Posts

WAZIRI MWAKYEMBE AFANYA ZIARA TCAA DAR

Image
Waziri wa Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe akisaini kitabu cha wageni wakati alipofanya  ziara ya kikazi katika Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wanafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA.Wapili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Mbwana Mbwana.Kulia ni makamu Mwenyekiti Weggoro Nyamajeje na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya TCAA ,Charles Chacha. Waziri Dk. Harrison Mwakyemba ndiyo wazili pee  aliyetembelea ofisi hizo tangua kuanzishwa.  Waziri wa Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (kulia)akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Ndege wa Mamlaka Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Nuis Kasambala alivyokuwa akimuelezea na kumuonyesha jinsi wanavyofanya mitihani kwa wanafunzi wa ndege  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuonge...

MGOSI WA SUI KWA KUBOMU

Image
Nikiikala hapa ku Daresalama, ninawaombea watoto wote wazuri na wabaya nyote sikukuu nyema yenye furaha na upendo. Hivi sasa naalikaga kutayarishaga singo yangu mupya mupya kabisa kkwa ajiliri ya Iddi hii, lakini produza   akasemaga ana makazi bwereree ya kina Dayamond na Omi Dimpoz hivyo singo yangu itatokaga kunako mwezi wa kenda. Haina neon lakini Iddi njema ku watoto nyote. Hivii unayesomaga huu ujumbe unaweza kunipaga hata kafaranga  laki moja hivi ya chaiii ya Idd  bandugu fanyeni wema kidogo tu mutapataga swawabu  kwa mungu. hakunaga mayele

AJIRA ZA UHAMIAJI ZAZUA JAMBO

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi  Mbarak Abdulwakil (kulia) akisalimiana na Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (DIGP) Abdulrahman Kaniki (kulia)  Uhamiaji waumbuka Serikali yafuta ajira mpya Yaunda kamati kuchunguza maofisa wake kwa madai yta rushwa ya ajira ya usaili  20,000 Uwanja wa Taifa SERIKALI imetangaza kufuta ajira mpya za maofisa wa Idara ya Uhamiaji, baada ya kuibuka kwa tuhuma za nafasi hizo kupewa watoto na ndugu wa vigogo wa idara hiyo kinyume na sheria. Mapema mwaka huu, idara hiyo ilitangaza nafasi ya kazi ambapo vijana zaidi ya 20,000 waliomba nafasi hizo na 10,700 ndio waliochaguliwa na kufanyiwa usaili wa awamu ya kwanza katika Uwanja wa Taifa. Katika tangazo lililotolewa awali, watu waliokuwa wakihitajika kwa ajili ya nafasi hizo ni 70 tu. Hata hivyo, baada ya usaili waliochaguliwa walikuwa 200. Baada ya kutangazwa kwa walioshinda nafasi hizo, zilitolewa tuhuma kuwa zaidi ya asilimia 90 ya waliopata ajira ...

VIKWAZO KWA URUSI KUWA JANGA KWA MABILIONEA

Image
Bilionea Alisher Usmanov akiwa na mkewe Irina   Bilionea wa Urusi Roman Abramovich, akiwa na rafiki yake  Dasha Zhukova Vikwazo vyawatisha mabilionea wa Urusi. ROHO za mabilionea wa Urusi ziko juu kwa uwezekano wa kuwekewa vikwazo vitakavyoporomosha si tu uchumi wao bali pia wa   taifa hilo. Uwezekano huo unatokana na mjadala unaoendelea katika mataifa ya Magharibi yasiyofurahishwa na ushiriki wa Moscow katika machafuko yanayoendelea mashariki mwa Ukraine. Mabilionea hao wana neno kuhusu uwezekano huo hata nini cha kufanya ili kuviepuka, lakini wanamgwaya Rais wa Urusi Vladimir Putin, hivyo kushindwa kuzungumza waziwazi. Marekani tayari imeweka mlolongo wa vikwazo dhidi ya kampuni za Urusi na mtu mmoja moja huku Uingereza na Uholanzi zikiongoza ajenda katika Umoja wa Ulaya (EU) juu ya vikwazo vikali zaidi kufuatia kuangushwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia, MH17. Wataalamu wa fedha wanaonya kuwa vikwazo vya ziada dhidi ya Urusi ...

VIOONGOZI IMTU KIZIMBANI DAR

Image
  Baadhi ya viongozi wa juu wa Hospitali  na Chuo cha Udaktari cha IMTU, wakiwa chini ya ulinzi wa askari  katika Mahakama ya Kinondoni jijini Dar es Salaam jana kusomewa mashtaka ya kutupa viungo vya binadamu hadharani. Kutoka kushoto ni  Venkat Subbaiah,  Appm Shankr,  Prabhakar  Rao na  Dinnesh Kumar.   VIONGOZI wanne wa Chuo Kikuu cha Tiba na Teknolojia (IMTU), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, mjini Dar es Salaam jana, wakikabiliwa na mashtaka mawili. Viongozi hao ambao ni raia wa India, ni Venkat Subbaiah (57), Appm Shankar (64), Prabhakar Rao (69) na Dinnesh Kumar (27). Wakisomewa makosa hayo mbele ya Hakimu Kwey Rusema, Wakili wa Serikali, Magoma Mtani, alidai tukio hilo lilitokea Julai 20, mwaka huu, katika eneo la bonde la Mpiji Majohe, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Wakili Magoma alidai katika kosa la kwanza, washtakiwa wote wanakabiliwa na shtaka la kushindwa kuhifadhi miili ya binad...

RAIS AFUTURISHA YATIMA, WALEMAVU WA NGOZI NA WATOTO WAISHIO KATIKA AMZINGIRA MAGUMU DSM

Image
  Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa meza kuu  na viongozi wa vituo mbalimbali vya yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakati wa futari  aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Juma...