AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
TAARIFA YA UTOAJI WA VIBALI VYA AJIRA KWA MWAKA
WA FEDHA 2024/25 NA MWAKA 2025/26 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Katika kuhakikisha kuwa Wizara, Idara, Taasisi za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakuwa na watumishi wa kutosha kutekeleza majukumu yake, Serikali katika kipindi cha miaka miwili ambayo ni mwaka wa fedha 2024/25 na Mwaka 2025/26, iliidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nafasi 86,500 za Ajira Mpya.
a) MWAKA WA FEDHA 2024/25
Ndugu Wanahabari; Serikali katika mwaka wa fedha 2024/25 ilitoa kibali cha nafasi 45,000 za ajira mpya kwa Taasisi mbalimbali na utekelezaji wake ulianza kuanzia tarehe 29 Aprili, 2025.
Ndugu Wanahabari; Kufuatia kutolewa kwa kibali hicho, mchakato wa kujaza nafasi hizo umefanyika na hadi sasa nafasi 30,863 zimejazwa na wahusika wamepangiwa vituo vya kazi. Aidha, nafasi 6,701 usaili umefanyika na wahusika watapangwa vituo vya kazi ndani ya Mwezi Oktoba, 2025 na nafasi 7,436 ujazaji wake utakamilika Mwezi Novemba, 2025 na wasailiwa kupangwa vituo vya kazi mwezi huo huo.
b) MWAKA WA FEDHA 2025/26
Ndugu Wanahabari; Katika mwaka wa fedha 2025/26 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliidhinishwa nafasi 41,500 za ajira mpya kwa Taasisi mbalimbali zikiwemo nafasi 12,176 za Walimu na nafasi 10,280 za kada za Afya ambapo utekelezaji wake unaanza mara moja.
Mchanganuo wa Mgawanyo wa Ajira Mpya 2025/26 Kisekta NA. SEKTA IDADI YA NAFASI ZILIZOTOLEWA
1
Elimu
12,176
2
Afya (Mamlaka za Serikali za Mtaa)
10,280
4
Kilimo
470
5
Mifugo
312
6
Uvuvi
47
7
Polisi
5,000
8
Magereza
750
9
Jeshi la Zimamoto
1,000
10
Uhamiaji
443
12
Kada Nyinginezo*
11,022 Jumla 41,500
Ninaelekeza Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kuanza mchakato wa kujaza nafasi hizi za mwaka 2025/26 pamoja na kukamilisha mchakato wa nafasi zote za Mwaka 2024/25. Ili kuhakikisha Sekretarieti ya Ajira inatekeleza jukumu hili ipasavyo, Waajiri wote wanaelekezwa kutoa ushirikiano.
Aidha, ninapenda pia kutoa maelekezo kwa Waajiri ambao Sekretarieti ya Ajira imekasimu madaraka ya uendeshaji wa mchakato wa ajira kwa baadhi ya kada, kuhakikisha wanaendesha usaili huu mara moja ili kujaza nafasi walizoidhinishiwa kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za uendeshaji wa usaili katika Utumishi wa Umma.
Ndugu Wanahabari; Kwa lengo la kuhakikisha zoezi la usaili linapunguza gharama na linafanyika kwa wakati, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inaelekezwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
i. Zoezi la usaili lifanyike kila Mkoa Tanzania Bara na vituo vilivyoandaliwa mahsusi wa upande wa Zanzibar ili kutoa fursa kwa waombaji kutoka katika maeneo husika kuomba na hatimaye kusailiwa;
ii. Waombaji watakaofaulu usaili lakini wakashindwa kupangiwa kazi baada ya usaili wawekwe katika Kanzidata na waendelee kupangiwa kazi kwa kadri nafasi za ajira mpya zitakapokuwa zinapatikana. Waombaji hawa watapangiwa kazi katika Taasisi zitakazokuwa na nafasi popote hapa nchini; na
iii. Barua za kupangiwa vituo vya kazi kwa wasailiwa watakaofualu usaili zipatikane katika “Mfumo wa Ajira Portal” kupitia akaunti za wahusika.
Ndugu Wanahabari; Mwisho ninapenda kuwashukuru kwa mwitikio wenu kila mnapoitwa na Ofisi hii na Taasisi nyingine za Umma kwani ninatambua kuwa bila kalamu zenu habari za Serikali haziwezi kufika kwa wananchi.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
TATHMINI YA KILELE CHA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA Kwa mujibu wa Hati Idhini ya Rais ya Mgawanyo wa
Majukumu ya Wizara iliyotolewa kupitia Tangazo la Serikali Na. 534 la tarehe 02
Julai, 2021; Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
(OR MUUUB) pamoja na majukumu mengine, imepewa jukumu la kusimamia
utendaji kazi katika Utumishi wa Umma. Usimamizi wa utendaji kazi katika
Utumishi wa Umma ni uzingatiaji wa Sera ya Menejimenti na Ajira Katika
Utumishi wa Umma (2008), Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298, Kanuni za
Utumishi wa Umma (2022), Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma (2009)
na Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Na. 3 wa Mwaka 2024 kuhusu
Utekelezaji wa Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa
Umma.
Ndugu Wanahabari
Katika kutekeleza majukumu yaliyobainishwa katika Hati
Idhini, Ofisi hii imekuwa na utamaduni wa kutekeleza kwa vitendo W iki ya
H uduma kwa M teja ambayo hua dhimishwa kuanzia tarehe 6 hadi 1 0 Oktoba kila
mwaka . Kwa upande wa Utumishi wa Umma Waajiri na watumishi wa umma
nchini wameendelea kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wateja wa
ndani na nje ya taasisi za o kwa viwango vya kuridhisha.
Tathmini iliyofanyika na Ofisi hii imebaini kuwa Waajiri na watumishi wa umma
wameweza kutekel eza dhima na malengo ya W iki ya H uduma kwa M teja kwa
viwango vya kuridhisha. Nichukue fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza.
Kwa upande wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliendelea kutoa huduma kwa wateja kwa kuzingatia Maadili ya Msingi iliendelea kutoa huduma kwa wateja kwa kuzingatia Maadili ya Msingi ((Core ValuesCore Values) za Ofisi hii ambazo ni Mteja Kwanza, Uzalendo, Uadilifu na Ubora. Aidha jumla ya wateja 312 312 waliwafikia na kuhudumiwa na Viongozi na watumishi na Viongozi wa Ofisi hii. Tathmini inaonesha idadi kubwa ya watumishi waliofika katika kipindi hicho, walikuwa na uhitaji wa kupata huduma mbalimbali zinazohusu masuala ya usimamizi wa utendaji kazi matumizi ya Mfumo wa Umma (PEPMIS/PIPMIS) .




Comments
Post a Comment