MWENYEKITI MWANYIKA APONGEZA TBS NA CAMARTEC
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Jafo (kulia), akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Deodatus Mwanyika, alipokuwa akifungua kikao cha Idara mbili za Wizara yake ambazo ni Shirika la Viwango nchini (TBS) na Kituo cha Uzalishaji zana za Kilimo Vijijini (CAMARTEC Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Deodatus Mwanyika, akifungua kikao hicho, ambapo alizipongeza taasisi hizo ambazo zinagusa maisha ya moja kwa maja ya wananchi wa Tanzania na kuwaomba watendaji wake kuwa makini zaidi kusikiliza malalamiko ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi kwa haraka, ili kumsaidia Rais DKT, Samia Suluhu Hassan, ambaye moyo wake ni kuona wananchi wanapata huduma zilizo bora. · Mkurugenzi wa Shirika la Viwango nchini (TBS) Dkt. Ashura A. Katunzi, akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti huyo Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uzalishaji zana za Kilimo Vijijini ...