MWENYEKITI MWANYIKA APONGEZA TBS NA CAMARTEC
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Jafo (kulia), akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Deodatus Mwanyika, alipokuwa akifungua kikao cha Idara mbili za Wizara yake ambazo ni Shirika la Viwango nchini (TBS) na Kituo cha Uzalishaji zana za Kilimo Vijijini (CAMARTEC Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Deodatus Mwanyika, akifungua kikao hicho, ambapo alizipongeza taasisi hizo ambazo zinagusa maisha ya moja kwa maja ya wananchi wa Tanzania na kuwaomba watendaji wake kuwa makini zaidi kusikiliza malalamiko ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi kwa haraka, ili kumsaidia Rais DKT, Samia Suluhu Hassan, ambaye moyo wake ni kuona wananchi wanapata huduma zilizo bora.
· Mkurugenzi wa Shirika la Viwango nchini (TBS) Dkt. Ashura A. Katunzi, akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti huyo
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uzalishaji zana za Kilimo Vijijini (CAMARTEC, Godfrey Mwinama, akiwasilisha maelezo yake kwa wabunge
Maofisa wa Taasisi hizo wakiwa katika kikao hicho
Maofisa wa TBS wakiwa kikaoni
Mjumbe wa Kamati hiyo Profesa Ishengoma ,akifatilia hotuba kwenye kishikwambi chake
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uzalishaji zana za Kilimo Vijijini (CAMARTEC, Godfrey Mwinama, akiwasilisha maelezo yake kwa wabunge
Mwenyekiti Mwanyika akisisitiza jambo
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo, akihitimisha kikao hicho kwa wabunge kwa majadiliano mazuri na Taasisi za wizara yake
Comments
Post a Comment