Mjumbe wa Kamati ya Ushindi UWT (Nyanda za Juu Kusini) 🌿 Sophia Mwakagenda akiwa mzigoni🌿


 Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya UWT (Nyanda za Juu Kusini) 🌿 Sophia Mwakagenda , akiwa na Mgombea ubunge jimbo la Njombe mjini  Deo Mwanyika

 akiwa Katika mwendelezo wa kampeni za elimu na uhamasishaji zilizofanyika Jimbo la Njombe Mjini , Sophia Mwakagenda amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi kwa amani na umoja, kwa kumpigia kura Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , pamoja na Mhe. Deo Mwanyika, Mgombea Ubunge wa Njombe Mjini, na wagombea wote wa chama katika ngazi mbalimbali.

Amesisitiza kuwa kura ni silaha ya maendeleo na chachu ya kuendeleza amani na ustawi wa taifa, akiwataka wananchi kuendeleza imani kwa viongozi wanaothibitisha kwa vitendo dhamira ya kuwatumikia wananchi.

🤜 “Tumuunge mkono Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Mhe. Deo Mwanyika ; viongozi wanaosimamia maendeleo ya watu kwa vitendo.” alisema Mwakagenda

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA