RAIS SAMIA NA MGENI WAKE WAWA KIVUTIO UZINDUZI WA MJI WA KISERIKALI MTUMBA.

 

Rais wa Jamhuri ya Angola,  João Manuel Gonçalves Lourenço ambaye akizungumza katika hafla  ya uzinduzi iliyofanyika  katika mji wa serikali Mtumba jijini Dodoma leo

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@


RAIS  Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemtaka Katibu Mkuu Kiongozi kwa kushirikiana na makatibu wakuu kuhakikisha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya misitu katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma, yanapandwa miti na kutunzwa ili mji  uwe na mandhari ya kijani na kuvutia.

Rais Samia Ametoa maagizo hayo leo wakati akisoma hotuba yake kwa  wananchi waliofika katika uzinduzi huo  na watumishi wa serikali baada ya kuzindua majengo ya ofisi za wizara na taasisi za Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, huku akiwashukuru wote waliohusika na utekelezaji wa miradi hiyo na kuwataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa bidii na ufanisi zaidi katika kuwahudumia  Watanzania.

Pia amewataka Viongozi na watumishi wa umma kuhakikisha majengo, miundombinu, mazingira na usafi wa Mji wa Serikali Mtumba vinatunzwa vizuri ili mji huo uendelee kuwa na mandhari  yenye kuvutia.

Rais amebainisha  kuwa katika ramani ya eneo la Mji wa Serikali kuna maeneo yaliyotengwa kuwa maeneo ya kijani na kuotesha misitu ambayo pia yanagawa baina ya wizara na wizara, hivyo maeneo hayo yanapaswa kutunzwa na kuwa kijani kweli. “Kama kuna mvua au kuna jua lakini misitu ile iliyokusudiwa ipandwe na ionekane Dodoma iko kijani,” amesema

Aidha, ameitaka Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na mamlaka nyingine za Serikali, kuendelea kusimamia utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma wa mwaka 2019–2039 ili kuepuka ujenzi holela usiozingatia taratibu za mipango miji.

Aidha amebainisha kuwa usimamizi huo unapaswa kuzuia shughuli zisizoendana na matumizi yaliyopangwa ya ardhi na kulinda maeneo ya huduma za jamii, hifadhi za barabara na maeneo ya wazi dhidi ya uvamizi, akisisitiza umuhimu wa kuheshimu Mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma.

Aidha, ameongeza  kusema kuwa uendelezaji wa Jiji la Dodoma unahitaji ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, hivyo ameielekeza Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kwa kushirikiana na sekta nyingine kuendelea kuhamasisha na kuweka mikakati madhubuti ya kuvutia wawekezaji kuunga mkono jitihada za Serikali za kuendeleza jiji hilo.  

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA