MBUNGE ACHACHAMAA KUHUSU SOKO LA HISA DAR ES SALAAM
Mbunge Hawa Mwaifunga, akichangia maoni yake katika semina iliyowahusisha viongozi wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) na baadhi ya makampuni yaliyomo kwenye soko hilo na kutaka fedha zake alizowekeza miaka kumi iliyopita arejeshewe kwani haoni faida ya kuwekeza kwenye baadhi ya makampuni.
Akichangia huku akishangiliwa na wabunge alisema miaka kumi iliyopita aliwekeza zaidi ya Sh milioni 10 Kampuni ya Vodacom Tanzania lakini chakushangaza alikuja kulipwa sh. lakini mbili (200,000) baada siku nyingi kupita tofauti na matarajio yake.
"Bora ningeenda kuwapatia wapigakura wangu kuliko kuwekeza huku sioni faida yake kama mtakuwa mkifanya hivi mtakuwa hampati wa kuwekeza fedha zao nakuomba mwenyekiti nije kuchukuwa fedha zangu kwako sasa hivi ,"alisema hayo huku akimuomba mwenyekiti wa kikao hicho ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge Mashimba Mashauri Ndaki aende kuchukuwa fedha zake alizowekeza kwenye soko hilo.
Hata hivyo Mkuu wa Idara ya Fedha na Masoko wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Hemed Masumai,amewatoa wasiwasi wabunge kwa kuwaeleza kuwa tofauti na awali hivi sasa kampuni hiyo ipo katika wakati mzuri wa kibiashara.
Mbunge Paul Makonda ambaye pia ni Waziri, akichangia na kutahadharisha kuhusu soko hiloNaibu Spika wa Bunge, Daniel Silo (kulia), akiwa sambamba na wabunge akisikiliza michango ya wabunge
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Kafiti William Kafiti, akitoa maoni yake katika semina hiyo.Mbunge wa jimbo la Muleba Kusini, Dkt. Oscar Ishengoma Kikoyo, akichangia maoni yake kwenye semina hiyo
Mbunge wa Jimbo la Butiama, Dkt. Wilson Mahera Charles, akichangiaMwenyekiti wa Semina hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti, Mashimba Ndaki, akiwatuliza wabunge kuhusu soko hilo na kuwaomba kuwekeza huko kwani Dunia ya sasa ndiko inakoelekea wao wasijitenge na ulimwengu huo wa kisasa
Comments
Post a Comment