DODOMA WASEMA AMANI KWANZA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rose-Mary Senyamule, akiongoza Matembezi ya Kuhamasisha Amani na kuliombea Taifa, matembezi hayo yalianza leo asubuhi Lango la Bunge Mkabala na Shule ya Sekondari Dodoma hadi viwanja vya Nyerere Square. Matembezi hayo pia yaliambatana na uchunguzi wa matibabu ya magonjwa ya Moyo, Macho, Figo, Saratani na Selimundo. Uchunguzi huo uliendeshwa na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa wakiongozwa na Mkurugenzi wake Profesa Abel Makubi..Makundi yote ya jumuiya ya Wanadodoma yakiongozwa na viongozi wake au wawakilishi wao kila aliyesimama alikuwa akiomba uchaguzi Mkuu uwe wa amani, bila amani hakitafanyika kitu. Akihitimisha Mkuu wa Mkoa alisema Serikali ipo makini wananchi mtoe taarifa kama kuna mtu au kikundi cha watu watakachokibaini kwamba kinataka kuhatarisha amani ili washugulike naye serikali imejipanga ipo makini na wasithumubu chamoto watakiona watakaothubutu, alibainisha Senyamule.
Comments
Post a Comment