RIDHIWANI AENDELEA NA MIKUTANO YA KAMPENI JIMBONI KWAKE

Kampeni zimeendelea kata ya Kiwangwa ambapo Mgombea Ubunge Wa CCM jimbo la Chalinze Ndg. Ridhiwani Kikwete amenadi Ilani ya CCM ya Mwaka 2025/30 ambapo pia amemuombea kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Samaha na Diwani wa kata hiyo Ndugu Malota Hussein Kwaga.

Katika mikutano hiyo, mgombea Ubunge wa Chalinze ndg. Ridhiwani Kikwete alimuelezea Dr. Samia kuwa ni mtu mwenye maono na mwanamapinduzi wa kweli ambaye amefanikisha yale ambayo wengi walidhani yasingewezekani. Amefanikisha usambazaji wa Umeme Chalinze kwa vijiji vyote na vitongoji zaidi ya asilimia 75, maji zaidi ya asilimia 94, Elimu bure,kilimo na mengineyo mengi.  Kampeni zinaendelea katika jimbo la Chalinze.# KaziNaUtuTunasongaMbele




 

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.