SPIKA ZUNGU ASIFU UBUNIFU WA VIJANA WA MKENDA ATAKA MAMILIONI YA RAIS SAMIA YAWAFIKIE NA WAO

Spika wa Bunge Mussa Azzan Zungu (kulia), akizungumza na vijana wabunifu kutoka vyuo Vya Nelson Mandela, Chuo Kikuu Mbeya, Dar Tech na Costech , Spika amemsifia Profesa Mkenda kwa kuwatia moyo wabunifu hao ambao sasa watakuwa tegemeo kwa Taifa. Ameitaka Serikali  muda umefika sasa wabunifu hawa kusaidiwa kuendeleza ubunifu wao na fedha zinazotolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan zitumike kuendeleza ubunifu wao ambao utakuwa na manufaa kwa nchi, Taasisi za Ndani na Nje ya nchi ziwaangalie kwa macho mawili kusambaza ubunifu huu. Maonyesho hayo yanafanyika viwanja vya bunge jijini Dodoma. Profesa Mkenda amesema vijana hao wataendelezwa kwa hali na mali ili Taifa lijivunie ugunduzi wao



Mbunge Amos Maganga, akiangalia bidhaa za wabunifu








 Akizungumza na wanahabario baada ya kutembelea mabanda ya wabunifu hao

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA