Posts

SPIKA ZUNGU ASIFU UBUNIFU WA VIJANA WA MKENDA ATAKA MAMILIONI YA RAIS SAMIA YAWAFIKIE NA WAO

Image
Spika wa Bunge Mussa Azzan Zungu (kulia), akizungumza na vijana wabunifu kutoka vyuo Vya Nelson Mandela, Chuo Kikuu Mbeya, Dar Tech na Costech , Spika amemsifia Profesa Mkenda kwa kuwatia moyo wabunifu hao ambao sasa watakuwa tegemeo kwa Taifa. Ameitaka Serikali  muda umefika sasa wabunifu hawa kusaidiwa kuendeleza ubunifu wao na fedha zinazotolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan zitumike kuendeleza ubunifu wao ambao utakuwa na manufaa kwa nchi, Taasisi za Ndani na Nje ya nchi ziwaangalie kwa macho mawili kusambaza ubunifu huu. Maonyesho hayo yanafanyika viwanja vya bunge jijini Dodoma. Profesa Mkenda amesema vijana hao wataendelezwa kwa hali na mali ili Taifa lijivunie ugunduzi wao Mbunge Amos Maganga, akiangalia bidhaa za wabunifu  Akizungumza na wanahabario baada ya kutembelea mabanda ya wabunifu hao

KAMA RAIS AMEANZA KUBANA MATUMIZI WEWE NANI-------SPIKA ZUNGU

Image
Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu, akiwasomea wabunge waraka kutoka kwa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, unaowataka watendaji wa Serikali kubana matumizi hususan ununuzi wa magari ya kifahari yenye bei kubwa  na mikutano kuwa na watendaji wengi ambao baadhi yao hawastahili kuwepo hapo.  Waraka huo unasema muda umefika sasa kutekeleza kwa vitendo kauri za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliposema atapunguza matumizi makubwa ya misafara yake ya magari  ambaye yeye amepunguza magari kwenye msafala wake, aidha hata kamati za bunge zinatakiwa kupunguza msululu wa watendaji wa Halmashauji wanofika kuhojiwa wafike  wasiopungua watano na siyo kama ilivyo sasa ambapo mkoa mmoja unapofika kamati za bunge, zingine zinawilaya zaidi ya tano zinakuwa na watedaji wengi kitu ambacho ni matumizi makubwa ya fedha za walipa kodi inafaa iepukwe kuanzia sasa. Aidha waraka unasema muda umefika sasa wa kujiepusha na ununuzi wa magari ya Sh milioni 500 sasa itabidi yanunuliwe yasiyozidi Sh m...

RAIS SAMIA NA MGENI WAKE WAWA KIVUTIO UZINDUZI WA MJI WA KISERIKALI MTUMBA.

Image
  Rais wa Jamhuri ya Angola,  João Manuel Gonçalves Lourenço ambaye akizungumza katika hafla  ya uzinduzi iliyofanyika  katika mji wa serikali Mtumba jijini Dodoma leo @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ RAIS  Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemtaka Katibu Mkuu Kiongozi kwa kushirikiana na makatibu wakuu kuhakikisha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya misitu katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma, yanapandwa miti na kutunzwa ili mji  uwe na mandhari ya kijani na kuvutia. Rais Samia Ametoa maagizo hayo leo wakati akisoma hotuba yake kwa  wananchi waliofika katika uzinduzi huo  na watumishi wa serikali baada ya kuzindua majengo ya ofisi za wizara na taasisi za Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, huku akiwashukuru wote waliohusika na utekelezaji wa miradi hiyo na kuwataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa bidii na ufanisi zaidi katika kuwahudumia  Watanzania. Pia amewataka Viongozi na watumishi wa umma kuhakikisha majengo, miundombinu, mazingi...

MKUTANO WA TANO KIKAO CHA KWANZA CHA BUNGE CHAANZA JIJINI DODOMA LEO

Image
Spika wa Bunge Mussa Zungu ,akiingia bungeni leo kuanzisha vikao vya bunge  jijini Dodoma, akiambatana na makatibu mezani wa bunge. Wabunge na Mawaziri wakiombea amani nchi kabla ya kuanza kikao huku nyimbo za Taifa na wa Afrika Mashariki ukipigwa Brasibendi ya Jeshi la Polisi ikipiga nyimbo hizo