KAMA RAIS AMEAZA KUBANA MATUMIZI WEWE NANI-------SPIKA ZUNGU

Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu, akiwasomea wabunge waraka kutoka kwa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, unaowataka watendaji wa Serikali kubana matumizi hususan ununuzi wa magari ya kifahari yenye bei kubwa  na mikutano kuwa na watendaji wengi ambao baadhi yao hawastahili kuwepo hapo.  Waraka huo unasema muda umefika sasa kutekeleza kwa vitendo kauri za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliposema atapunguza matumizi makubwa ya misafara yake ya magari  ambaye yeye amepunguza magari kwenye msafala wake, aidha hata kamati za bunge zinatakiwa kupunguza msululu wa watendaji wa Halmashauji wanofika kuhojiwa wafike  wasiopungua watano na siyo kama ilivyo sasa ambapo mkoa mmoja unapofika kamati za bunge, zingine zinawilaya zaidi ya tano zinakuwa na watedaji wengi kitu ambacho ni matumizi makubwa ya fedha za walipa kodi inafaa iepukwe kuanzia sasa. Aidha waraka unasema muda umefika sasa wa kujiepusha na ununuzi wa magari ya Sh milioni 500 sasa itabidi yanunuliwe yasiyozidi Sh milioni 100, baadhi ya watendaji serikali itabidi wakopeshwe magari kuepuka na matumizi makubwa 



















 

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA