SASA NI ZAMU YA SEKTA BINAFSI; SERIKALI YAPANDISHA KIMA CHA CHINI CHA MISHAHARA KWA SEKTA BINAFSI---- WAZIRI RIDHIWANI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete akitangaza kwa umma amri ya kuhusu kupandishwa kwa kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi nchini leo 17 Oktoba 2025 Dar es 

Kwa mujibu wa sheria za Kazi zinazotoa mamlaka ya kutangaza Kima Cha Chini Cha Mshahara wa sekta binafsi, leo nimetangaza ongezeko la Kima Cha Chini Cha Mshahara kwa sekta binafsi kuwa kimeongezeka kwa asilimia 33•4 ambapo sasa kima Cha Chini kimeongezeka toka Shilingi 275,060 mwaka 2022 hadi Shilingi 358,322 mwaka 2025.

Zoezi hili ambalo ufanyika kila baada ya miaka mitatu, ni hatua nyengine kufuatia kukamilika kwa tamko la kima cha chini cha Mshahara kwa watumishi wa umma ambapo Serikali imepandisha mishahara kwa asilimia 35•1 ambapo sasa kima cha chini cha mishahara kuwa Shilingi 500,000 kama ilivyotangazwa na Dr. Samia Suluhu Hassan , Rais wa JMT wakati wa kilele cha Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani. Hii ni alama nyengine ya mafanikio katika kuimarisha ustawi wa wafanyakazi Tanzania.





 

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA