MOI SASA MATIBABU YA KISASA TUPU BALOZI DKT. MPOKI

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa utoaji wa tiba bora, uwepo wa wataalamu wabobezi pamoja na matumizi  kupitia QR Code, unaolenga kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali. Amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma leo.

Aidha, amesema Kuwa baada ya mgonjwa kuweka miadi, mfumo wa MOI utaonyesha taarifa za mgonjwa, daktari anayetarajiwa kumuona pamoja na kliniki na muda wa huduma, hivyo kupunguza muda wa kusubiri hospitalini.

Aidha akibainisha Kuwa mfumo huo umeanzishwa kutokana na changamoto ya msongamano, ambapo historia wagonjwa walikuwa wakifika hospitalini saa 10 za alfajiri na kusubiri hadi saa 8 mchana ili kuonana na daktari.

Pia, ameseme kuwa mfumo huo utawawezesha wagonjwa kufika katika muda waliopangiwa na kuendelea na shughuli nyingine, badala ya kutumia muda mrefu kusubiri huduma hospitalini.

Mkurugenzi huyo amesema katika mwaka wa fedha 2025/26 MOI imehudumia jumla ya wagonjwa 211,389, wakiwemo 202,000 waliokuja kupata huduma bila kulazwa na takribani 10,000 waliolazwa.

Ameongeza kuwa MOI imeendelea kuboresha huduma za mifupa na mfumo wa fahamu kwa kutumia teknolojia za kisasa, huku sasa ikikidhi asilimia 98 ya mahitaji ya wagonjwa wa mifupa, misuli na majeraha na asilimia 97 ya wagonjwa wa mfumo wa fahamu.

Aidha, MOI imeendelea kuboresha tiba ya kiharusi kwa kutumia Biplane Angiography (Cath Lab), huduma za kubadilisha nyonga na magoti, upasuaji wa magoti kwa kutumia matundu pamoja na huduma za maumivu sugu.

Ameongeza kuwa katika mwaka 2025,2026 idara ya radiolojia ilifanya vipimo takribani 84,000, huku kitengo cha physiotherapia kikihudumia wagonjwa 72,000, ikiwa ni sehemu ya juhudi za taasisi hiyo kuendelea kuboresha huduma kwa wagonjwa.






Wanahabari wakimsikiliza Mkurugenzi huyo leo







 

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA