WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHIRIKI IBADA YA KUSIMIKWA ASKOFU

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza Mwangalizi Mkuu wa Kanisa la Wabaptist Tanzania Askofu Arnold Manase Molell, mara baada ya kusimikwa kuwa Askofu na Mwangalizi Mkuu wa Kanisa hilo, katika viwanja vya Baptist Seminary Ngaramtoni Arusha. Novemba 6,2022. (

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waumini wa Kanisa la Baptist Tanzania, makati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ibada maalum ya kumsimika Askofu Mteule na Mwangalizi Mkuu wa Kanisa hilo, katika viwanja vya Baptist Seminary Ngaramtoni Arusha. Novemba 6,2022.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea Tuzo ya Heshima kwa Niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua mchango wake katika kuwatumikia Watanzania, Tuzo hiyo imetolewa na kanisa la Wababtist Tanzania na kukabishiwa na Mwangalizi Mkuu wa Kanisa la Wabaptist Tanzania Askofu Arnold Manase Molell, katika viwanja vya Baptist Seminary Ngaramtoni Arusha. Novemba 6,2022.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mwangalizi Mkuu wa Kanisa la Wabaptist Tanzania Askofu Arnold Manase Molell, wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ibada maalum ya kumsimika Askofu Mteule na mwangalizi Mkuu wa Kanisa hilo, katika viwanja vya Baptist Seminary Ngaramtoni Arusha. Novemba 6,2022.

Askofu Mstaafu wa Kanisa la Wabaptist Tanzania Harry Mwasanjala (Katikati) akiwaongoza viongozi wa Kanisa hilo Askofu Mstaafu Richard Mwaihuti (kulia) na Mchungaji wa Kanisa la Baptist Tanzania Mkoa wa Tanga, Elias Msumai kumsimika Askofu Mteule wa Kanisa la Wabaptist Tanzania Askofu, Arnold Manase Mollel kuwa Askofu na Mwangalizi Mkuu wa kanisa hilo, kwenye viwanja vya Baptist Seminary Ngaramtoni Arusha. Novemba 6,2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?