AJIRA ZA UHAMIAJI ZAZUA JAMBO
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil (kulia) akisalimiana na Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (DIGP) Abdulrahman Kaniki (kulia)
Uhamiaji waumbuka
Serikali yafuta ajira mpya
Yaunda kamati kuchunguza maofisa wake
kwa madai yta rushwa ya ajira ya usaili 20,000
Uwanja wa Taifa
SERIKALI imetangaza kufuta ajira mpya za maofisa wa
Idara ya Uhamiaji, baada ya kuibuka kwa tuhuma za nafasi hizo kupewa watoto na
ndugu wa vigogo wa idara hiyo kinyume na sheria.
Mapema mwaka huu, idara hiyo ilitangaza nafasi ya kazi
ambapo vijana zaidi ya 20,000 waliomba nafasi hizo na 10,700 ndio
waliochaguliwa na kufanyiwa usaili wa awamu ya kwanza katika Uwanja wa Taifa.
Katika tangazo lililotolewa awali, watu waliokuwa
wakihitajika kwa ajili ya nafasi hizo ni 70 tu. Hata hivyo, baada ya usaili
waliochaguliwa walikuwa 200.
Baada ya kutangazwa kwa walioshinda nafasi hizo,
zilitolewa tuhuma kuwa zaidi ya asilimia 90 ya waliopata ajira hizo wana
uhusiano wa namna moja na maofisa wa idara hiyo.
Akitangaza uamuzi huo mjini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, alisema Serikali imefikia uamuzi huo
ili kujiangalia upya na kuchukua hatua dhidi ya wahusika wote.
“Serikali
imefuta mara moja ajira zote za Uhamiaji zilizotangazwa katika ngazi ya
konstebo na koplo hivi karibuni.
Kwa msingi huo, waliotakiwa kuripoti Agosti 6 mwaka
huu wanatakiwa kusubiri hadi hapo watakapotangaziwa tena baada ya uchunguzi
kukamilika na uamuzi kufanyika,” alisema Abdulwakil.
Naye Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Isaac Nantanga, alisema pamoja na uamuzi huo, Katibu Mkuu ameunda kamati ndogo
itakayochunguza tuhuma hizo.
“Tumepokea taarifa kupitia vyombo vya habari jana
(juzi) na Katibu Mkuu ameamua kuunda kamati ambayo itafanya kazi kwa kipindi
kifupi ili kujua ukweli wa jambo hili,” alisema Nantanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya kuchaguliwa kwa maofisa hao,
pamoja na mambo mengine vigezo vilivyotumika kuwapata ni pamoja na usawa wa
kijinsia, muungano pamoja na ufaulu kwenye usaili.
Mara baada ya watu kufanya usaili kwenye uwanja huo,
baadhi ya tuhuma zilitolewa zikiwamo za rushwa na usalama mdogo.
Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Ndani ilikanusha
taarifa hizo na kusema kuwa katika uwanja huo kulikuwa na maofisa wa taasisi za
wizara hiyo kuhakikisha kuwa zoezi hilo
linafanyika kwa usalama.
Kuhusu tuhuma za rushwa, taarifa ya wizara hiyo ilisema
kuwa katika uwanja huo, kulikuwa na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (Takukuru) ili kudhibiti hali hiyo.

Kuhusu tuhuma za rushwa, taarifa ya wizara hiyo
ilisema kuwa katika uwanja huo, kulikuwa na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili kudhibiti hali hiyo.
Majina yanayodaiwa kuwa ya
ndugu waliopata upendeleo wa ajira katika idara hiyo nyeti ya serikalia ni haya
1
Abdulhaq Amin Mandemla anadaiwa kuwa mtoto wa Afisa Uhamiaji Amin Mandemla.
2
Alphonce Kishe mtoto wa Afisa Uhamiaji Aleluya Kishe
3
Asha Burhan Idd ndugu wa
Afisa Uhamiaji Tatu Burahan Idd.
4
Beatrice Temba Ndugu wa Afisa Uhamiaji Joseph Kasike
5
Geofrey Justine Mhagama ndugu wa Afisa Uhamiaji Rose Mhagama
6
Iginga Daniel Mgendi Mtoto
wa wa Afisa Uhamiaji Daniel Mgendi
7
Issack Michael Makwiya mtoto
wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Makwiya
8
John Alfred Mungulu Mtoto wa
Afisa Uhamiaji Alfred Mungulu
9
Joseph A. Milambo Mtoto wa
Karani wa Uhamiaji Milambo.
10
Michael A, Choma Mtoto wa Afisa uhamiaji John Choma
11
Shimba H. Zakayo mtoto wa
Afisa Uhamiaji Zakayo Mchele.
12
Upendo E. mgonjaMttoto wa
Afisa Uhamiaji Mgonja
13
Vaileth A. Kidesu Mtoto wa
Afisa Uhamiaji Adamu Kidesu
14
Elizabeth Edward ndugu wa Afisa Uhamiaji Edward Martin
15
Ester Mahirane Ndugu wa Afisa
Uhamiaji Mahirane
16
Basil Lucian John ndugu
wa Afisa Uhamiaji Magnus Lucian John.
17
Frank E. Kajura Ndugu wa Afisa Uhamiaji Kajura
18
Jacob P. Ulungi Ndugu wa Afisa uhamiaji Magnus Ulungi.
19
Janeth John Milinga Ndugu wa
aliyekuwa Afisa uhamiaji Milinga.
20
Janeth R. Lukuwi Ndugu wa
Afisa Uhamiaji Eliza Lukuwi
21
Joseph N. Yondani Mtoto
wa Afisa Uhamiaji Mary Yondani.
22
Leila Khatib Irovya mtoto wa
Afisa Uhamiaji Abbas Irovya
23
Lucia F. Mlula Ndugu wa Afisa
Uhamiaji Dismas Mlula
24
Neema Kassim Lukosi Ndugu wa
Afisa Uhamiaji Zubeda Abbas
25
Pendo D. Gambadu Ndugu
wa Afisa Uhamiaji Gambadu
26
Paschalia E.Mwenda Ndugu wa Martine Mwenda
27
Theresia Ernest Kalunde Mtoto
wa Ernest Kalunde
28
Veronica G. Vitalis mtoto wa
Afisa Uhamiaji Vitalis
29
Victor G. Mlay Mtoto wa
Aliyekuwa Afisa Uhamiaji Vitalis Mlay
30
Catherine J. Mapunda Mtoto wa
Afisa Uhamiaji Lucy Mapunda
Hii ni sampuli tu ya moja ya tatu tu kwani
zaidi ya asilimia 90 ni watoto na ndugu wa Maafisa Uhamiaji kama ni hivyo kusingekuwepo
na kutangaza nafasi za kazi wangekuwa wanagawiana ndani kwa ndani kama
inavyodaiwa idara nyingine nyeti ya Serikali nayo inadaiwa kufanya hivyo.
Comments
Post a Comment