DKT. NCHIMBI AHITIMISHA KAMPENI MKOA WA DODOMA.
Share MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo Oktoba 17, 2025, amehitimisha kampeni zake katika Mkoa wa Dodoma, ambapo maelfu ya wananchi walijitokeza kumsikiliza akiwasilisha sera na ahadi zilizomo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Katika ziara yake ya kampeni mkoani humo, Dkt. Nchimbi amefanya mikutano mikubwa katika wilaya za Mpwapwa, Kongwa, Kondoa na Dodoma Mjini, akisisitiza dhamira ya CCM kuendeleza utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta za afya, elimu, kilimo, maji na miundombinu, ikiwemo ujenzi wa barabara na reli ya kisasa (SGR) kutoka Dodoma–Kigoma na Dodoma–Mwanza, endapo wananchi watakipatia chama hicho ridhaa ya kuendelea kuongoza kwa miaka mitano ijayo. Amesema, Serikali ya CCM pia imepanga kukamilisha ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, pamoja na ujenzi wa uwanja mkubwa wa mpira wa miguu jijini Dodoma, ambao utatumika kwa mashindano ya AFCON 2027, ikiwa n...