WADAU WA ELIMU WAKUTANA JIJINI DODOMA KUJADILI MAGEUZI YA SEKTA HIYO


Serikali ya Awamu ya Sita chini  imepiga hatua kubwa katika mageuzi ya sekta ya elimu nchini, baada ya kutangaza rasmi kuwa elimu ya lazima sasa itakuwa miaka 10 kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.


Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata fursa sawa ya kujifunza, kukuza maarifa na kupata ujuzi utakaomwezesha kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.


Akizungumza  Oktoba 22, 2025, jijini Dodoma katika mkutano wa mwaka wa tathmini ya pamoja ya sekta ya elimu, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, Prof. Daniel Mushi (pichani juu), alisema kuwa maboresho hayo makubwa yatahitaji ushirikiano wa karibu kati ya serikali, wadau wa elimu na jamii kwa ujumla.


“Mageuzi haya ni ya kimkakati. Tunataka elimu ya lazima iwe jumuishi, yenye ubora na inayomwandaa mwanafunzi kuwa mbunifu na mwenye mchango chanya katika maendeleo ya taifa. Tunatambua ipo haja ya kuongeza miundombinu, walimu na sera shirikishi,” amesema Prof. Mushi.



Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Sylvia Lupembe (kushoto), akiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya wanafunzi wakishiliki katika mkutano huo








 

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA