MWAMBEGELE ATEMBELEA VITUO VYA KUPIGIA KURA NCHINI
KATAVI UCHAGUZI OKTOBA 27, 2025
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, MHE. JAJI WA RUFANI JACOBS MWAMBEGELE ametembelea na kujionea maandalizi ya ujenzi wa vituo 83 kati ya 90 vya Wapiga Kura vilivyotengwa maalum kwaajili ya wakazi wa zilizokuwa Kata za Ilangu, Ipwaga, Bulamata na Mishamo zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi ambazo zilifutwa na Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura 287.
Jaji Mwambegele alitembelea eneo hilo la Kata ya Tongwe katika Kitongoji cha Luhafwe akiwa ameambatana na Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Katavi, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tanganyika na watendaji wengine wa uchaguzi kuangalia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliopangwa kufanyika Oktoba 29, 2025 nchini kote.
Baada ya kujionea maandalizi hayo ya Uchaguzi Mkuu

Comments
Post a Comment