WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUWA MFANO WA KUIGWA
Mjumbe wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Betty Mkwasa, akifungua Mkutano wa Uelimishaji na Mashauriano Juu ya Utoaji wa Huduma za Mawasiliano kwa Mkoa wa Dodoma. Mkutano huo umefanyika leo ambapo aliwashauri wanahabari kuwa kioo cha jamii, alisema haiwezekani kuwa mwanahabari ndiyo uwe mtu wa kuvaa hovyo, tabia mbaya kutozingatia taratibu za utendaji kazi. "Mwandishi wa habari ni lazima vaa yako ufahamu kwamba kuna mavazi ya kwenda kwenye kazi za usiku na mavazi ya mchana. Haiwezekani mwandishi unaenda kulipoti matembezi ya hisani ukavaa tai na viatu vya mchuchumio au ukaenda kwenye mkutano wa kitaifa au kimataifa ukavaa mavazi ya michezo." Aidha habari zote aliomba kuhakikiwa kila sehemu husika kabla ya kurushwa zizingatie taaluma ili kuepusha kudharaulika kwa taaluma ya habari. Mkutano huo uliwashirikisha wamiliki wa mitandao,redio za mitandaoni na Televisheni, Blogs . Aidha Maofisa wa Mamlaka ya mawasiliano nchichi(TCRA), wali...