, Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Baraza la Taifa la Usimamizi wa 33 Mazingira, Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania na Mifuko ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii. Kupitia tathimini hiyo, Tume iligundua kuwa taasisi za Serikali za utoaji haki zisizo za kimahakama zinakabiliwa na uhaba wa rasilimaliwatu na fedha, wananchi kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya huduma na majukumu ya taasisi hizo, na baadhi ya taasisi kuwa na Ofisi katika ngazi za mikoa tu. Tume ilizishauri taasisi hizo kubainisha mahitaji na kuwasilisha katika mamlaka husika maombi ya kuongezewa rasilimaliwatu na fedha ili ziwe na ufanisi katika kuhudumia wananchi. (h) Kuendelea kuimarisha mifumo ya utoaji haki ili haki ipatikane kwa wote na kwa wakati (i) Usikilizaji wa Mashauri 52. Mheshimiwa Spika, suala la kupunguza mlundikano wa mashauri mahakamani ni moja ya vipaumbele muhimu vya Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata haki sawa na kwa wakati. Kwa kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 kulikuwa na jumla ya mashauri 196,592 mahakamani; kati ya hayo 52,056 ni mashauri yaliyokuwepo mwanzoni mwa Julai, 2023 na mashauri 144,536 yalifunguliwa. Kati ya mashauri 196,592 yaliyokuwepo, mashauri 133,823 yalisikilizwa na kuhitimishwa na mashauri 62,769 yanaendelea katika hatua mbalimbali. Aidha, mashauri yenye umri mrefu 34 Mahakamani ni 2,087 sawa na asilimia 3 ya mashauri yote yaliyobaki Mahakamani. Aidha, katika mashauri yaliyopo Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani umri mrefu ni miaka miwili (2); Mahakama za Hakimu Mkazi na Wilaya umri mrefu ni mwaka mmoja (1); Mahakama za Mwanzo umri mrefu ni miezi sita (6). (ii) Kuendelea Kutekeleza Mpango wa Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Mahakama katika Ngazi Mbalimbali 53. Mheshimiwa Spika, Mahakama ya Tanzania imeendelea na utekelezaji wa Mpango wa Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Mahakama wa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026). Hadi kufikia Aprili 2024, Miradi iliyokamilika ni Mahakama za Wilaya ya Ulanga, Kwimba na Liwale; Ukarabati wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Maswa: Ujenzi wa Majengo ya Mahakama za Mwanzo Usevya (Mlele), Nyakibimbili (Bukoba), Mahenge (Kilolo), Newala Mjini (Newala), Madale (DSM), Kinesi (Rorya) na Luilo (Ludewa). 54. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024 hadi kufikia Aprili, 2024 hali ya ujenzi na ukarabati wa majengo mbalimbali ya Mahakama ni kama ifuatavyo: (i) Ujenzi wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki sita (6) ambavyo ni Katavi Songea (Ruvuma), 35 Songwe Njombe, Simiyu na Geita; (ii) Ujenzi wa majengo ya Mahakama za Mwanzo tatu (3) ambazo ni Mahakama ya Mwanzo: Ilangala (Ukerewe), Mbalizi (Mbeya) na Machame (Kilimanjaro); (iii) Kuendelea kwa ujenzi wa majengo ya Mahakama za Wilaya sita (6) ambazo ni Mahakama ya Wilaya; Kibiti (Pwani), Nachingwea (Lindi), Simanjiro (Manyara), Hanang (Manyara), Mbulu (Manyara) na Tunduru (Ruvuma); (iv) Ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Korogwe ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 61: (v) Ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Wilaya Ubungo ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 98; (vi) Ukarabati wa jengo la zamani la Mahakama Kuu Dodoma ambapo ukarabati umefikia asilimia 49; (vii) Ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama ambapo hadi sasa umefikia asilimia 97.3; (viii) Ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo KabangaNgara unaendelea na upo asilimia 97 katika hatua ya ukamilishaji (finishing stage); (ix) Ujenzi wa nyumba 48 za Majaji eneo la 36 Iyumbu Dodoma ambapo ujenzi umefikia asilimia 98 kwa Majengo yote; na (x) Kuendelea kwa ujenzi wa nyumba ya Jaji Mkuu, jijini Dodoma ambapo ujenzi umefikia asilimia 53. (iii) Mifumo ya TEHAMA katika Huduma za Mahakama 55. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/2024 maboresho ya mifumo ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za Mahakama yameendelea kwa lengo la kuimarisha upatikanaji haki kwa wananchi. Hadi kufikia Aprili, 2024 Mfumo wa Usimamizi wa Mashauri umeboreshwa. Mifumo ya e-project management, e-library, ewakili, e-court broker, process server na Judicial portal imefuatiliwa na kufanyiwa maboresho. Aidha, matumizi ya TEHAMA yameimarika katika utoaji haki ikiwemo matumizi ya Mfumo wa Unukuzi na Tafsiri (Transcription and Translation System-TTS); e-case management; na virtual conference. (i) Kuimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala kwa kuanzisha na kuendesha Kituo cha Kimataifa cha Utatuzi wa Migogoro 56. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/2024, Serikali imesajili jumla ya watoa huduma 46 walioomba kuthibitishwa kama Watoa 37 Huduma za Utatuzi wa Migogoro kwa njia mbadala, ambapo Waendesha Maridhiano 3, Watoa Huduma za Majadiliano 3, Wapatanishi 13 na Wasuluhishi 27. Hivyo, hadi aprili, 2024 wapo Watatuzi wa Migogoro kwa Njia Mbadala 576, kati ya hao, Waendesha Maridhiano 38, Watoa Huduma za Majadiliano 60, Wapatanishi 185 na Wasuluhishi 293. 57. Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na taratibu za kuanzisha Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi Tanzania (Tanzania International Arbitration Centre), hadi kufikia Aprili, 2024 Andiko la Kuanzisha Kituo hicho limeandaliwa ikiwa ni pamoja na kuainisha mapendekezo ya muundo wa taasisi; gharama za kuanzisha na kuendesha taasisi; mifumo ya ushirikiano na taasisi nyingine zinazohusiana na masuala ya usuluhishi Tanzania. Taasisi hiyo itakuwa na Kituo Dar es Salaam ambapo tayari jengo kwa ajili ya kuanzisha Kituo hicho limepatikana. (j) Kuimarisha Mfumo wa Elimu ya Sheria Taasisi ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania 58. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 Taasisi Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School of Tanzania – LST) ilisajili jumla ya wanafunzi 1,242 sawa na asilimia 82.8 ya lengo la udahili wa wanafunzi 1,500 kwa kundi la 37 na 38. Aidha, katika kipindi 38 husika, Taasisi imetoa wahitimu 272 wanaostahili kusajiliwa kuwa Mawakili na kufanya idadi ya wahitimu waliopata mafunzo kupitia Taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007 kufikia 8,717. Vilevile, Taasisi ilipata ithibati kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi na kuanzisha programu ya mafunzo ya watoa huduma ya msaada wa kisheria ngazi ya cheti. Aidha, wahitimu 15 waliofanya mitihani ya Astashahada ya Wasaidizi wa Sheria walifaulu na kutunukiwa Astashahada ya Wasaidizi wa Sheria. 59. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kupitia Wasajili Wasaidizi wa Msaada wa Kisheria imetoa huduma ya msaada wa kisheria kwa watu 7,270 wakiwemo wanaume 3,810 na wanawake 3,460 sawa na asilimia 52.41 na asilimia 47.59 mtawalia. Katika idadi hiyo, watu wazima walikuwa 7,071 (97.26%) na watoto walikuwa 199 (2.74%). Maeneo yaliyopatiwa msaada wa Kisheria ni Migogoro ya ndoa 1,694, ardhi 1,663, Madai 1,621, Mirathi 796, Jinai 683, Masuala ya Biashara 241 na Migogoro mingine mchanganyiko 572. Aidha, Taasisi itaendelea kuboresha na kuimarisha usimamizi wa wanafunzi wakati wa mafunzo uwandani ili wananchi wengi hususan katika maeneo ya pembezoni waweze kupata msaada wa kisheria. 39 Mheshimiwa Spika, kupitia Kituo cha Msaada wa Kisheria cha Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo Tanzania, wananchi 195 (Wanawake 81 na Wanaume 114) wamepatiwa msaada wa kisheria na elimu ya sheria imetolewa kwa wadau 700 wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. LST kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania imefanya mapitio ya mtaala wa mafunzo ya uanasheria kwa vitendo ambao utaanza kutumika rasmi Julai, 2024. Mapitio hayo yana lengo la kuimarisha utoaji wa mafunzo na kuwajengea wanafunzi umahiri kulingana na mahitaji ya sasa ya soko. Mapitio hayo yamefanyika kwa dhana ya mabadiliko kwa kuzingatia maendeleo katika jamii. Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto 60. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (Institute of Judicial Administration – IJA) kimedahili jumla ya wanafunzi 958 wa Astashahada na Stashahada ya Sheria ambayo ni sawa na 73.7% ya lengo la udahili wa wanafunzi 1,300. Aidha, katika kipindi hicho jumla ya wanafunzi 608 walihitimu mafunzo ya ngazi ya Astahashada na Stashahada ya Sheria. 61. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha watumishi wa Mahakama na watumishi wengine wa Sekta ya Sheria wanakuwa na ujuzi na weledi wa kutosha katika kutimiza wajibu wao wa utoaji 40 haki kwa ufanisi, Wizara kupitia Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (Institute of Judicial Administration – IJA) imeendelea kutoa mafunzo endelevu na elekezi kwa watumishi wa Mahakama na wadau wa Sekta ya Sheria nchini. Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili, 2024, Chuo kimeendelea kutekeleza jukumu lake la kuratibu mafunzo elekezi kwa Majaji wapya saba (7) wa Mahakama ya Rufani na 20 wa Mahakama Kuu pamoja Mahakimu wapya 39 kupitia Mahakama ya Tanzania. 62. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/2024, IJA imeratibu mafunzo endelevu kwa maafisa 274 wa Mahakama yakiwemo ya kubadilishana uzoefu juu ya uhalifu wa mtandaoni pamoja na uhalifu wa kifedha; mafunzo ya utekelezaji wa amri za fidia, faini na gharama katika mashauri ya jinai kwa Maafisa Mahakama 147; mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika kushughulikia mashauri ya ndoa kwa Maafisa Mahakama 104; mafunzo ya namna ya kushughulikia utekelezaji wa wosia na usimamizi wa mirathi kwa Maafisa Mahakama 104; mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika kushughulikia mashauri ya uchaguzi kwa Maafisa Mahakama 132; mafunzo ya programu ya ushauri maalum wa kitaaluma kwa Maafisa Mahakama 40; Mafunzo ya wakufunzi ya namna ya kuepusha kurejesha majeraha ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto kwa Maafisa Mahakama 11 na mafunzo kwa njia ya mtandao kwa 41 Mahakimu 100 wenye mamlaka ya ziada; na mfumo wa usimamizi wa mashauri na ujuzi wa uongozi kwa Maafisa Mahakama 398. 63. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/2024, IJA imetoa mafunzo mbalimbali kwa wadau wa mnyororo wa utoaji haki yakiwemo ya Madalali na Wasambaza Nyaraka za Mahakama 70; maandalizi na matumizi ya jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao kwa Watumishi 37 wa Mahakama; mafunzo ya namna bora ya kushughulikia mashauri ya wanyamapori na makosa yanayofanana na hayo kwa Mahakimu, Wapelelezi na Waendesha Mashtaka 331; mafunzo ya kuandaa, kutengeneza na kutumia maudhui ya kwenye mtandao kwa ajili ya kufundishia na kujifunza kwa Watumishi 19 wa Mahakama; mafunzo ya namna bora ya kushughulikia mashauri ya watoto kwa Makarani 27 wa Mahakama; na mafunzo ya ujuzi wa kompyuta (computer literacy) na stadi za msingi/awali za kidigiti (Basic Digital Skills) kwa Waandishi Waendesha Ofisi na Wasaidizi wa Kumbukumbu 1,785. 42 64. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/2024, IJA ilishiriki katika matukio mbalimbali kitaifa, kikanda na kimataifa ikiwemo; kikao cha 6 cha Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu juu ya majadiliano kuhusu haki za binadamu kilichofanyika nchini Algeria; mdahalo wa makosa ya uhalifu wa Kupangwa wa Kimataifa Unaovuka Mipaka, uliofanyika Jijini Dodoma; kikao cha majadiliano juu ya Masuala ya Rushwa na Uhuru wa Mahakama yaliyofanyika katika Jiji la Prague nchini Czech; Kongamano la Majaji wa eneo la Bahari ya Hindi kuhusu Uhalifu wa Baharini nchini Shelisheli (Sychelles); Mafunzo ya mtandao juu ya Sheria ya Wakimbizi ambayo yaliandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Kimahakama (JIFA). Pia, IJA iliandaa Kongamano (Symposium) la Maafisa wa Mahakama na wadau wengine lililohusu makosa ya uhalifu wa kifedha kwa udhamini wa Programu ya Kitaifa ya Kuzijengea Uwezo Taasisi za Umma zinazohusika na Kupambana na Rushwa Tanzania. 65. Mheshimiwa Spika, moja ya majukumu ya Chuo ya Uongozi wa Mahakama ni kuandaa majarida na machapisho yanayohusiana na Sekta ya Sheria au masuala ya kimahakama. Katika mwaka 2023/2024, IJA iliandika na kuzindua kitabu kinachoitwa Ndoto Iliyotimia: Maisha ya Jaji Robert Habesh Kisanga; na Kitabu cha Mkusanyiko wa Mashauri ya Ukatili wa Kingono kwa Watoto ya Tanzania na Ireland kwa ushirikiano na Taasisi ya 43 Irish Rule of Law International (IRLI); Mwongozo wa Mafunzo ya Mashauri ya Watoto kwa Wasaidizi wa Kumbukumbu wa Mahakama kwa kushirikiana na UNICEF na kutoa chapisho la Utamaduni wa Mahakama. (k) Kuratibu mapitio na marekebisho ya sheria 66. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu mapitio na marekebisho ya Sheria mbalimbali. Lengo likiwa ni kuboresha ufanisi na kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu ya Sekta ya Sheria. Katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, Wizara kwa Kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliandaa na kuwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali katika Sekta ya Sheria (The Legal Sector Laws (Miscellaneous Ammendments) Bill No. 4 of 2023). Katika kipindi hicho Sheria 22 za Sekta ya Sheria zilifanyiwa marekebisho kama ilivyofafanuliwa katika Kiambatisho Na.4. 67. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/2024, Wizara kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imefanya mapitio ya mfumo wa sheria na tathmini ya utekelezaji wa Sheria kwa lengo la kuhakikisha kuwa sheria zinaakisi mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiteknolojia. Tume imefanya mapitio ya mfumo wa sheria zinazosimamia makosa dhidi ya maadili kwa kufanya utafiti katika mikoa 18 ya Tanzania Bara. Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Arusha, Manyara, Singida, 44 Dodoma, Iringa, Mbeya, Katavi, Kigoma, Tabora, Mwanza, Geita, Mara, Ruvuma, Lindi na Mtwara. Taarifa ya utafiti imekamilika na kuwasilishwa Serikalini kwa utekelezaji. 68. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia kuwa Sekta ya Sanaa nchini inakua kwa kasi na kuajiri vijana wengi na kutoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi na kuongeza Pato la Taifa, Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutunga sheria ili kusimamia haki za kazi za Sanaa. Katika kipindi cha mwaka 2023/2024, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imefanya tathmini ya Sheria zinazosimamia Hakimilki na Hakishiriki zikiwemo, Sheria ya Hakimilki na Hakishiriki, Sura ya 218; Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza, Sura ya 230; Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa, Sura ya 204; Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332; Sheria ya Usimamizi wa Tozo na Ushuru, Sura ya 147 na Sheria ya Makosa Mtandaoni, Sura ya 443. Dhumuni la tathmini lililenga kupima kama malengo ya kutungwa kwa sheria hizo yamefikiwa katika kuhakikisha kuwa Sekta ya Sanaa inakua ya kibiashara na yenye tija kwa wasanii na Taifa kwa ujumla. Tathmini hiyo imehusisha wadau wanaosimamia utekelezaji wa Sheria za Hakimilki na Hakishiriki katika Mikoa mitano (5) ya Dar es Salaam, Pwani, Mbeya, Dodoma na Mwanza. Taarifa ya tathmini hiyo itawasilishwa serikalini kwa ajili ya kufanyiwa kazi. 45 69. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imetekeleza mapendekezo ya Tume ya Kuangalia namna ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai kwa kufanya mapitio ya sheria zinazosimamia dhamana ikiwemo Sheria zilizofanyiwa mapitio ni pamoja na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20; Sheria ya Kudhibiti Makosa ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa, Sura ya 200; Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi, Sura ya 446; Sheria ya Mahakama za Mahakimu, Sura ya 11; Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Sura ya 95; Sheria ya Mamlaka ya Rufaa, Sura ya 141; Sheria ya Usalama wa Taifa, Sura ya 47; Sheria ya Mtoto, Sura ya 13 na Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi, Sura ya 322. Aidha, Tume imefanya mapitio ya Sheria za Adhabu ya Viboko na tathmini ya utekelezaji wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20 hususan Kifungu 91(1) kinachohusiana na uondoshaji mashauri mahakamani (nolle proseque) pamoja na tathmini ya Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi. 46 70. Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mfumo wa Haki Jinai nchini, Tume ya Kurekebisha Sheria imefanya utafiti wa Mfumo wa Sheria Unaosimamia Makosa ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa ili kubaini upungufu uliopo na kupendekeza makosa yanayostahili kuwa ya uhujumu uchumi na makosa yasiyostahili kuwa ya uhujumu uchumi.Utafiti huo umefanyika katika Mikoa Sita (6) ya Dodoma, Dar Es Salaam, Arusha, Manyara, Mara na Mwanza. (l) Kuandaa Sera Mahsusi Zinazosimamia Mifumo ya Utoaji Haki 71. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa sera na sheria zinaandaliwa ili kuimarisha upatikanaji haki na kutoa mchango kwa maendeleo ya Taifa, Wizara imeanza maandalizi ya Sera ya Taifa ya Haki Jinai. Sera hiyo itajumuisha masuala mbalimbali katika mnyororo wa haki jinai ikiwemo utoaji taarifa za matukio ya uhalifu; ushahidi; uchunguzi wa uhalifu; ufunguaji wa hati za mashtaka; uendeshaji wa mashtaka; utoaji wa hukumu; usimamizi wa wafungwa magerezani; na urejeshwaji wa wafungwa uraiani baada ya kumaliza kifungo au kupata msamaha wa adhabu ya kifungo. 47 (m) Kuendelea Kuimarisha Mfumo wa Uangalizi wa Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi 72. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 Wizara ilitoa mafunzo ya kujenga uelewa kuhusu masuala ya uangalizi wa utajiri asili na maliasilia za nchi kwa Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi, wanaohusika na uangalizi na usimamizi wa utajiri asili na maliasilia za nchi. Mafunzo hayo yalihusu usimamizi na uwajibikaji katika ulinzi na matumizi ya utajiri asili na maliasilia za nchi, usimamizi wa mikataba, na itifaki baina ya Tanzania na nchi nyingine kwa kuzingatia Sheria za Uangalizi wa Utajiri Asili na Maliasilia za nchi Sura ya 449 na 450. 73. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/2024, Wizara imeendelea kushiriki katika majukumu ya kupitia mikataba mbalimbali inayohusu uwekezaji kwenye utajiri asili na maliasilia za nchi baina ya Tanzania na nchi nyingine ambapo katika kipindi cha mwezi April, 2024 Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepitia mikataba ya uwekezaji 18 kwa lengo la kubaini iwapo inakidhi mahitaji ya sasa ya kiuchumi na kijamii. Vilevile, katika kipindi tajwa Wizara imeandaa na kusambaza Rasimu ya Mwongozo wa Usajili wa 48 Mikataba ya Utajiri asili na Maliasilia za nchi katika sekta zinazohusika na usimamizi wa utajiri asili na maliasilia kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa uzingatiwaji wa Sheria tajwa ambapo mikataba mitano (5) inayohusu uwekezaji katika madini na fukwe za bahari imesajiliwa. 74. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwezi Julai 2023 hadi April,2024 Wizara imepokea taarifa kutoka sekta 10 zinazosimamia masuala ya utajiri asili na maliasilia za nchi ambazo zimetoa taarifa ya namna ambavyo Sheria na Sera za sekta husika zilivyozingatia misingi ya Sheria za Uangalizi wa utajiri asili na Maliasilia za nchi ambayo ni Mamlaka ya nchi ya kudhibiti na kumiliki utajiri asili na maliasilia za nchi; uvunaji na matumizi endelevu ya utajiri asili na maliasilia kwa vizazi vya sasa na vijavyo; Msingi wa wananchi kunufaika na utajiri asili na maliasili; Misingi ya ushirikishwaji wa wananchi katika matumizi na uvunaji wa utajiri asili na maliasilia; pamoja na msingi wa mgawanyo wa mapato na uwazi katika mikataba ya utajiri asili na maliasilia. katika kipindi husika, Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Madini pamoja na Shirika la Maendeleo la Taifa ilitembelea mradi wa Liganga na Mchuchuma uliopo Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe. Ziara hiyo, ililenga kutembelea eneo la mradi kuonana na wananchi wanaozunguka eneo hilo ili kutambua afua zinazoweza kuwasaidia wananchi kiuchumi pindi mradi huo utakapoanza kwa 49 kuzingatia Sheria za Utajiri asili na maliasilia za nchi, kusikiliza kero za wananchi wa eneo la mradi na kubaini changamoto mbalimbali za kisheria zinazokwamisha utekelezaji wa mradi huo. (n) Kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za sheria nchini 75. Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mfumo wa utoaji haki, Wizara imetoa vifaa vya TEHAMA kwa taasisi za haki jinai ambavyo ni: (i) Seti 24 za Video Conference kwa ajili ya kuendesha mashauri kwa njia ya mtandao kwa Mahakama ya Tanzania ambazo zitafungwa kwenye Mahakama 24 za Mikoa; na (ii) Jumla ya Kompyuta za mezani tano (5), Kompyuta mpakato 86, printa 13 na televisheni moja (1) zimetolewa kwa ajili ya magereza ya Njombe, Ludewa na Msalato; Ofisi ya Taifa ya Mashtaka; na Taasisi ya Afya ya Akili ya Mirembe sehemu ya Isanga ili kuimarisha huduma za TEHAMA katika utoaji haki. 76. Mheshimiwa Spika, Wizara imeanzisha Kituo cha Huduma kwa Wateja (Contact Centre) kwa ajili ya kupokea malalamiko, taarifa na maoni kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali wa 50 utoaji haki. Lengo la kuanzishwa kituo hiki ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanaondolewa adha ya kusafiri umbali mrefu na gharama kubwa kufuatilia haki zao. Kituo hiki kimeanza kutumika tangu Februari, 2024 kupitia namba 0262160360 na tayari kituo kimepokea malalamiko 24 ambapo hadi Aprili, 2024 malalamiko hayo yamefanyiwa kazi. 77. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) imeendelea kusogeza na kuimarisha utoaji wa huduma kwa mwananchi kupitia TEHAMA. Katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 huduma za usajili wa Vizazi, Vifo, Ndoa, Talaka na Bodi za Wadhamini zimewezeshwa kupatikana kidijitali (eRITA) na mwananchi anaweza kutuma maombi popote alipo bila kufika ofisi za Wakala na kuchagua Ofisi ya Wilaya iliyokaribu kwa ajili ya kupata huduma ya cheti cha kuzaliwa, kifo, ndoa, talaka, leseni ya kufungisha ndoa na cheti cha usajili wa Bodi ya Wadhamini. 78. Mheshimiwa Spika, katika kipindi husika Wizara kupitia Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) imeunganisha na kuwezesha kubadilishana taarifa ya mifumo yake na Taasisi tisa (9) za Serikali ambazo ni: - Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Wizara ya Katiba na Sheria, Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Mawasiliano 51 Tanzania (TCRA) na Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu. Vilevile, katika kuhakikisha matukio ya vizazi na vifo yanasajiliwa kwa wakati, Wakala imeunganisha mfumo wa usajili wa vizazi na vifo na mfumo wa” GoTHoMIS” unaosimamiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Mfumo wa DHIS2 wa Wizara ya Afya ili kuwezesha kupatikana taarifa za matukio ya vizazi na vifo pindi yanapotokea. Vilevile, taarifa za huduma zinazotolewa na Wakala zinapatikana kidijitali kupitia Basi Mtandao la Serikali (GovESB). Aidha, Wakala inatarajia hadi kufikia Desemba, 2024 iwe imeunganisha wadau wote wanaohitaji na kutumia taarifa za RITA. (o) Kuendelea na Utekelezaji wa Mkakati wa Pili wa Taifa wa Haki Mtoto 2020/2021-2024/2025 79. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, Wizara imeendelea na utekelezaji wa Mkakati wa Pili wa Taifa wa Haki Mtoto kwa kufanya kikao cha tatu cha Jukwaa la Haki Mtoto, ambapo masuala mbalimbali kuhusu haki za mtoto yalijadiliwa, ikiwemo kuendelea na mpango wa kuweka mazingira wezeshi ya ukuaji na upatikanaji haki kwa mtoto nchini. Vilevile, kuendelea kuratibu kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya ukatili wa mtoto kwa njia ya mitandao ikiwa na lengo la kuhakikisha mtoto anakuwa katika mazingira mazuri na salama, ikizingatiwa kuwa mtoto ni taifa la leo na kesho. Pia, katika 52 kutekeleza Mkakati huu, Wizara imeendelea na mpango wa uratibu wa utoaji huduma za msaada wa kisheria hususan katika masuala ya ukatili dhidi ya mtoto nchini kwa kuwajengea uwezo watoto, Wasajili Wasaidizi, Wasaidizi wa Kisheria, Viongozi wa Serikali za Mitaa, Viongozi wa kidini na Kimila katika kushughulikia masuala yanayohusiana na ukatili dhidi ya mtoto. Vilevile, Jukwaa hili limeweka mkakati wa kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa watoto wanaokinzana na sheria kwa kuwapatia Mawakili wa kuwawakilisha katika mashauri yaliyo mahakamani. (p) Kutoa Elimu kwa Umma kuhusu majukumu ya Tume na Kamati za Maadili ya Maafisa Mahakama ngazi ya Mikoa na Wilaya 80. Mheshimiwa Spika, Tume ya Utumishi wa Mahakama imeendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya Tume na Kamati za Maadili ya Maafisa Mahakama ngazi ya Mikoa na Wilaya kwa kutoa Mafunzo elekezi juu ya Kanuni za Maadili za Maafisa Mahakama na Kanuni Mpya za Uendeshaji wa Kamati za Maadili ya Maafisa Mahakama wa Wilaya na Mikoa. Katika kipindi husika, jumla ya wajumbe 91 kutoka Kamati za Maadili ya Maafisa Mahakama wa Wilaya na Mkoa kwa Mikoa ya Mbeya, Songwe, Kilimanjaro, Tanga, Katavi na Rukwa walijengewa uwezo kuhusu uendeshaji wa kamati za Mikoa na Wilaya. 53 81. Mheshimiwa Spika, Tume ilifanya ziara katika Mikoa ya Kagera, Geita na Morogoro. Lengo la ziara hiyo ni kujitangaza kwa wananchi na watumishi wa Mahakama ili wajue Sheria iliyounda Tume, Muundo, Mamlaka pamoja na majukumu ya Kamati za Maadili za Mikoa na Wilaya. Aidha, Tume ilitoa elimu kwa Umma katika Maonesho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika Januari, 2024 jijini Dodoma ambapo jumla ya washiriki 81 walipata elimu. 82. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha Kamati za Maadili ya Maafisa Mahakama ngazi za Mikoa na Wilaya, Tume ya Utumishi wa Mahakama ilifanya ziara kwenye Mikoa minne (4) ya Dodoma, Singida, Shinyanga na Simiyu. Lengo la ziara hiyo ni kutoa mafunzo kwa wajumbe wa Kamati za Maadili ya Maafisa Mahakama pamoja na elimu kwa umma kuhusu uwepo wa Kamati hizi. Aidha, watendaji wa Tume walifanya ukaguzi kwenye mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu na Mara kwa Lengo la kuangalia namna Kamati zinavyotekeleza majukumu yake pamoja na kupokea maoni ya kuboresha utendaji wa Kamati za Maadili ya Maafisa Mahakama. (q) Kufanya Tafsiri, Uandishi, Uhakiki wa Mikataba na Urekebu wa sheria 83. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha upatikanaji haki na utawala bora, Serikali kupitia Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Sekta ya 54 Sheria, Namba 11/2023 ilifanya marekebisho ya muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuanzisha Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria. Lengo la maboresho haya ni kuongeza tija na ufanisi katika shughuli za uandishi wa sheria, urekebu na ufasiri wa sheria. Maboresho haya pia, yanalenga kuhakikisha upatikanaji wa sheria, kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu sheria, na hivyo kuiwezesha nchi kutekeleza mipango ya maendeleo. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwandishi Mkuu wa Sheria inaendelea kukamilisha taratibu za kiutawala ili kuwezesha Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. 84. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa sheria za nchi zinakwenda na wakati na zinaakisi Sera na vipaumbele vya Serikali katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, mazingira na teknolojia. Katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 Ofisi iliandaa Miswada 14. Miswada iliyoandaliwa ni kama ilivyooneshwa kwenye Kiambatisho Na.5. Aidha, Miswada ya Sheria 15 ilijadiliwa na kupitishwa kuwa Sheria na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sheria hizo ni kama zilivyooneshwa kwenye Kiambatisho Na.6. 55 85. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilihakiki na kuchapisha jumla ya Sheria Ndogo 885, ikilinganishwa na Sheria Ndogo 631 zilizohakikiwa na kuchapishwa katika kipindi kama hicho mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la asilimia 40. Sheria hizo zinajumuisha Kanuni 138, Amri 420, Notisi 323 na Matamko manne (4). Orodha ya Sheria Ndogo zilizoandaliwa kuanzia Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 zinaonekana kwenye Kiambatisho Na.7. Lengo la kutengenezwa kwa sheria ndogo ni kufafanua kwa kina na kwa undani maudhui yaliyobainishwa kwenye Sheria Kuu. 86. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, jumla ya Sheria Kuu 74 zimefanyiwa ufasiri kwa awamu ya pili. Sheria hizo zinasubiri kufanyiwa uhakiki wa mwisho na kuchapishwa kati Gazeti la Serikali (Kiambatisho Na.8). 87. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekamilisha urekebu wa Sheria Kuu 446 kwa lengo la kutoa toleo la urekebu la Sheria Kuu la mwaka 2023 (Revised Edition 2023). Toleo hili lipo katika hatua za mwisho za uchapishaji na utengenezaji wa Juzuu linalotarajiwa kuzinduliwa Juni, 2024. 56 88. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, imeendelea kushiriki na kutoa ushauri wa kisheria katika majadiliano mbalimbali ya Mikataba ya kibishara, mikutano ya kitaifa, kikanda na kimataifa. Katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 jumla ya Mikataba ya Kitaifa na Kimataifa 1,280 kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Mashirika ya Umma, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ilifanyiwa upekuzi ikilinganishwa na Mikataba 1,171 iliyofanyiwa upekuzi katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023 sawa ongezeko la asilimia 9. Ongezeko hili linatokana na kuongezeka kwa idadi ya Miradi ya Serikali na miradi inayofadhiliwa na Wadau wa Maendeleo. Aidha, Hati za Makubaliano 341 zilifanyiwa upekuzi ikilinganishwa na idadi ya Hati za Makubaliano 295 zilizofanyiwa upekuzi katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. Ongezeko hili linaakisi jitihada za Serikali kuhamasisha uwekezaji na diplomasia ya ushirikiano wa kikanda na kimataifa. 89. Mheshimiwa Spika, kati ya Mikataba 1,280 iliyofanyiwa upekuzi, Mikataba 458 ilithaminishwa katika sarafu mbalimbali katika mchanganuo ufuatao: Mikataba 351 ilikuwa na thamani ya Shilingi za Kitanzania trilioni 10.52; Mikataba 92 ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani bilioni 2.30 sawa na Shilingi za Kitanzania trilioni 5.40; na Mikataba 15 ilikuwa na thamani ya Fedha ya Jumuiya ya Ulaya (Euro) 57 360,577,992.11 sawa na Shilingi za Kitanzania trilioni 1.002. Mikataba iliyofanyiwa upekuzi ilihusisha masuala ya ununuzi, ujenzi na ukarabati wa majengo, utoaji wa huduma za jamii kama vile ujenzi wa shule, hospitali na barabara. 90. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ina jukumu la kutoa ushauri wa kisheria kwa Serikali Kuu, Wizara, Idara zinazojitegemea, Mashirika ya Umma, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na kwa wananchi. Lengo ni kuhakikisha Serikali na Taasisi zake zinapata faida kutokana na utekelezaji wa majukumu yake na hivyo, kuikinga Serikali kuingia katika kesi mbalimbali kwa kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu za nchi zinafuatwa. Katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 jumla ya maombi ya ushauri wa kisheria 1,707 yalipokelewa na kufanyiwa kazi ikilinganishwa na maombi 812 katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023 sawa na ongezeko la asilimia 110. Kati ya maombi 1,707, maombi 390 yalihusu malalamiko ya watu binafsi na maombi 1,317 yanatoka katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Mashirika ya Umma, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. (r) Kuendesha Mashtaka ya Jinai 91. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (OTM) iliendesha kesi za jinai katika 58 Mahakama za Wilaya, Hakimu Mkazi, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani. Jumla ya kesi za jinai 27,205 ziliendeshwa katika Mahakama za Wilaya na Hakimu Mkazi ikilinganishwa na kesi 32,609, zilizoendeshwa katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. Aidha, jumla ya kesi 16,928 sawa na asilimia 62 zilihitimishwa ikilinganishwa na kesi 18,485 sawa na asilimia 57 ya kesi zilizohitimishwa katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. Kati ya kesi zilizohitimishwa, 10,444 zilihitimishwa kwa washtakiwa kutiwa hatiani ikilinganishwa na kesi 10,392 zilizohitimishwa kwa kipindi cha kuanzia Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 92. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iliendesha jumla ya kesi 680 katika Mahakama za watoto (Juvenile Courts) ambapo kesi 454 zilihitimishwa sawa na asilimia 67. 93. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili, 2024, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iliendesha jumla ya kesi 6,649 katika Mahakama Kuu ya Tanzania ikilinganishwa na kesi 6,425 zilizoendeshwa katika kipindi kama hicho mwaka 2022/2023. Aidha, kesi 2,408 zilihitimishwa sawa na asilimia 36 ikilinganishwa na kesi 2,629 zilizohitimishwa kwa kipindi kama hicho mwaka 2022/2023 sawa na asilimia 41 ya kesi zilizoendeshwa. 59 94. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iliendesha jumla ya kesi 2,905 za jinai katika Mahakama ya Rufani ikilinganishwa na kesi 1,535 zilizoendeshwa kipindi kama hicho katika mwaka 2022/23. Kati ya kesi hizo, kesi 414 zilihitimishwa sawa na asilimia 14 ya kesi zilizokuwa zikiendeshwa ikilinganishwa na kesi 267 zilizohitimishwa kipindi kama hicho mwaka 2022/2023 sawa na asilimia 17 ya kesi zilizokuwa zikiendeshwa. 95. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/2024 hadi Aprili, 2024, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iliendesha kesi kubwa 64 katika Mahakama Kuu – Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ikilinganishwa na kesi 90 zilizoendeshwa kipindi kama hicho mwaka 2022/2023. Aidha, kesi 24 zilihitimishwa katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 na kesi 40 zinaendelea katika hatua mbalimbali. 96. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka inaendelea kukagua magereza na vituo vya polisi nchini kwa lengo la kuainisha changamoto za kiutendaji na kiupelelezi na kutoa maelekezo stahiki ya kutatua changamoto hizo kwa mujibu wa sheria. Katika mwaka 2023/2024, hadi kufikia Aprili, 2024 jumla ya magereza 107 yalikaguliwa ikilinganishwa na magereza 63 yaliyokaguliwa kipindi kama hicho katika mwaka 60 2022/2023 sawa na ongezeko la magereza 44. Pia, ukaguzi umefanyika katika vituo vya Polisi 251 ikilinganishwa na vituo 140 vilivyokaguliwa katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2022/2023 ikiwa ni ongezeko la vituo 111. Katika ukaguzi huo jumla ya mahabusi 1,250 waliachiwa ikilinganishwa na mahabusi 333 walioachiwa kipindi kama hicho kwa mwaka 2022/2023 ikiwa ni ongezeko la mahabusi 917 (Kiambatisho Na.9). (s) Uratibu na Usimamizi wa Shughuli za Upelelezi wa Makosa ya Jinai 97. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/2024 hadi Aprili, 2024 OTM ilishughulikia jumla ya majalada 16,854 kutoka vyombo vya upelelezi ikilinganishwa na majalada 12,535 yaliyoshughulikiwa katika kipindi kipindi kama hicho mwaka 2022/2023. Kati ya majalada hayo, majalada 11,255 yaliandaliwa hati za mashtaka sawa na asilimia 67 ya majalada yaliyoshughulikiwa ikilinganishwa na majalada 6,349 yaliandaliwa hati za mashtaka katika mwaka 2022/2023 sawa na asilimia 51 ya majalada yaliyoshughulikiwa. 98. Mheshimiwa Spika, kati ya majalada 16,854 yaliyopokelewa, majalada 1,138 yalifungwa ikilinganishwa na majalada 658 yaliyofungwa kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023 na majalada 3,439 yalirejeshwa kwa upelelezi zaidi ikilinganishwa na majalada 2,856 61 yaliyorejeshwa kwa upelelezi zaidi katika kipindi kama hicho katika mwaka 2022/2023. Hivyo, kufanya majalada yaliyofanyiwa kazi katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili, 2024 kuwa 15,832 sawa na asilimia 94 ya majalada yaliyopokelewa ikilinganishwa na 9,863 sawa na asilimia 79 ya majalada yaliyofanyiwa kazi kwa kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. Vilevile, majalada 1,022 yalikuwa yanaendelea kufanyiwa kazi kote nchini, sawa na asilimia 6 ya majalada yote yaliyopokelewa ikilinganishwa na majalada 2,672 sawa na asilimia 21 yaliyokuwa yanaendelea kufanyiwa kazi kwa kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 99. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kubuni mikakati ya kupunguza mlundikano wa mahabusi na wafungwa magerezani na kupunguza gharama za uendeshaji wa kesi kwa kuhimiza matumizi ya adhabu mbadala. Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili, 2024 Wizara kupitia Mahakama imetoa Waraka wa Mhe. Jaji Kiongozi Na 4/2019 unaosisitiza maafisa wa Mahakama kutoa kipaumbele katika adhabu mbadala ya kifungo cha nje; Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Na.1 ya Mwaka 2022 (The Written Laws- Miscellaneous Ammendments Act No. 1 of 2022) imetungwa ambayo ilifanya marekebisho ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20, kwa kuweka Kifungu kipya cha 131A kinachoweka sharti la Mwendesha Mashtaka kufungua Kesi mahakamani mara tu baada ya 62 kukamilisha shughuli za upelelezi ili kuepusha watuhumiwa kuwekwa vizuizini wakati kazi ya upelelezi ikiwa inaendelea. (t) Kushughulikia Urejeshwaji wa Wahalifu na Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Makosa ya Jinai 100. Mheshimiwa Spika, Tanzania imeendelea kushirikiana na mataifa mengine katika kusimamia kurejeshwa kwa watuhumiwa wa uhalifu katika nchi walikofanya makosa. Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili, 2024 Wizara imepitia mikataba ya urejeshwaji wa wahalifu watoro kutoka nchi mbalimbali na kujadili namna bora ya kuboresha mikataba husika. Katika kipindi hicho, Wizara ilipokea na kushughulikia jumla ya maombi nane (8) kutoka nchi zifuatazo Uturuki (4), India (1), Afrika Kusini (2) na Kenya (1). Aidha, Tanzania imetuma jumla ya maombi saba (7) ya kuomba wahalifu katika nchi ya Kenya (2), Afrika Kusini (1), Saudi Arabia (1), India (1), Uganda (1) na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (1). (u) Kuwaachilia Huru Wagonjwa wa Afya ya akili walio chini ya uangalizi wa Taasisi ya Afya ya Akili Isanga 101. Mheshimiwa Spika, kutokana na kuthibitika kuwa wagonjwa hao walitenda makosa wakiwa na ugonjwa wa afya ya akili, Mahakama haikuwatia hatiani na hivyo kuamuru wawe chini 63 ya uangalizi wa Taasisi ya Afya ya Akili Isanga Dodoma kuendelea na matibabu wakisubiri amri ya Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Sheria kwa mujibu wa Kifungu cha 219 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20. Hivyo katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 jumla ya maombi 14 yaliwasilishwa Wizarani ambapo Amri ya kuwaachilia wagonjwa hao wa afya ya akili imetolewa. (v) Kuimarisha Utekelezaji wa Programu ya Kutenganisha Shughuli za Mashtaka na Upelelezi 102. Mheshimiwa Spika, OTM imeendelea kutekeleza mpango wa kutenganisha shughuli za mashtaka na upelelezi kwa kuendelea kuongeza idadi ya Mawakili wa Serikali na kuendelea kutoa vibali vya kuendesha mashtaka kwa Waendesha Mashtaka kutoka Ofisi na Taasisi mbalimbali. Lengo la mpango huu ni kusogeza huduma za kimashtaka kwa wananchi katika ngazi za Mikoa na Wilaya. Katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, OTM ilihuisha Kanzidata ya Waendesha Mashtaka waliopewa kibali cha kuendesha mashtaka na Mkurugenzi wa Mashtaka na Daftari la Mawakili wa Serikali. Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ina jumla ya Mawakili 663 pamoja na Waendesha Mashtaka waliopewa kibali na Mkurugenzi wa Mashtaka wapatao 1,095 nchi nzima. Pia, jumla ya wataalam 233 wanaohusika 64 na upelelezi katika maeneo ya maandishi, picha, alama za vidole na milipuko wametangazwa katika Gazeti la Serikali. 103. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeendelea kusogeza huduma za kimashtaka kwa wananchi katika ngazi za Mikoa na Wilaya. Katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, Ofisi inaendelea kutoa huduma za kimashtaka katika mikoa 30 ya Kimashtaka na Ofisi 92 za Wilaya. Kushughulikia Uendeshaji wa Mashauri ya Madai na Usuluhishi 104. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inaendelea kuiwakilisha Serikali katika kuendesha mashauri mbalimbali ya madai na usuluhishi ndani na nje ya nchi. 105. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2024, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imeendesha jumla ya mashauri ya Madai 7,813 (mashauri ya ndani ya nchi 7,798 na mashauri ya nje ya nchi 15), kati ya hayo, mashauri 6,113 ni mwendelezo wa mashauri ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 na mashauri 1,700 ni mashauri yaliyofunguliwa katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024. Katika kipindi hicho, mashauri 762 yalimalizika, yakijumuisha, mashauri ya ndani ya nchi 750 na mashauri ya nje ya nchi 12. Aidha, kati ya mashauri ya madai yaliyomalizika, mashauri 719 65 yalihitimishwa Mahakamani na mashauri 43 yalihitimishwa kwa njia ya majadiliano nje ya mahakama. 106. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ilishinda jumla ya mashauri 705 yenye madai ya fedha na kufanikiwa kuokoa fedha za Serikali jumla ya Shilingi 396,202,611,667.70. Vilevile Ofisi imeokoa jumla ya Shilingi 10,205,263,509.43 zilizotokana na mashauri 43 yaliyohitimishwa kwa njia ya majadiliano nje ya Mahakama. Hivyo, kufanya kiasi kilichookolewa kwa kushinda kesi za Madai na kufanya majadiliano nje ya Mahakama kuwa jumla ya Shilingi 406,407,875,177.13. 107. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/2024, hadi kufikia Aprili, 2024, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imehitimisha mashauri ya madai yasiyohusisha fedha yakiwemo mashauri ya katiba, haki za binadamu, uwekezaji na biashara. Kwa mfano, Serikali imeshinda Shauri la kupinga kujengwa kwa mradi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki, shauri la kupinga Mkataba wa Uwekezaji katika Bandari ya Dar es salaam na Shauri la kupinga uwekezaji katika kiwanda cha Saruji cha Tanga. 108. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mashauri ya Usuluhishi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, imeendesha jumla ya mashauri ya usuluhishi 179 kati ya mashauri hayo mashauri 66 148 ni ya ndani ya nchi na mashauri 31 ni ya nje ya nchi. Katika kipindi hiki, jumla ya mashauri 19 yalimalizika, ambapo mashauri 8 yalimalizika katika mabaraza/mahakama ya ndani ya nchi na mashauri 2 yalimalizika katika mabaraza nje ya nchi. Aidha mashauri 6 ya kitaifa na mashauri 3 ya kimataifa yalimalizika kwa njia ya majadiliano. 109. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, imewezesha Serikali kushinda katika mashauri matano (5) yaliyoendeshwa ndani ya nchi (Kitaifa) na kuokoa Shilingi 7,297,302,818.21 na shauri moja (1) la kimataifa na kuokoa Shilingi 818,285,700.00 (Milioni 818.28) na Dola za Marekani 11,732,699.45 sawa na Shilingi 30,153,037,586.50 (Bilioni 30.15). Hivyo, Serikali imeokoa jumla ya Shilingi 38,268,626,104.71 (Bilioni 38.26) kutokana na kushinda mashauri hayo ya usuluhishi. 110. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2024, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, imehitimisha mashauri tisa (9) ya usuluhishi kwa njia ya majadiliano nje ya Mahakama, kati ya hayo mashauri sita (6) ni ya ndani ya nchi na mashauri matatu (3) ya nje ya nchi. Kupitia majadiliano haya, Serikali imeokoa Shilingi 47,510,903,758.35; Dola za Marekani 60,322,799.82 (sawa na Shilingi 141,456,965,577.90) na Euro 487,982,230.66 (sawa na Shilingi 1,317,552,022,700.00 (Trilioni 67 1.3), hivyo, Serikali imeokoa jumla ya Shilingi 1,506,519,892,036.25 (Trilioni 1.5). 111. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inaendelea kuendesha mashauri ya usuluhishi 160 katika vyombo na mabaraza mbalimbali ya usuluhishi ndani na nje ya nchi. (w) Kuratibu Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu, Usimamizi wa Ufilisi na Udhamini 112. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imeendelea kuimarisha shughuli za usajili wa matukio muhimu ya binadamu, ufilisi na udhamini kwa ajili ya mipango na maendeleo ya Taifa. Katika mwaka wa fedha 2023/2024, hadi kufikia Aprili, 2024 RITA imesajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa 1,520,899 pamoja na vyeti vya vifo 25,783. Aidha, uhakiki umefanyika kwa vyeti vya kuzaliwa vya wanafunzi 130,493 na vyeti vya vifo 20,175 vya wazazi wa wanafunzi wanaoomba mkopo Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu. 113. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 Wizara kupitia Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini ilisajili jumla ya watoto 678,371 wenye umri chini ya miaka mitano katika mikoa ya Kigoma, Kagera na Dar es Salaam. Aidha, Mradi huu umeendelea kutekelezwa katika Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, 68 Halmashauri 184, Kata 3,957 na Vituo vya Afya 7,304 na kufanya idadi ya watoto wa umri chini ya miaka mitano waliosajiliwa kupitia mpango huu kufikia 9,609,664 na kuweza kuongeza kiwango cha usajili katika kundi hili kutoka asilimia 13 mwaka 2012 hadi asilimia 68 mwaka 2024. 114. Mheshimiwa Spika, katika kuboresha usajili na utoaji wa vyeti kwa wakati kwa watoto wanaozaliwa, RITA kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais - TAMISEMI imeendela kutoa maelekezo kwa Mamlaka 184 za Serikali za Mitaa kuhakikisha watoto wanapozaliwa wanasajiliwa ikiwa ni sehemu ya haki ya mtoto. Pamoja na kuingiza taarifa hizo kwenye kanzidata ya RITA ili Serikali ipate takwimu za watoto waliozaliwa kwa ajili ya mipango ya maendeleo. 115. Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza Kampeni ya Kitaifa ya Kulinda Maadili, Haki na Ukatili Dhidi ya Watoto, katika mwaka 2023/2024 hadi kufikia Aprili, 2024, RITA imesajili jumla ya hati 28 za kuasili watoto baada ya kupokea amri za Mahakama. 116. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia RITA inaendelea na usajili wa matukio ya ndoa na talaka ambapo katika kipindi husika jumla ya marejesho 35,777 ya ndoa zilizofungwa na nakala za hukumu za talaka 798 zimesajiliwa. 69 117. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia RITA imeendelea na jukumu la usimamizi na usajili wa bodi za wadhamini ambapo katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 RITA ilipokea jumla ya maombi ya huduma za bodi za wadhamini 1,112. Kati ya maombi hayo 1,039 yalihitimishwa na 83 yanaendelea kufanyiwa kazi kama yalivyoainishwa katika Kiambatisho Na.10. Vilevile, katika kuboresha utendaji wa bodi hizo, RITA imeandaa mwongozo wa Katiba ambayo inatakiwa kufuatwa na bodi zote za wadhamini zilizosajiliwa na zinazotarajiwa kusajiliwa RITA. Kupitia mwongozo huo migogoro ya bodi za wadhamini inayowasilishwa RITA itapungua kutokana na kuwepo kwa ibara inayohusu namna ya kusuluhisha migogoro hiyo pindi itakapojitokeza katika taasisi hizo. 118. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/2024 hadi kufikia Aprili, 2024 Wizara kupitia RITA imehudhuria mashauri 47 yaliyopo katika mahakama mbalimbali pamoja na Mabaraza ya Ardhi na Nyumba yanayohusu masuala ya mirathi na Bodi za Wadhamini zinazosimamiwa na Wakala. Jumla ya mashauri 25 yamemalizika hivyo kuendelea na taratibu nyingine za ugawaji wa mali kwa wanufaika na mashauri 22 yanaendelea kufanyiwa kazi. Aidha, RITA inasimamia jumla ya mirathi 90 ambapo mirathi saba (7) imefungwa baada ya kugawa mali kwa wanufaika na 83 zinaendelea kufanyiwa kazi. 70 119. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Wakala imeendelea kuimarisha upatikanaji haki kwa wakati kwa wananchi hususan katika masuala ya mirathi. Katika Mwaka wa Fedha, 2023/2024 hadi kufikia Aprili, 2024 RITA imeandika na kutunza wosia 118 na kuendelea kutoa elimu zaidi wa wanachi kuhusiana na faida za kuandika na kuhifadhi wosia ili kupunguza migogoro ya mirathi inayojitokeza katika jamii. Aidha, Wizara kupitia RITA imetoa elimu kuhusu uandishi wa wosia na masuala ya mirathi kwa wananchi 29,826 kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia 14,156 (Wanawake 8,494 na Wanaume 5,662); na makongamano na maonyesho ya Kitaifa ikiwemo ya Wiki ya Sheria, Nane Nane na Saba Saba 15,670 (wanawake 8,305 na wanaume 7,365). (x) Utekelezaji wa Masuala ya Kisheria katika ngazi ya Kikanda na Kimataifa 120. Mheshimiwa Spika katika kuimarisha ushirikiano wa masuala ya kisheria kikanda na kimataifa, Wizara imeshiriki mikutano miwili ya kimataifa ikiwemo Mkutano wa kikao cha 46 cha nchi wanachama wa ESAAMLG kilichofanyika Kasane- Botswana Septemba, 2023 na Mkutano wa Bodi ya Uongozi ya (United Nations African Institute for Prevention of Crime and the Treatment of Offenders - UNAFRI), Addis Ababa, Ethiopia na Septemba 2023 Wizara ilishiriki katika warsha 71 iliyoandaliwa na Sekretarieti ya Umoja wa Afrika iliyofanyika Cape Town Afrika Kusini Septemba, 2023 kujadili Itifaki ya Hali za Binadamu na Watu Kuhusiana Mtazamo Mahususi wa Haki ya Utaifa na Kuondoa Hali ya Kutokuwa na Utaifa Afrika (Protocal to the Frican Charter on Human and Peoples’ Rights Relating to the Specific Aspect of the Rights to a Nationality and Eradication of Statelessness in Africa). Aidha, Desemba, 2023 Wizara ya Katiba na Sheria imesaini Hati ya Makubaliano na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Shirikisho la Urusi ili kuimarisha ushirikiano katika Sekta ya Sheria. 121. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ilishiriki katika mkutano wa Kamati Ndogo ya Umoja wa Kudhiti Fedha Haramu Duniani na Afrika na Mashariki ya Kati (FATF (ICRG-AMEJG) uliofanyika nchini Jordan. Aidha, Wizara ilishiriki katika Mkutano Maalum wa Nane wa Kamati ya Mawaziri wa Sheria na Haki ya Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia tarehe 11 hadi 13 Desemba, 2023. Pia, Wizara ilishiriki katika Mkutano wa Kawaida wa Tisa wa Kamati ya Mawaziri wa Sheria na Haki ya Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia tarehe 14 hadi 16 Desemba, 2023. Vilevile, Wizara ilishiriki katika Mkutano Maalum wa Tisa wa Kamati ya Mawaziri wa Sheria na Haki ya Umoja wa Afrika uliofanyika Darban, Afrika ya Kusini tarehe 07 hadi 12 Februari, 2024. Ushiri wa Wizara katika mikutano 72 hiyo umewezesha lugha ya Kiswahili kutumika rasmi katika vikao vya Kamati ya Mawaziri wa Umoja wa Afrika kuanzia tarehe 07 Februari, 2024. 122. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, Wizara kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ilishiriki katika Mkutano wa 10 wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Rushwa (UNCAC) uliofanyika Atlanta, Marekani. Lengo la Mkutano lilikuwa ni kubadilishana uzoefu wa namna ya kupambana na uhalifu kwa nchi wanachama. 123. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa nchi mwenyeji wa Kikao cha 77 cha Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu. Katika kikao hicho jumla ya wadau 1,860 wameshiriki. Baadhi ya manufaa kwa Tanzania kuwa nchi mwenyeji wa Kikao hiki ni pamoja na kuingiza fedha za kigeni takribani Dola za Marekani 7,000,000. Katika kikao hiki, Serikali iliwasilisha taarifa kuhusu; upatikanaji wa haki ya elimu; uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa taarifa; kupinga ukali na ubaguzi dhidi ya wanawake; haki za watoto, wazee na watu wenye ulemavu; kuinua wanawake kiuchumi; kulinda mazingira; haki ya upatikanaji wa maji safi na salama; kupinga utesaji; kulinda wakimbizi; maendeleo ya vijana; na kuzingatia haki za binadamu wakati wa kutekeleza zoezi la 73 kuwahamisha wafugaji kutoka eneo la Ngorongoro kuhamia Kijiji cha Msomera, Handeni katika Mkoa wa Tanga. 124. Mheshimiwa Spika, Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Jumuiya ya Madola. Mkutano huo ulifanyika kuanzia tarehe 04 hadi 08 Machi, 2024 Unguja, Zanzibar. Aidha, Mkutano huo ulifunguliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jumla ya wageni 188 kutoka katika nchi 34 Wanachama wa Jumuiya ya Madola walishiriki. Yapo manufaa ambayo Tanzania imenufaika kwa kuwa nchi mwenyeji wa Kikao hiki ikiwemo kuingiza fedha za kigeni takribani Dola za Marekani 540,000. Manufaa mengine ya Tanzania kuwa nchi mwenyeji wa mikutano ya kikanda na kimataifa katika Sekta ya Sheria ni pamoja na: - (i) Kuongezeka sifa na heshima kwa Tanzania kidiplomasia na kuimarisha uhusiano wa kimataifa; (ii) Tanzania kuendelea kuaminika na kuheshimika kimataifa katika kutambua na kuheshimu utawala wa sheria na haki za binadamu; na 74 (iii) Kufahamika kwa vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania na hivyo kuongezeka kwa idadi ya watalii siku zijazo. 125. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha ushirikiano wa masuala ya kisheria katika ngazi za kikanda na kimataifa, Wizara kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika kipindi cha kuanzia Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, ilishiriki katika Kongamano la East African Legislative Summit on the Budapest Convention. Kongamano hili lilifanyika Jijini Arusha ambapo washiriki walitokea katika nchi za Kenya, Malawi, Msumbiji na Tanzania. Kongamano hilo lilijadili Muundo wa Sheria za Makosa ya Kimtandao za Nchi za Afrika Mashariki na namna gani nchi hizo zinaweza kujiunga katika Mkataba wa Kimataifa wa Makosa ya Kimtandao (Budapest Convention). 126. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, Wizara kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ilishiriki kikao Kazi cha Ushirikiano wa Kimataifa kati ya “Interpol” na Maafisa wa Polisi kutoka nchini Thailand na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai. Kikao hicho kilijadili ubadilishanaji wa taarifa kuhusu tuhuma za kusafirisha Kobe 116 kutoka Tanzania. 127. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, Wizara kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeshiriki katika Mkutano wa 17 wa Wataalam wa Utekelezaji wa 75 Mkataba wa Kimataifa wa Kupambana na Rushwa (UNCAC). Mkutano huu ulifanyika Vienna nchini Austria na kuwakutanisha pamoja maafisa viunganishi (focal persons) kutoka Nchi Wanachama. Lengo kuu la kikao hiki lilikuwa kufanya mapitio ya utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa kuhusu Urejeshwaji wa Mali zilizopatikana kwa njia ya Uhalifu. 128. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, Wizara kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ilipata fursa ya kushiriki Mkutano wa Geiger Working Group uliohusisha nchi kumi (10) ikiwemo Tanzania. Washiriki kutoka nchi Wanachama walijadili na kubadilishana uzoefu kuhusiana na namna ya kuzuia matumizi mabaya ya Mionzi na Nyuklia (Radiological and Nuclear Materials). Mkutano huo ulifanyikia tarehe 17 - 19 Oktoba, 2023, Zanzibar. (y) Ujenzi wa Majengo ya Ofisi 129. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili 2024, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imekamilisha ujenzi wa Ofisi za Mashtaka za Mikoa ya Shinyanga, Manyara, Katavi na Rukwa. Vilevile, OTM inaendelea na ujenzi wa Ofisi katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Njombe na Geita. Aidha, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inaendelea na ujenzi wa ofisi katika mikoa ya Mwanza (68%) na Arusha (12%). 76 (z) Kuimarisha Mfumo wa Kisheria na Kiutendaji ili kuchangia Mapambano Dhidi ya Rushwa 130. Mheshimiwa Spika, Wizara na Taasisi zake, inatekeleza afua zenye lengo la kuchangia mapambano dhidi ya rushwa. Katika mwaka wa fedha 2023/2024 kupitia Mradi wa Kujenga Uwezo Uendelevu wa kupambana na Rushwa Tanzania (Building Sustainable Anti-Corruption Action in Tanzania – BSAAT), kazi zifuatazo zimetekelezwa: (i) Uzinduzi wa Miongozo mitatu (3) ambayo ni Mwongozo wa Kuwajali na Kuwalinda Mashahidi (Witness Care and Protection Guidelines), Utaifishaji na Urejeshaji Mali (Asset Forfeiture and Recovery) pamoja na Usaidizi wa Kisheria wa Pande zote katika Masuala ya Jinai (Mutual Legal Assistance in Criminal Matters) kwa Waendesha Mashtaka na Wapelelezi. Lengo la Miongozo hii ni kuwawezesha waendesha Mashtaka na Wapelelezi kuwa na uelewa wa kutosha wa Sheria ya Ulinzi wa Mashahidi, Urejeshaji na Utaifishaji Mali pamoja na ushughulikiaji wa maombi ya usaidizi wa kisheria wa pande zote katika masuala ya jinai. (ii) Majalada makubwa ya rushwa yapatayo 15 yamepitiwa katika mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam. Katika mapitio hayo majalada manne (4) upelelezi wake umekamilika, 77 Majalada Saba (7) upelelezi haujakamilika na hivyo yalirudishwa TAKUKURU kwa ajili ya kuyafanyiwa kazi maeneo ambayo yalikuwa na upungufu na kukamilisha upelelezi kabla ya kuyasajili mahakamani, Majalada matatu (3) ushahidi wake ulionekana umetokana na mlolongo mmoja katika utendaji wa makosa hayo na hivyo chombo chunguzi kilielekezwa kuyaunganisha majalada hayo na kuwa jalada moja na jalada moja (1) lilifungwa. Aidha, katika zoezi hili, Mkurugenzi wa Mashtaka aliweka notisi mbili za zuio la mali “Prohibitory Notice”. (iii) Majalada 14 yamepitiwa kuhusu maombi ya msaada wa kukusanya ushahidi kutoka nje. Lengo la mapitio hayo ni kuratibu ukusanyaji wa ushahidi, kuchambua nyaraka zilizowasilishwa na kuangalia kama zimekidhi vigezo na masharti ya ushahidi kutoka nchi zilizoomba. (iv) Maombi saba (7) ya kuzuia mali (restrained application) yameandaliwa na kusajiliwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya. Katika mkoa wa Dar es Salaam maombi matatu (3) yalisajiliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, maombi mengine matatu (3) yalisajiliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza na ombi moja (1) lilisajiliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya. 78 Aidha katika zoezi hili, Mkurugenzi wa Mashtaka ameweka notisi mbili (2) za zuio (prohibitory notice). (v) Mwongozo wa Kubadilishana Taarifa za Kutambua Magenge ya Uhalifu umeandaliwa. Mwangozo huo, utatumiwa na wachunguzi na waendesha mashtaka katika kutambua na kubaini magenge ya uhalifu ili kujenga mfumo bora ya kukabiliana nayo kwa mbinu za kisasa. (aa) Kuboresha Utendaji na Maendeleo ya Rasilimaliwatu iliyo chini ya Wizara I. Wizara ya Katiba na Sheria 131. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kushughulikia na kuratibu upatikanaji wa watumishi kulingana na mahitaji, ambapo katika kipindi cha mwezi Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 watumishi 18 wamepokelewa kutoka kwenye Taasisi mbalimbali, wakiwemo Maafisa Sheria 12, Wachumi wanne (4) na kada nyinginezo (2). Hivyo, kufikia mwezi Aprili, 2024 Wizara ina jumla watumishi 138 wa kada mbalimbali kati ya watumishi 182 wanaohitajika kwa mujibu wa tathmini ya kazi (Job List). Upungufu mkubwa wa watumishi bado upo kwenye kada ya Wanasheria (20), Wachumi (13) na Wakaguzi wa Ndani (3). Jitihada za kufuatilia upatikanaji wa watumishi wanaohitajika zinaendelea kufanyika. Pia, 79 watumishi watatu (3) waliteuliwa kwenye nafasi za uongozi. Vilevile, watumishi 24 wameshiriki mafunzo wakiwemo 5 mafunzo ya muda mrefu na 19 mafunzo ya muda mfupi. Pia, watumishi 45 wameshiriki mafunzo ya ndani. II. Mahakama ya Tanzania 132. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2024, Mahakama ya Tanzania ina jumla ya Watumishi 5,666. Aidha, katika Mwaka wa Fedha 2023/2024, Mahakama ya Tanzania imewezesha watumishi 119 kushiriki mafunzo ya muda mrefu na watumishi 1,848 wameshiriki mafunzo ya muda mfupi. III. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali 133. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ina jumla ya Watumishi 177. Kati ya watumishi waliopo 177, Watumishi 106 ni kada ya Mawakili ya Serikali na Watumishi 71 ni Watumishi wa kada nyingine. Katika kipindi kuanzia Julai, 2023 hadi Aprili, 2024, Watumishi 38 walithibitishwa kazini, Mtumishi mmoja (1) aliajiriwa, Watumishi wawili (2) waliteuliwa kuwa Wakurugenzi Wasaidizi, Watumishi 13 wamepatiwa mafunzo ya muda mrefu na Watumishi 112 walipatiwa mafunzo ya muda mfupi. 80 IV. Ofisi ya Taifa ya Mashtaka 134. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeendelea kutekeleza masuala mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya rasilimaliwatu. Hadi kufikia Aprili, 2024 Ofisi ilikuwa na jumla ya watumishi 943 kati ya hao, Mawakili wa Serikali ni 663, Makatibu Sheria ni 123 na kada nyingine ni 157. Kati ya watumishi hao, watumishi 37 ni ajira mpya ambao wameajiriwa katika kipindi hiki (Makatibu Sheria 36 na Mtakwimu 1) waliohama 5 na kuhamia 4. Aidha, Ofisi imethibitisha kazini watumishi 231, na kuratibu mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi kwa watumishi 40 Mafunzo ya muda mrefu na watumishi wanne (4) mafunzo ya muda mfupi. V. Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali 135. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili, 2024 Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ina jumla watumishi 238. Kati ya watumishi waliopo Mawakili wa Serikali wapo 125, Makatibu Sheria wapo 18 na watumishi wa kada nyingine wapo 95. Aidha, watumishi watano (5) wameteuliwa katika nafasi za uongozi na watumishi nane (8) wameajiriwa katika masharti ya kudumu na malipo ya pensheni. Vilevile, watumishi 11 walihudhuria mafunzo ya muda mrefu na watumishi 56 walihudhuria mafunzo ya muda mfupi 81 VI. Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania 136. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2024 Tume ilikuwa na jumla ya Watumishi 54 wa fani mbalimbali. Aidha, katika kipindi husika watumishi 11 walihamia, mtumishi mmoja (1) aliajiriwa kwa masharti ya kudumu na nafasi mbili (2) za uongozi zilijazwa. VII. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora 137. Mheshimiwa Spika, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ina jumla ya watumishi 144. katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili, 2024 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliajiri watumishi 10 na watumishi wawili (2) walithibitishwa kazini. Pia, watumishi 13 walithibitishwa katika vyeo, watumishi 144 walipata mafunzo ndani ya nchi, watumishi wawili (2) walihama na watatu (3) walistaafu utumishi. VIII. Tume ya Utumishi wa Mahakama 138. Mheshimiwa Spika, Sheria ya Usimamizi wa Mahakama, Sura ya 237 vifungu vya 14(1) na 29(1) vimeainisha majukumu ya Tume ya Utumishi wa Mahakama, ikiwa ni pamoja na uteuzi, ajira, masuala ya nidhamu na maadili kwa MaafiMahama na. 82 139. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024; Tume ilimshauri Mheshimiwa Rais juu ya Uteuzi wa Majaji 21 wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Msajili Mkuu wa Mahakama na Msajili wa Mahakama Kuu. Pia, katika kuimarisha utendaji wa Mahakama, Tume ilimteua Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Naibu Wasajili 30, Katibu wa Jaji Mkuu na kuwathibitisha katika vyeo viongozi 43. Aidha, iliwathibitisha kazini watumishi 204 wakiwemo Mahakimu Wakazi 19 na kupandishwa vyeo Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo 211. Tume imeratibu kibali cha ajira mbadala kwa watumishi wa Mahakama 112 za Kada mbalimbali. IX. Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini 140. Mheshimiwa Spika, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) una jumla ya watumishi 211 ikilinganishwa na Watumishi 342 wanaohitajika hivyo kuna upungufu wa watumishi 131. Katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 Wizara kupitia RITA imepandisha vyeo watumishi wawili (2), imewathibitisha watumishi 16 kwenye vyeo, watumishi 113 walipatiwa mafunzo ikiwemo watumishi 105 mafunzo ya muda mfupi na watumishi nane (8) mafunzo ya muda mrefu. Aidha, watumishi 11 walihamia katika Wakala, watumishi saba (7) walihamishwa kwenda kwenye Taasisi nyingine za Serikali na watumishi wawili (2) wamestaafu kwa mujibu wa sheria. 83 X. Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania 141. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia Julai 2023 hadi Aprili, 2024 Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania ilipata kibali cha kuajiri watumishi saba (7) wa kada mbalimbali na kuwasilishwa Sekretarieti ya Ajira kwa hatua zaidi. Wizara inaendelea kufuatilia suala hili. Aidha, Mtumishi Mmoja (1) amepata uteuzi, sita (6) walihamia na 14 walihudhuria mafunzo ya muda mrefu na mfupi. XI. Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto 142. Mheshimiwa Spika, Katika Kipindi cha Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 Chuo kina jumla ya watumishi 109, watumishi 64 ni wanaume, sawa na asilimia 58.7 na watumishi 45 ni wanawake, sawa na asilimia 41.3. Aidha; katika kipindi cha julai hadi Aprili, 2024, watumishi 6 ni ajira mpya, mtumishi 1 amethibitishwa kazini, watumishi 22 wamethibitishwa kwenye vyeo, mtumishi mmoja (1) ameteuliwa, watumishi watano (5) wamehamia, watumishi saba (7) wamehama, mtumishi mmoja (1) amestaafu. Aidha, jumla ya watumishi 91 wamepata mafunzo, kati ya hao watumishi 84 wamepta mafunzo ya muda mfupi na watumishi saba (7) wanaendelea na mafunzo ya muda mrefu. 84 G. CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA NA MIKAKATI YA KUKABILIANA NAZO 143. Mheshimiwa Spika, licha ya mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa majukumu, Wizara ya Katiba na Sheria na taasisi zake ilikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo: (i) Uhaba na uchakavu wa ofisi na makazi hususan katika Mahakama za Mwanzo na Wilaya; (ii) Kuongezeka kwa uhitaji wa huduma za kisheria ikilinganishwa na uwezo rasilimali fedha na watumishi; (iii) Kuongezeka kwa makosa yanayotokana na uhalifu kwa njia ya mtandao ikilinganishwa na uwezo wa kuyabaini. (iv) Gharama kubwa za kuendesha mashauri ya nje ya nchi ikilinganishwa na bajeti iliyotengwa jambo ambalo linasababisha kuomba kupatiwa fedha nje ya bajeti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali; na (v) Upungufu wa Mawakili wa Serikali wenye ubobezi katika maeneo ya gesi, mafuta, uwekezaji, anga, madini, uchumi wa buluu, na maeneo mengine ya kimkakati hali inayosababisha kupungua kwa 85 ufanisi katika uendeshaji, usikilizwaji wa kesi na upekuzi wa mikataba. 144. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto zilizotajwa, Wizara kwa kushirikiana na taasisi zake imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na: (i) Kuendelea kuboresha miundombinu ya Mahakama kulingana na Mpango wa Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Mahakama; (ii) Kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za kisheria na upatikanaji haki; (iii) Kuendelea kuwapatia mafunzo endelevu wataalamu wa Sekta ya Sheria ili kukabiliana na makosa yanayotendeka kwa kutumia teknolojia za kisasa hususan TEHAMA; (iv) Kuimarisha matumizi ya utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala pamoja na kutumia TEHAMA ili kupunguza ushughulikiaji wa mashauri kwa kukutana ana kwa ana; na (v) Kuwajengea uwezo Mawakili kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na mfupi katika maeneo maalum ya kimkakati. 86 H. MPANGO NA BAJETI YA WIZARA NA TAASISI ZAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 (a) Vipaumbele vya Wizara 145. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 Wizara na Taasisi zake itaendelea kuboresha utoaji wa huduma za kisheria na utoaji haki kwa umma ili kuendana na Mipango ya Sekta ya Sheria nchini; na Mipango ya Kikanda na Kimataifa ili kufikia malengo yaliyopangwa kwa kipindi husika. Katika kufikia azma hiyo maeneo mahsusi ya kipaumbele yameainishwa ambayo ni: (i) Kutunga Sera ya Taifa ya Haki Jinai; (ii) Kushughulikia masuala ya kikatiba ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya Katiba na Uraia kwa Umma; (iii) Kusimamia mfumo wa haki na utoaji haki ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya Mahakama, kuharakisha mashauri ya kawaida na kumaliza mashauri ya muda mrefu; (iv) Uandishi wa sheria ikiwa ni pamoja na Kuandaa Toleo la Sheria Ndogo zilizofanyiwa urekebu mwaka 2025 na kuimarisha Marejeo na Ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mikataba iliyosainiwa; (v) Kuendesha mashtaka ya jinai Kuimarisha utenganishaji wa shughuli za Mashtaka na 87 Upelelezi; (vi) Kushughulikia uendeshaji wa mashauri ya madai na usuluhishi wa migogoro ya kibiashara, sheria za kimataifa na mikataba; (vii) Kuwezesha uanzishwaji wa Kituo cha Usuluhishi wa Migogoro (viii) Kuwezesha Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria kuanza kutekeleza majukumu yake (ix) Kuratibu masuala ya haki za binadamu, utawala bora na utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia; (x) Kuimarisha usajili wa matukio muhimu ya binadamu pamoja na usajili na ufilisi katika Mikoa yote ya Tanzania Bara; (xi) Kuratibu tathmini na maboresho ya sheria ikiwa ni pamoja na Kufanya Mapitio ya Mifumo wa Sheria inayosimamia Elimu, Michezo ya Kubahatisha, Adhabu ya kifo na Kifungo cha Maisha na Kufanya Utafiti wa Mfumo wa Sheria Unaosimamia Utatuzi wa Migogoro ya Kibenki na Taasisi za fedha; (xii) Kuratibu ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa sheria za utajiri asili na maliasilia za nchi; (xiii)Kushughulikia urejeshwaji wa wahalifu na masuala ya ushirikiano wa kimataifa kwenye makosa ya jinai; (xiv) Kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji haki na huduma za kisheria; na 88 (xv) Kuboresha utendaji na maendeleo ya rasilimali watu ya Wizara na taasisi zake ikiwemo ajira, uteuzi, nidhamu na maadili. (b) Kazi Zitakazotekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 146. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa, baadhi ya kazi zitakazotekelezwa na Wizara ya Katiba na Sheria (Fungu 41) katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 ni pamoja na:- (i) Kutayarisha Sera ya Haki Jinai na Mkakati wa Utekelezaji wa Sera hiyo; (ii) Kuandaa na kutekeleza mkakati wa kulinda haki za binadamu na watu; (iii) Kuandaa taarifa za utekelezaji wa Mikataba miwili (2) ya Haki za Binadamu ambayo Serikali imeridhia; (iv) Kuratibu Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu wa Mapitio Katika Kipindi Maalum (UPR); (v) Kutekeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia; (vi) Kuanzisha na kuratibu madawati ya Huduma za Msaada wa Kisheria ngazi ya kitaifa na kijamii; 89 (vii) Kushughulikia maombi ya kuongezewa muda wa kufungua mashauri ya madai nje ya muda wa ukomo mahakamani; (viii) Kuandaa mikataba ya kuwarejesha wahalifu watoro kwenye nchi walikofanya uhalifu; (ix) Kuratibu tafsiri ya Sheria 161 kutoka lugha ya Kiingereza kwenda lugha ya Kiswahili; (x) Kuwezesha uanzishwaji na uendeshaji wa Kituo cha Taifa cha Usuluhishi wa Migogoro kwa njia mbadala Tanzania; (xi) Kuimarisha mifumo ya Sheria na Kanuni za Utatuzi wa Migogoro kwa njia mbadala; (xii) Kuratibu na kuwezesha Mapitio ya Sheria 20 zinazohusu Haki jinai; (xiii) Kusajili mikataba 30 ya Utajiri asili na maliasilia za nchi ambazo Wizara, Idara na Taasisi za Serikali zimeingia na wawekezaji; (xiv) Kukamilisha Mkakati wa Kitaifa wa utekelezaji wa Sheria za Utajiri asili na Maliasilia za Nchi Sura 449 na 450; 90 (xv) Kutoa uelewa kuhusu Sheria za Utajiri asili na maliasilia za Nchi Sura 449 na 450 kwa Mawaziri 10, Makatibu Wakuu 10, Wakurugenzi wa halmashauri 50, Maafisa Viunganishi 15 na Wawakilishi wa Wananchi 100 katika mikoa mitano (5) ya Tanzania Bara; (xvi) Kufanya tathmini ya utekelezaji wa Sheria za Utajiri asili na Maliasilia za Nchini Sura 449 na 450 katika Mikoa mitano (5) yenye uwekezaji mkubwa wa utajiri asili na maliasilia za Nchi; (xvii) Kutoa mafunzo kwa Halmashauri 50 za Wilaya kuhusu utawala bora kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; (xviii) Kufanya tathmini ya uelewa wa wanafunzi kuhusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika Taasisi 10 za elimu; (xix) Kufanya ziara katika magereza 20 na vizuizi 20 katika vituo vya polisi ili kutathmini uzingatiwaji wa utoaji haki; (xx) Kutoa Elimu ya Katiba na Uraia kwa Umma Katika Halmashauri 184; 91 (xxi) Kutoa mafunzo kwa Askari Polisi na Magereza kuhusu utoaji wa huduma za kisheria katika maeneo ya vizuizi; (xxii) Kuendeleza, kuboresha na kufungamanisha mifumo ya kielektroniki ya utoaji haki katika Sekta ya Sheria; (xxiii) Kuanzisha na kuendesha Mfuko wa Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi; (xxiv) Kutoa mafunzo ya uanasheria kwa vitendo kwa wanafunzi 1,500; (xxv) Kusajiri na kutoa vyeti kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano; (xxvi) Kuratibu na kusimamia usajili wa matukio muhimu ya binadamu ikiwemo vizazi, vifo, ndoa, talaka na watoto wa kuasili; na (xxvii) Kuratibu na kusimamia ufilisi na udhamani ikiwemo kutoa elimu ya wosia kwa umma. 147. Mheshimiwa Spika, baadhi ya kazi zitakazotekelezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama (Fungu 12) katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 ni pamoja na:- 92 (i) Kuendesha na kusimamia zoezi la usaili baada ya kupata kibali cha Ajira kutoka ORUTUMISHI; (ii) Kusimamia zoezi la Uteuzi kwa Watumishi wa Mahakama; (iii) Kutoa mafunzo kwa Kamati za Maadili za Mikoa na Wilaya; (iv) Kuendesha vikao vya mashauri na nidhamu; (v) Kufanya ziara kwa ajili ya kutoa elimu kwa Umma kuhusu majukumu ya Tume na Kamati za Maadili za Mikoa na Wilaya; (vi) Kutoa elimu kwa umma kupitia Vyombo vya habari na matukio mbalimbali; na (vii) Kuendelea kuimarisha Mifumo ya Ajira, Nidhamu na Maadili kwa watumishi wa Mahakama. 148. Mheshimiwa Spika, baadhi ya kazi zitakazotekelezwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Fungu 16) katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 ni pamoja na: (i) Kufanya urekebu wa Sheria Ndogo; (ii) Kutoa Toleo la Sheria Ndogo zilizofanyiwa Urekebu la Mwaka 2025; 93 (iii) Kuanza na kukamilisha tafsiri ya sheria 188 za Awamu ya Pili. (iv) Kutoa elimu kwa Viongozi wa Umma kuhusu matumizi sahihi ya Sheria zinazowagusa moja kwa moja mfano: Sheria ya Tawala za Mikoa, Sura ya 97; Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Wilaya), Sura ya 287; na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Miji), Sura ya 288 (v) Kufanya uchambuzi wa masuala ya Sheria yanayoleta changamoto kwa wananchi mara kwa mara mfano: migogoro ya matumizi na umiliki wa ardhi na mirathi n.k.; (vi) Kufanya Marejeo ya Mikataba ya Nishati na Rasilimali za Nchi yakiwemo Madini kwa kuainisha athari zinazohusiana na Mikataba husika ili kusaidia kutengeneza mpango wa kushughulikia athari hizo; (vii) Kufanya Ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mikataba iliyosainiwa; (viii) Kuunganisha Mfumo wa OAG-MIS na Mifumo mingine kama vile Mfumo wa Kesi wa Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka; na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA); 94 (ix) Kuwajengea uwezo Watumishi kwa kuwapatia mafunzo katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mikataba, Uandishi wa Sheria, Ushauri wa Kisheria, Uchumi, Fedha na Utawala; (x) Kufanya Majadiliano ya Mikataba ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa kwa kushiriki majadiliano ya mikataba ya Kimataifa na Kushiriki Mikutano ya Kikanda na Kimataifa. (EAC; SADC; Joint Commission Meetings; AU; (UN); na Vikao vya Bilateral na Multilateral; (xi) Kumaliza ujenzi wa jengo la Mkoa wa Mwanza na kuendelea na ujenzi wa jengo la Mkoa wa Arusha; na (xii) Kukusanya takwimu na taarifa muhimu kuhusu aina za uhalifu zinazotendeka, maeneo yanayokumbwa na uhalifu, na mifumo ya uhalifu inayotumiwa. 149. Mheshimiwa Spika, baadhi ya kazi zitakazotekelezwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (Fungu 19) katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 ni pamoja na:- (i) Kuiwakilisha serikali kwenye mashauri ya kikatiba, haki za binadamu, uchaguzi na mashauri yote ya kimataifa; 95 (ii) Kuiwakilisha serikali kwenye mashauri ya usuluhishi ndani na nje ya nchi; (iii) Kuiwakilisha serikali kwenye kesi za madai na usuluhishi za kimataifa; (iv) Kuendelea kuboresha mfumo wa kielektroniki wa utunzaji wa taarifa za mashauri; (v) Kuendelea kiboresha ofisi za Wakili Mkuu wa Serikali katika mikoa; (vi) Kuendelea kuhamasisha matumizi ya njia mbadala za utatuzi wa migogoro; na (vii) Kusimamia, kufuatilia na kupitia taratibu za uendeshaji wa mashauri ya madai na usuluhishi. 150. Mheshimiwa Spika, baadhi ya kazi zitakazotekelezwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (Fungu 35) katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 ni pamoja na:- (i) Kuendelea na uendeshaji wa kesi za jinai; (ii) Kushughulikia malalamiko yanayohusu haki jinai kwa wakati; (iii) Kufanya ukaguzi katika maeneo yanayohifadhi mahabusi na wafungwa; (iv) Kufanya vikao mbalimbali na vyombo chunguzi; 96 (v) Kuhuisha miongozo mbalimbali kwa lengo la kuharakisha upelelezi; (vi) Kuendelea kufungua Ofisi za Wilaya kwenye Wilaya ambazo hazina Ofisi; (vii) Kuendesha mashauri ya utaifishaji wa mali zinazotokana na uhalifu; (viii) Kutayarisha programu mbalimbali za utoaji elimu kwa jamii juu ya utaifishaji na urejeshwaji wa mali zinazotokana na uhalifu; (ix) Kutoa ushirikiano katika kukusanya ushahidi na kusafirisha mashahidi na wahalifu; (x) Kushiriki katika mikutano ya kamati mbalimbali za uanachama wa Mamlaka mbalimbali zinazohusika na uendeshaji wa mashauri ya jinai; na (xi) Kuendelea na ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Mashtaka katika Mikoa na Wilaya. 151. Mheshimiwa Spika, baadhi ya kazi zitakazotekelezwa na Mfuko wa Mahakama (Fungu 40) katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 ni pamoja na:- (i) Kutatua mashauri ya kawaida na kumaliza mashauri ya muda mrefu (backlog); (ii) Kuimarisha uwezo katika Ukaguzi na usimamizi wa shughuli za Mahakama; (iii) Kujenga na kukarabati majengo ya Mahakama katika ngazi mbalimbali; 97 (iv) Kuboresha mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kama nyenzo muhimu ya kuboresha utoaji wa huduma; (v) Kuongeza ushirikiano na wadau wa haki jinai ili kuharakisha huduma ya utoaji haki; na (vi) Kuimarisha maendeleo ya rasilimali watu, ikiwa ni pamoja na mafunzo, na nidhamu kwa watumishi. 152. Mheshimiwa Spika, baadhi ya kazi zitakazotekelezwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (Fungu 55) katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 ni pamoja na:- (i) Kufanya utafiti wa namna Mamlaka ya Serikali za Mitaa zinavyoendesha shughuli zao katika kuzingatia haki za binadamu na misingi ya utawala bora; (ii) Kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora; (iii) Kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara; (iv) Kupokea na kushughulikia malalamiko kuhusu masuala ya uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora; (v) Kutoa ushauri wa kisheria kwa Serikali kuhusu Sheria, Miswada na Kanuni kuhusu uzingatiaji wa Haki za Binadamu na Misingi 98 ya Utawala Bora. (vi) Kufungua ofisi ya Tume katika Mkoa wa Tabora; (vii) Kufanya ufuatiliaji na kutathmini hali ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi wa Mkuu 2025; (viii) Kufanya ukaguzi wa magereza, vituo vya polisi na maeneo mengine ya vizuizi ili kutathimini hali ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora; (ix) Kuratibu mahusiano na wajibu wa Tume katika Taasisi za Kimataifa na Kikanda za Haki za Binadamu na Utawala Bora. 153. Mheshimiwa Spika, baadhi ya kazi zitakazotekelezwa na Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (Fungu 59) katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 ni pamoja na:- (i) Kufanya Mapitio ya Mfumo wa Sheria Unaosimamia Elimu; (ii) Kufanya Tathmini ya Mfumo wa Sheria Unaosimamia Michezo ya Kubahatisha; (iii) Kufanya Utafiti wa Mfumo wa Sheria Unaosimamia Adhabu ya kifo na Kifungo cha Maisha; (iv) Kufanya Utafiti wa Mfumo wa Sheria Unaosimamia Utatuzi wa Migogoro ya Kibenki na Taasisi za fedha; (v) Kujenga Mfumo wa kielektroniki wa utendaji 99 kazi (LRMIS); (vi) Kuwezesha Mawakili 18 kuhudhuria Mfunzo ya Utafiti, Tathmini na Uandishi wa Sheria; na (vii) Kuendelea na Ujenzi wa Ofisi katika Mji wa Serikali-Mtumba. (c) Makusanyo ya Maduhuli 154. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Wizara na Taasisi inatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi 12,676,199,000 ikiwa ni maduhuli kama ilivyoainishwa katika Kiambatisho Na.11. (d) Makadirio ya Fedha kwa ajili ya Kutekeleza Mpango na Bejeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 155. Mheshimiwa Spika, ili kufanikisha utekelezaji wa vipaumbele vilivyoainishwa, Wizara inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 441,260,152,000.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo. Mchanganuo wa makadirio ya bajeti kwa mafungu nane (8) ya Wizara na taasisi zake

Mbunge Oliver Semguluka, akiwasili Bungeni leo
Mbunge Sophia Mwakagenda, akiwasili bungeni leo



Waziri Mkuu  Kassim Mjaliwa, akibadilishana mawazo na wabunge  Mpembenwa na Kwagirwa ,nje ya ukumbi wa bunge leo

 

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.